Mkasa wa Kweli Uliomkuta Kigogo wa Serikali Aliyetumbuliwa Baadaye Kutimuliwa na Mkewe

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
729
1,000
Mume amepewa jina la Mopao ( sio jina halisi)
Mke amepewa jina la Mopa (sio jina halisi)

Mkasa wa Kweli Uliomkuta Kigogo wa Serikali Aliyetumbuliwa Baadaye Kutimuliwa na Mkewe.

Mkasa wa kusikitisha unaomuhusisha Kigogo mmoja aliyeishi maisha mazuri kwa kuitumikia Serikali moja barani Afrika.

Kigogo huyu almaarufu Mopao aliishi na mkewe almaarufu Mopa waliishi maisha ya furaha wakijaaliwa kupata Watoto wawili.

Mungu aliwabariki wote hao kwa nyadhifa nzuri, Mopao akiwa Mkurugenzi Serikalini huku Mopa akihudumu kwenye Taasisi nyeti ya Kifedha akiwa Mwanasheria.

Wanandoa hao waliishi kwenye nyumba ambayo Mke alipewa na Taasisi ya Kifedha aliyofanyia kazi.

Maisha yalibadilika ghafla kufuatia Mopoa kutumbuliwa kazini. Serikali ya nchi hiyo ilishaamua kurejesha nidhamu kwa Watumishi wa Umma!

Wanandoa hao waliendelea kuishi pamoja wakipambana na changamoto mbalimbali zilizotokana na Mume kukosa ajira!

Mume akihangaika kutafuta maisha huku akimtegemea Mkewe kwa makazi, malazi, matibabu, usafiri n.k

Kwa wastani Mopa alikuwa mkarimu na alimruhusu Mopao kutumia hata gari lake la kisasa kabisa.


Hata hivyo mambo yalibadilika tena baada ya siku moja Mopao kurejea nyumbani na kukuta mlango umepigwa kufuli huku nguo zake zikiwa zimetupwa nje.
Mopao aliamua kuvunja mlango na alipoingia ndani alikuta nyumba ikiwa tupu!

Mopa alishaamua kuhama na kukabidhi nyumba huku akiacha ujumbe wenye tuhuma lukuk


Kwamba alikiuka maadili ya ndoa kwa kuchepuka

Kwamba amekuwa akitumia kwa anasa mali za mkewe

Kwamba amekuwa mlevi mkubwa huku akitumia hela za Mkewe

Tuhuma zote hizo Mopao alizikanusha vikali sana huku akidai kukosa kipato ndiyo chanzo cha yote hayo!

Kama vile haitoshi Mopa alimshtaki Mopao Polisi kwa madai ya kuvunja mlango na kufanya uharibifu wa nyumba aliyopewa na Taasisi

Mopa alienda mbali zaidi kwa kufungua kesi mahakamani akidai taraka kutoka kwa Mopao

Ndugu yetu Mopao amechanganyikiwa, haelewi afanye nini, hajui aanzie wapi wala aende wapi


Mkewe alimfanyia hisani kwa kwa kumpatia Mumewe kiasi kidogo cha fedha akaanze maisha

Hatujui nani ni msemakweli ila Ndugu yetu Mopao amechanganyikiwa, haelewi afanye nini, hajui aanzie wapi wala aende wapi


Nitumie fursa hii kuwaomba tumshauri mwenzetu aliye kwenye uhitaji mkubwa wa faraja.Aksanteni
 

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
3,082
2,000
Usikute mleta uzi alikuwa staff mate wa mopao so anaeleza hapa as if wana JF tupo naye ofisi moja tunamjua

MY TAKE
Mleta uzi acha ukuda maisha hayana formula usipende toa ushuhuda maisha ya watu pigania maisha yako.
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,378
2,000
In maana Mopao alipokuwa mtumishi hakuwekeza?...au analilia penzi?

Mwanamke mwenye mapenzi ya kweli ni mama, hao wengine wanaweza badilika hata kama umeishi nae ndani miaka 30!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom