Mkasa wa kweli: ungefanyeje?

Mkasa wa kweli: ungefanyeje?

Mimi sipendi watu wanotishatisha, kama bado hajajiua mwambie ajiue bwana.. mimi mwenyewe nakutamani uwe mrs Daddo tujenge maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kuachana kuna mengi sana but always huwa naamini nguzo kuu ya mahusiano huwa ni ukweli.Truth will always set you free. Hapo mpatie mda akamilishe mambo yake let's say mwaka mmoja but mpe condition bila kukamilosha talaka hakutakuwa na future kati yenu. Kuachana ktk ndoa kuna vitu vingi sana vilivyopelekea mpk watu wakaachana let's not dig into the past jamani
Kama kaamua kuwa na wewe mpatie Nafasi. Mpatie mda akamilishe mambo yake meanwhile endelea na mambo mengine ya kimaendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amante kwa kutumia mda wako kunipa ukweli. Huyo mwanamke niKweli haishi humo kwakuwa Hata kazi anafanyia mbali na hapo kwa mumewe. Me binafsi ninachoumia ni ile kuficha ukweli wa jambo zito kiasi hicho.
Kweli niko heartbroken. Nadhani nikipona naweza amua otherwise.

1. Ndoa yao kiuhaliasia imevunjika na wewe umethibitisha hilo.

2. Mnaishi pamoja kwa miaka mitatu kinadharia wewe ndo mke wake.


Sababu inayokuumiza ni moja tu, kwamba alikuficha ama tuseme umechelewa kufahamu maana ungefahamu tu.

Kama utamuacha, jua ya kwamba umemuacha kwa sababu ya kukucheleweshea ukweli wa jambo nyeti.
 
Mimi ni mwanamke
Nipo kwenye mahusiano ya kuishi pamoja kupika na kupakua na mwanaume Mwenye miaka 45 kwa muda wa miaka 3 Huku tulipanes Mipango yakuoana. Wakat tunaanza alidai Ana watoto 2 (ke na me) mama tofauti ila hajawaoa. Na mtoto mkubwa anaishi na shangazi yake. Anadai alichelewa kuoa kutokana na ugumu wa maisha aliyokulia na pia alihaso sana hadi Leo kufikia alipo.

Kuna kipindi niliwahi kupata tetesi kwamba améoa ila alikataa katakata. Juzikati alipata msiba wa moja ya mzazi wake ikabidi aende ila alikataa mimi nisiende. Baada yayeye kuondoka nikapanga Safari nikamfwata ila nilipofika stand akanipotezea hakuja kunipokea.

Niliamua kutumia mbinu zangu hadi kufika kwao na kukuta msiba.
Nilishangaa kukuta ameoa tena ndoa ya kanisani. Tulipokaa na kuzungumza alijitetea kwamba walishaachana kwa kuwa hawakuwa na maelewano na ni kama ndoa haikuwepo. Walishasuluhishwa ikashindikana. Ila Bado mwanamke alikuwa hajahamisha Mali zake kutoka kwenye nyumba ya mwanaume (aliikuta alipoolewa).
Pía alijitetea alinificha kwa kuwa aliogopa nitamwacha.

Mipango iliyopo: amesema anatoa talaka kisha mengine yaendelee kama yalivyopangwa.
Sasa wazoefu na wasio wazoefu naomba mnishauri nifanyejee?? Maana siko vizuri.

Nyongeza:
Tuliwekwa kikao mimi yeye mkewe na ndugu zake. Nikamuuliza alikuwa wapi mbona ckuwahi kumsikia Hata cku moja wala kumuona? Mkewe alikiri kutokuwa vizuri na mumewe na pía ashapata mwingine. Na watu wote walikiri kwamba ile ndoa kiuhalisia ilibaki vyeti. Na ndio wakashauri talaka ili kila mtu awe huru.
Bwana ameomba msamaha sana na anatishia Hata kujiua.

Wewe ndo huyo kwa picha?
 
Ndoa ni ya kikristo au kiislam, kama jibu ni la kwanza changanya lapa kama ni la pili basi subiri talaka uoane nae.
 
Back
Top Bottom