Mkasa wa kweli: Kazi za ndani nchini Oman zilivyonikutanisha na kifo

hii story inaweza ikawa inawakilisha hali halisi ya maisha ya Oman tu lakini si ya kweli hata kidogo ni ya kutunga..kwa namna mtiririko wake ulivyo na kama ni kweli msimuliaji jiandae kuna maswali utatakiwa utupe ufafanuzi baada ya simulizi yako kwisha...nafuatilia kwa makini
 
Kinondoni sweetheart ghafla Kanungila Karim

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Aseeeeh
SEHEMU YA 03



PAMOJA na kukarahishwa na maswali yaliyokuwa katika dhana halisi ya kibaguzi, lakini nilivyoingia tu ndani ya lile jumba, akili yangu ikahamia kwenye mandhari ya mule ndani. Niwe mkweli, tangu nizaliwe hadi leo hii, sijawahi kuona sebule nzuri kama lile la jumba la kifahari la tajiri Abdallah Mustapha lililopo Suwaiq nje kidogo ya Jiji la Muscut nchini Oman.
Macho yangu yalikuwa hayatulii, niligeuza shingo huku na kule, nikivutiwa na fenicha ghali zilizokuwa mule ndani. Nilikuwa mtulivu wakati Marimu akifanya mazungumzo na yule msichana wa Kiarabu utaratibu wa mkataba wangu.
“Shika hii,” yule msichana wa Kiarabu alinipa karatasi.
“ Agripina Soma vizuri huo mkataba wako wa kazi mama, kisha tia saini hapo chini, ” Mariamu ambaye alikuwa kama wakala wangu alishadadia baada ya kuwa nimepokea karatasi ile.
Nilipitia ule mkataba ulioandikwa kwa Lugha ya Kingereza. Pamoja na kwamba sijui lolote kuhusu mambo ya sheria, hasa sheria za mikataba ya ajira. Nilihisi tu, mkataba ule ulikuwa na mapungufu fulani ambayo nashindwa kuyabainisha hapa moja kwa moja.
Nilipo gota kwenye nukta ya mwisho ya mkataba ule, sikuamini nilipoona nitalipwa kiasi cha Riyal 100 ambayo kwa pesa za kwetu ilikuwa ni karibu shilingi laki sita na ushee.
Yanii kufanya usafi, kuosha vyombo, kufua na kupika, hivyo tu. Nalipwa laki sita na ushee!!!
Niliona ni pesa nyingi nilizo takiwa kulipwa ukilinganisha na kazi nitakazokuwa nikifanya. Niliamini wakati wa kupunguza umasikini kwenye familia yangu ndiyo huo.
Sikutaka kuchelewa. Nilimwaga saini kwenye ile karatasi na nikawa nimeingia mkataba wa miaka miwili Kwa makubaliano ya kuongezewa mkataba endapo mwajiri wangu atakubaliana na utendaji wangu wa kazi.
Muda mfupi badaye, nilielekezwa mazingira ya jumba lile sanjari na kutambulishwa kwa wafanya kazi wenzangu wawili mmoja mwanamke aliyeitwa Fatuma emeke kutoka Liberia na yule mvulana wa Kisomali, ambaye nilitambulishwa kwa jina la Hussein Jabal, baada ya mambo hayo kukamilika Mariamu aliniaga:
“Mimi naondoka.”
“Sawa...Lakini kuna ajambo nilitaka kukuuliza Mariamu.”
“...kuhusu?”
“Kuhusu uvumi wa wasichana wa kazi kufanyiwa ushenzi wakiwa huku ikiwemo kubakwa.”
“Kubakwa!!!” Mariamu alishangaa.
“Ndio, kubakwa”
“Kubakwa ni sehemu ndogo sana ya changamoto zilizopo huku, kwanza ni jambo la kawaida tu, kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa tayari kuipokea hali hiyo pale itakapokutokea.” Mariamu aliongea kauli hiyo kiwepesi sana.

“Niwe tayari kubakwa pale hali hiyo itakapo tokea?”niliuliza nikiwa nimemkazia jicho.
“Siyo uwe tayari kubakwa...”
“Bali?”
“Uwe tayari kufanya mapenzi kwa hiyari.”
“Sijaja huku kufanya mapenzi na mtu wa aina yeyote. Lakini pia, sikuja huku ili ninyanyasike kwa namna yeyote ile Mariamu, hukunieleza mambo hayo kabla ya kupanda ndege, kwa nini unanigeuka?” nilisema kwa sauti kavu lakini yenye viashiria vya hofu kubwa.

“Ngoja nikupe siri moja...” Mariamu alisema. Kabla hajamaliza mara Zakia alitokea na kunitaka nianze majukumu yangu.
Mariamu aliniaga, akanipa miadi ya kuonana wakati mwingine. Nikabakia nikiwa na mashaka na wasiwasi moyoni.
Mashaka yalikuwa makubwa sana. Sikuwa na imani tena na Mariamu. Kama nilivyosema awali, mwanamke huyo nilimwona ni mtu aliyejaa hila usoni mwake, tangu siku ya kwanza aliponipokea uwanja wa ndege wa Muscat.
Siku hiyo, nilianza kazi kwa nidhamu na umakini. Mwenyeji wangu akiwa ni Fatuma Emeke msichana mweusi na mzuri wa umbo kutoka nchini Liberia.
Siku kadhaa nikiwa ndani ya ile nyumba ya kihafahari, kama mfanya kazi wa ndani (house girl) nilibaini jambo jipya.

Yule mwanamke wa kiarabu. Zakia Al Majidi mke wa Abdallah Mustapha alikuwa ni mke wa pili wa tajiri huyo ambaye alikuwa na watoto wawili wa kiume kutoka kwa mke wake waliokuwa wakiishi na mama yao katika mji wa Al Jibrih mashariki mwa Jiji la Muscut nchini Oman.
Niliendelea kufanya kazi nikiwa ni mtu mwenye mori na ari. Sikuwahi kukutana na matukio kama yalivyokuwa yakivumishwa nikiwa Tanzania. Ama nilivyokuwa nikihisi. Hapakuwa na mtu aliyewahi kunisumbua kimapenzi aidha kuninyanyasa kwa namna yoyote ile ingawa majivuno na ubaguzi wa rangi wa Bi Zakia, sikuwa napendezwa nao.
Nilimaliza mwezi mmoja salama, nililipwa mshahara wa kwanza vizuri bila tatizo lolote. Siku napokea pesa kama malipo ya kazi zangu lilikuwa ni jambo la furaha mno kwenye maisha yangu. Niliamini huo ndiyo muda wa kukamilisha ndoto zangu za kupunguza hali ya maisha duni kwenye familia yangu.
Hapa kuna jambo moja nimesahau kulieleza: Nimesahau kueleza kwamba, moja ya sheria ambazo ziliwekwa na Bi Zakia pale nyumbani kwake, dhidi ya wafanyakazi wa ndani ilikuwa ni kutotumia simu za mkononi. Hadi leo sijui yule Mwarabu kwa nini alituwekea sheria ya kijinga vile.
Nakumbuka Kila mwisho wa wiki, nilikuwa nikifunga safari hadi Muscut. Huko nilipiga simu nyumbani, nikawasiliana na na familia yangu. Lakini pia, nilikuwa nikiwatumia pesa kwa njia kama ‘mape-xpress’ ‘western union’ ‘telegram’ na kadhalika.
Katika kipindi chote cha maisha yangu ndani ya nyumba ya tajiri Abdallah Mustafa, mtu wa karibu kwangu alikuwa ni yule mvulana Hussein Jabal, raia wa Somalia. Ukiachilia mbali Fatuma ambaye alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu wa wa kike tuliyeshirikiana kwenye kazi zote za ndani. Ukaribu wangu na mvulana huyu ulitokana na uwezo wake wa kuzungumza Kiswahili.
Mbali na hilo, Hussein alikuwa ni mtu mcheshi na msikivu, Kila siku baada ya kazi, tulikaa kwenye bustani ya majani na kuzungumza mambo mengi, nilipata kuelewa mambo mengi kuhusu mtu yule. Hata yeye alijua mambo kadhaa kuhusu maisha yangu.
Ukaribu wangu na Hussein ulinifanya nimzoe. Kumzoea kukazaa hali ya kumuwaza kila wakati. Hali ile ya kumuwaza kila wakati, kukatengeneza hali nyingine ya kummisi hususani pale awapo mbali na mimi.
Taswira ya sura ya Hussein Jabal ilianza kuniganda kichwani mwangu. Sikutaka kujiongopea kabisa kwamba moyo wangu hauvutiwi na uso wenye pua ndefu, macho makubwa sanjari na meno yaliyojipanga vizuri mithili ya punje za muhindi.
Sikutaka kabisa kujifariji kuwa nafsi yangu haikuvutika na umbo kakamavu la yule mvulana.
Lakini hata hivyo, akili yangu haikuwa tayari kuukubali ukweli uliotoka moyoni mwangu, ukweli wenye viashiria vyote vya mapenzi kwa mvulana yule.
Nilijikumbusha na kujionya juu ya msukumo huo. Sauti moja kichwani iliniambia jiepushe na mapenzi, yatakuletea matatizo mapenzi, fuata kilichokuleta Agripina. Sauti hiyo ilikuwa ikigonga kichwa changu kama kengele, lakini pamoja na hilo, bado moyo wangu ulikumbwa na wazimu dhidi ya mvulana yule. Taa nyekundu ilikwisha waka moyoni.

UKITAKA YOTE NJOO WHATSAP NA ELFU MBILI YAKO TU NAMBA NI 0687750295,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom