Mkasa wa kweli: ungefanyeje?

Mkasa wa kweli: ungefanyeje?

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
1,002
Reaction score
2,286
Mimi ni mwanamke
Nipo kwenye mahusiano ya kuishi pamoja kupika na kupakua na mwanaume Mwenye miaka 45 kwa muda wa miaka 3 Huku tulipanes Mipango yakuoana. Wakat tunaanza alidai Ana watoto 2 (ke na me) mama tofauti ila hajawaoa. Na mtoto mkubwa anaishi na shangazi yake. Anadai alichelewa kuoa kutokana na ugumu wa maisha aliyokulia na pia alihaso sana hadi Leo kufikia alipo.

Kuna kipindi niliwahi kupata tetesi kwamba améoa ila alikataa katakata. Juzikati alipata msiba wa moja ya mzazi wake ikabidi aende ila alikataa mimi nisiende. Baada yayeye kuondoka nikapanga Safari nikamfwata ila nilipofika stand akanipotezea hakuja kunipokea.

Niliamua kutumia mbinu zangu hadi kufika kwao na kukuta msiba.
Nilishangaa kukuta ameoa tena ndoa ya kanisani. Tulipokaa na kuzungumza alijitetea kwamba walishaachana kwa kuwa hawakuwa na maelewano na ni kama ndoa haikuwepo. Walishasuluhishwa ikashindikana. Ila Bado mwanamke alikuwa hajahamisha Mali zake kutoka kwenye nyumba ya mwanaume (aliikuta alipoolewa).
Pía alijitetea alinificha kwa kuwa aliogopa nitamwacha.

Mipango iliyopo: amesema anatoa talaka kisha mengine yaendelee kama yalivyopangwa.
Sasa wazoefu na wasio wazoefu naomba mnishauri nifanyejee?? Maana siko vizuri.

Nyongeza:
Tuliwekwa kikao mimi yeye mkewe na ndugu zake. Nikamuuliza alikuwa wapi mbona ckuwahi kumsikia Hata cku moja wala kumuona? Mkewe alikiri kutokuwa vizuri na mumewe na pía ashapata mwingine. Na watu wote walikiri kwamba ile ndoa kiuhalisia ilibaki vyeti. Na ndio wakashauri talaka ili kila mtu awe huru.
Bwana ameomba msamaha sana na anatishia Hata kujiua.
 
Mrs Bishanga,
wa kwako hyomkufa nae angekua hakutaki siku nyingi sana angeshakuacha..........................na uzee huo utaenda kumchukua nan saa hzi😉😀😀
 
Pole kwa mkasa,,, fanya hivi usimuache saiv maana upo kwenye mshtuko endelea nae huku ukitibu jeraha lako, ukijiona umepona mbwage
Asante kwa ushauri. Ngoja niwasikilize na wengine.
Tuliwekwa kikao mimi yeye mkewe na ndugu zake. Nikamuuliza alikuwa wapi mbona ckuwahi kumsikia Hata cku moja wala kumuona? Mkewe alikiri kutokuwa vizuri na mumewe na pía ashapata mwingine. Na watu wote walikiri kwamba ile ndoa kiuhalisia ilibaki vyeti. Na ndio wakashauri talaka ili kila mtu awe huru.
Bwana ameomba msamaha sana na anatishia Hata kujiua.
 
Asante kwa ushauri. Ngoja niwasikilize na wengine.
Tuliwekwa kikao mimi yeye mkewe na ndugu zake. Nikamuuliza alikuwa wapi mona ckuwahi kumsikia Hata cku moja wapa kumuona? Mkewe alikiri kutokuwa vizuri na mumewe na pía ashapata mwingine. Na watu wote walikiri kwamba ile ndoa kiuhalisia ilibaki vyeti. Na ndio wakashauri talaka ili lila mtu awe huru.
Haya maelezo yaongeze hapo juu, na kama mliita na kikao na ukashuhudiwa kuwa wako na migogoro yao na mke akakiri kuwa kashapata mtu mwingine,,, subiri talaka itoke uolewe

kwenye uchumba wenu utakuwa ushamuona ni mtu wa aina gani ye kutoelewana na mkewe wa kwanza haimaanishi hata wewe hutoelewana nae,,,
 
Una umri gani??
Kwanini alikuficha kama kweli hawako wote mpaka ukaupata ukweli mwenyewe?
Kwa uelewa wangu mdogo ndoa za kikristo hazina talaka ila kama wakienda mahakamani wanaweza pata (nadhani).
Kwanini akufiche wakati ilikua rahisi kusema tu ameoa hawako on good terms watapeana talaka...?
Inakuingia akilini kua mkewe ana mahusiano mengine lakini hajahamisha mali kwa mumewe?
Wewe ndo unamjua huyo bwana na mazingira yq mahusiano yenu lakini there's something fishy hapo.
Achia ngazi live without him. It's never late to save yourself from a heart break (which I think is already broken). Hapo sioni ndoa aiseee kama vipi kubali kua hawara mchezo uishe.
Mengine watakushauri wahenga humu.
 
Kwa majibu haya, wewe ndiye mke wake.

Achana na habari zingine, utaenda kuteseka bure na utajutia kumuacha mume anayekupenda.

Amini usiamini, hata ukimuacha ataoa mwingine. Hawezi kuishi na huyo aliyebakia mke wa kwenye makaratasi.

Kaa, tulia mlee familia. Shukuru kwa kuwa umepajua kwao kiufasaha na ukweli umejua.

Basi ngoja niishie hapa.

Asante kwa ushauri. Ngoja niwasikilize na wengine.
Tuliwekwa kikao mimi yeye mkewe na ndugu zake. Nikamuuliza alikuwa wapi mona ckuwahi kumsikia Hata cku moja wapa kumuona? Mkewe alikiri kutokuwa vizuri na mumewe na pía ashapata mwingine. Na watu wote walikiri kwamba ile ndoa kiuhalisia ilibaki vyeti. Na ndio wakashauri talaka ili lila mtu awe huru.
 
meghan markle,
Amante kwa kutumia mda wako kunipa ukweli. Huyo mwanamke niKweli haishi humo kwakuwa Hata kazi anafanyia mbali na hapo kwa mumewe. Me binafsi ninachoumia ni ile kuficha ukweli wa jambo zito kiasi hicho.
Kweli niko heartbroken. Nadhani nikipona naweza amua otherwise.
 
Nimeshaongeza
Haya maelezo yaongeze hapo juu, na kama mliita na kikao na ukashuhudiwa kuwa wako na migogoro yao na mke akakiri kuwa kashapata mtu mwingine,,, subiri talaka itoke uolewe

kwenye uchumba wenu utakuwa ushamuona ni mtu wa aina gani ye kutoelewana na mkewe wa kwanza haimaanishi hata wewe hutoelewana nae,,,
 
True that hakutakiwa kukuficha.... Anyways maamuzi unayo wewe.
Ila daaah ningekua mimi nilivyosensitive na kamoyo kangu ningempa ultimatum.
Aamue aanze kuprocess divorce na wewe uone kabisa kua anashulika na divorce ama usepe zako. Miaka mitatu mko wote alikua anasubiri nini kupata divorce hadi ugundue ndo ajibaraguze hivyo?
(Kumbuka divorce itamcost maana kuna kugawana mali na mkewe labda ndio anacho ogopa)
All the best
Amante kwa kutumia mda wako kunipa ukweli. Huyo mwanamke niKweli haishi humo kwakuwa Hata kazi anafanyia mbali na hapo kwa mumewe. Me binafsi ninachoumia ni ile kuficha ukweli wa jambo zito kiasi hicho.
Kweli niko heartbroken. Nadhani nikipona naweza amua otherwise.
 
Hakuna cha kukushauri maana wewe ni mzinzi na huyo mke wake anatakiwa akukamate ugoni.
 
Amante kwa kutumia mda wako kunipa ukweli. Huyo mwanamke niKweli haishi humo kwakuwa Hata kazi anafanyia mbali na hapo kwa mumewe. Me binafsi ninachoumia ni ile kuficha ukweli wa jambo zito kiasi hicho.
Kweli niko heartbroken. Nadhani nikipona naweza amua otherwise.
Kwa hili kuficha ni amekosea, msamehe

Lakini yawezekana ni kwasababu mgogoro ulikuwa haujafikia talaka na pengine alihofia kukwambia utamuacha,, lakini kukubali mkaweka kikao na mtalaka wake mtarajiwa basi ni wazi anakupenda

Kukuficha ni kuchanganyikiwa huku home kimenuka arudi kwako baby wake akuelezee dah kiubinaadamu kuna hali ya kusema acha nimalize hili ndo nimwambie sasa
 
Nilisisitiza talaka pia. Na kama akipotezea ntamuacha nitakapopata nguvu. Mali añadai hawakuchuma chochote pamoja maana amani ilidumu kwa mwaka mmoja tu baada ya hapo maruerue. Vitu vyote alivikuta
True that hakutakiwa kukuficha.... Anyways maamuzi unayo wewe.
Ila daaah ningekua mimi nilivyosensitive na kamoyo kangu ningempa ultimatum.
Aamue aanze kuprocess divorce na wewe uone kabisa kua anashulika na divorce ama usepe zako. Miaka mitatu mko wote alikua anasubiri nini kupata divorce hadi ugundue ndo ajibaraguze hivyo?
(Kumbuka divorce itamcost maana kuna kugawana mali na mkewe labda ndio anacho ogopa)
All the best
 
Sikia dada yangu,huyo ni mmeo wala usihofie ule uongo. Kuna wakati wanaume huwa tunalazimika kudanganya baada ya kujua huyo mtu uliyenaye anataka kusikia nn! Yaani km mwanamke nampenda,na nnajua kuna vitu hapendi nitasema uongo kwenye hiyo category. Nikuhakikishie huyo mtu wala usihangaike na talaka,talaka ni makaratasi tu,mtakuwa mnachelewa tu kuanza kutengeneza familia. Kumbuka ndoa ya kanisani haina talaka. Mimi nilioa mwaka 1997,lkn kufikia mwaka 2005 ndoa yangu ilikuwa jehanam. Lkn nilivumilia kulinda heshima ya watoto wangu. Mwaka 2008,nilipata mtu na nikaanza naye urafiki nikiwa ndani ya ndoa. Sikuwa nimemuacha mke wangu,na muda mwingi niliutumia sana kwa mke wangu ingawa ukweli ndoa haikuwepo. Mwaka 2010 nikabahatika kupata mtoto na huyo rafiki yangu,huyu wa ndoa hata kujamiiana tulikuwa tumeacha. Tulibaki hivyo,na hakujua km nimezaa nje na nilikuwa kila ijumaa jioni naenda kwa mpenzi wangu narudi jpili. Mwaka 2013 niliumwa jicho na kufanyiwa upasuaji,nilikuwa nahitaji mtu mwenye upendo nami kunihudumia. Hapo ndo ulikuwa mtihani. Nilichagua kwenda kwa mke wangu wa ndoa baada ya kutoka hospital. Lkn kilichonipata Mungu anajua,siku 3 baadae nikaita taxi nikatimkia Kwa mpenzi wangu. Na siku iliyofuata nikampigia simu mke wangu nikaweka wazi uhusiano wangu na kwamba tayari tulikuwa na mtoto wa miaka 3. Hakuweza kustahimili zile taarifa,kesho yake akapeleka canter akabeba kila kitu cha ndani na watoto wangu akawaacha hapo. Sikumfanya chochote,kesho yake nikaenda keko nikanunua fenicha zote mpya. Na maisha yanaendelea na yule aliyekuwa mpenzi wangu,ndo mke wangu hadi leo. Na huwezi amini yaani hapa naona km nimekutana naye jana tu. tunapendana ile mbaya na tayari tuna mtoto mwingine now ana miaka 4. Baada ya maelezo haya marefu,leo ukienda usirudi tena kule kwako..
 
Back
Top Bottom