Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,447
- Thread starter
- #221
Labda
Labda
Hahahahah
Sehemu ya mwisho ni lini??SEHEMU YA 12
Nilishukuru japo kwa hilo kwani niliona angalau sasa ndugu zangu watapata fursa ya kuona maiti yangu na kuzikwa kwenye ardhi ya nchi yangu, nafsi yangu haikuogopa kufa, ila kilichoniumiza ni kufa nikiwa na mtoto tumboni, hilo liliniliza machozi.
“Usilie Agripina ndivyo maisha yalivyo, hujafa hujaumbika” mtu mmoja mwenyeji wa Kigoma alinipa moyo.
“Silii kwa sababu ya hukumu, namlilia mwanangu aliye tumboni”
“Una mtoto tumboni?”
“Ndio.”
“Nafikiri huwezi kutumikia adhabu ya kifo hadi pale utakapokuwa umejifungua mtoto.”
“Labda ngoja tusubiri,” nilisema kinyonge huku matone ya machozi yakijikusanya kwenye macho yangu.
Siku, wiki na miezi ikayoyoma, niliendelea kuishi ndani ya gereza kama mfungwa ninayesubiri siku ya kutumikia adhabu yangu ya kifo. Wakati nikingoja siku ya hukumu pia tumbo langu lilizidi kuwa kubwa.
Siku moja nikafuatwa na askari magereza walikuwa kama sita, mikononi mwao walibeba bunduki. Walinizunguka huku wakionekana kuwa makini na mimi, mmoja miongoni mwao akanisogelea na kunieleza ilibaki wiki moja tu kabla ya kutumikia adhabu yangu ya kifo.
Nilihisi mate mepesi yakijaa mdomoni, pamoja na kwamba nilikuwa sina hofu dhidi ya kifo lakini kwa mara ya kwanza nikahisi mwili ukinisisimka, hofu ikanisambaa kifuani mwangu, taswira ya tukio la mtu kunyongwa likajitengenza kwenye akili yangu, kwa kweli niliogopa mno.
Walipoondoka wale askari, wafungwa wenzangu walinifuata na kuniuliza nilikuwa naambiwa nini. Niliwaeleza yote nilioambiwa na wale askari wa kiarabu, simanzi na hofu ilienea katika nyuso za wafungwa hasa Watanzania wenzangu ambao pia walihukumiwa kifo.
“Ndiyo maana wameanza kuwa makini na wewe, kuanzia leo unaweza usiwe na sisi tena ndani ya selo. Siku za mfungwa kunyongwa zikikaribia huwa anawekwa mbali na watu kwa imani kwamba anaweza kufanya lolote dhidi ya mtu yeyote ili mradi asife peke yake,” alisema mfungwa mmoja miongoni mwa waliokuja kunipa pole.
Saa kumi na mbili jioni nilijiwa tena na wale askari wenye bunduki, kama alivyonieleza yule mfungwa mwezangu nilihamishwa na kupelekwa katika selo ya peke yangu. Niliingizwa kwenye chumba kimoja kizuri ambacho kilikuwa na kila kitu cha thamani, chumba hicho kilikuwa ndani ya jela hiyo.
Sikujua mantiki ya kuingizwa kwenye chumba nadhifu ingawa wakati mwingine nilihisi hizo ni itifaki za kumkirimu mtu ambaye hukumu yake ya kifo ipo jirani, hata hivyo wakati mwingine nilipingana na fikra hizo kwa kuwa mwanzoni nilipohukumiwa kifo, sikufanyiwa ikhisani ya mambo haya.
Niliishi ndani ya chumba kile nadhifu, kila siku nikiletewa vyakula vizuri ambavyo nafikiri vingine sijawahi kuvila hadi leo ninaposimulia mkasa huu. Wiki ile moja ilienda harakaharaka, hatimaye siku ya hukumu ikafika.
Walikuja askari wenye bunduki na kunitoa nje ya chumba kile, nilifungwa minyororo miguuni, mnyororo huo ukaunganishwa na shingo yangu ukapita hadi mikononi, kisha nikavikwa soksi nyeusi usoni.
Nilishikwa bega kwa nguvu na askari mmoja miongoni mwa waliokuwa wamenizunguka huku mkono mmoja wa askari yule ukiwa umekamata silaha yake vizuri.
Akawa ananiongoza na kunipeleka mahali nisikokujua, mapigo yangu ya moyo yakawa yananidunda “duk duk duk” nikaanza kutokwa jasho mwilini, hofu ya kifo ikawa kubwa, hatimaye nikaanza kulia, machozi na kamasi vilinitoka ndani ya ile soksi nyeusi iliyofunika uso wangu. Hata hivyo hakuna aliyejali hilo..
Nilifikishwa ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na baridi kali kisha nikaondolewa ile soksi usoni, nikashangaa nilipojikuta nipo ndani ya mochwari, moyo wangu ukalipuka “paaa” niliogopa.
Ndugu msomaji hapa ngoja niseme kitu. Hakuna hukumu mbaya ambayo inavuruga saikorojia ya mtu kama hukumu ya kifo, kama wadau wa sheria watapata bahati ya kusoma maandishi haya ni vema wakafanyia marekebisho sheria hii katika taifa letu, kwani sheria hii inamtafuna binadamu kisaikolojia kabla ya kuitumikia.
Baadhi ya nchi za ulaya na Marekani, sheria ya hukumu ya kifo haipo kidogo na baadhi ya nchi za Afrika, lakini kwa bara la Asia bado sheria hii inaendelea kutesa saikolojia ya binadamu kwa kiwango kibaya sana.
Baada ya kujiona nipo ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti nilianza kuhisi kizunguzungu, maiti nyingi zilikuwa zimetapakaa chini huku zikiwa zimefunikwa kwa mashuka meupe, kulikuwa na harufu kama ya jiki (ile dawa ya kuondoa madoa), nikatambua hiyo ni dawa ambazo maiti zile zimedungwa kwenye miili yao ili pengine zisiharibike.
Nafsi yangu ikazidi kuzongwa na jinamzi la hofu baada ya kubaini kuwa kumbe na mimi dakika chache nitakuwa maiti kama zile zilizolazwa pale chini kisha nitachomwa sindano yenye dawa ambayo ina harufu ya jiki kisha nitalazwa chini na kufunikwa shuka jeupe nikingoja kuzikwa.
“Mlazeni juu ya kitanda” alisema daktari huku akivuta sumu kwa kutumia sindano kwenye kichupa kidogo.
Nilishikwa na askari wawili nikalazwa juu ya kitanda, nikawa nimelala chali, mtoto wangu aliyekuwa tumboni nikamsikia akichezacheza. Machozi yalinitoka.
“Tutaonana mbinguni kwa baba mwanangu, samahani kwa kutumikia adhabu yangu, Labda pengine ni sahihi tu kufa na mama yako. Kama usipokufa sasa utakufa baadae kwa Ukimwi ambao naamini tayari nimekwisha kuambukiza.”
Nilinong’ona huku nikisubiri kudungwa sindano yenye sumu hadi kufa. Nilimwona daktari yule akiinyanyua sindano iliyokuwa imejazwa dawa ya Tetrodotoxin ambayo ni sumu maalumu kwa kuulia watu waliohukumiwa kifo, akaibonyeza kidogo ile sindano, matone madogo ya sumu yakaruka angani, kisha akanisogelea pale kitandani nilipolazwa tayari mkononi akiwa amekamata sindano ya SUMU.
“Nina mimba jamani, msiniue,” nilisema huku nikilia, macho yangu yakimtizama mtu yule kwa huruma.
“Nina mtoto tumboni baba yangu niache tafadhali, usinichome sindano ya sumu,” niliendela kulalama, hakuna kilicho badilika. Mtu huyo hakuwa na muda na mimi, alionekana alikwisha zoea huruma zile. Kwahiyo jambo lile mbele yake ilikuwa ni kitu cha kawaida. Hakunijali kabisa hata usoni hakuniangalia.
Alitizama saa yake ya mkononi nikaona ameganda kwenye saa hiyo. Ni kama alikuwa akingoja muda fulani uwadie ndipo afanye kazi yake. Naam! hisia zangu zilikuwa sahihi, baada ya sekunde kadhaa akanigeukia tena na kunikabili:
“Mfungeni mikanda,” alitoa amri. Askari wenye bunduki wakaanza kufanya kazi hiyo. Pamoja na kwamba nilifumgwa minyororo kwenye mikono na miguu lakini nilifungwa tena mikanda.
Nikawa siwezi kufurukuta. Daktari yule alinisogelea tena akiwa na sindano mkononi, akanijia usawa wa shingo yangu kisha akaniinamia na kunidunga sindano ile ya sumu kwenye shingo yangu.
Nilifumba macho wakati tendo hilo linafanyika ingawa niliusikia uchungu wa sindano ile hasa wakati daktari anaibinya sumu ya Tetrodotoxin kuingia ndani ya mishipa ya mwili wangu.
Sekunde tatu zilitosha kunifanya nianze kuona maluweluwe, nikajiona napatwa na maumivu makali mwili wote, yalikuwa ni maumivu kama vile nababuliwa na moto, nikataka kupiga kelele mdomo nao ukawa mzito, mara povu zito likaanza kunitoka modomoni, damu ikanitoka puani .
Giza la ajabu likazikumba mboni zangu, muda mfupi badaye sikujua tena kilicho endelea duniani.
Toba!!
Nimekufa!!!.
Je mwanamke huyo alikufa? Usikose sehemu ya MWISHO ya mkasa huu wa kweli.
Anawachukulia mapunga!!mwandishi punga kweli anatuchukuliaje wasomajii
Wee jamaa umeshatoka Mirembe?mwandishi punga kweli anatuchukuliaje wasomajii
Huu mchanganyiko hata hata akipewa fisi haliMfyuuu....karudie na binam ako mzaa nyanyako shemeji wa bibi ako,.kilembwe cha babu ako😛
Dah kumbe ni hadith ya kweli hii??huyo bint alifariki maskini da RIP agripina.Safi sana. Nimependa hitimisho limekaa poa sana
Yaan dah, kwakweli yule babu na baharia walaaniwe kbs kwa walichokifanya.Dah kumbe ni hadith ya kweli hii??huyo bint alifariki maskini da RIP agripina.
Kasaidie kwanza ndugu zako huko vijijini waende ata shuleDah nipo mbali sana na Nchiyetu nduguzagu ila mimi kama mwanaume kweli leo chozi limenitoka nilitegemea agripina nimuone labda nimsaidie chochote ila nimekwazika sana kuwa Amefariki dah!!admn naombq nipewe contact zakuwapata ndugu wake coz me pia hom ni Muheza tanga