Mkasa ulionikuta baada ya kumtongoza msichana wa JF

Mkasa ulionikuta baada ya kumtongoza msichana wa JF

Huna hela umeambiwa agiza kinywaji nayo unaona tabu? sasa na elfu tatu yako si hata maji madogo tu ungekunywa kama ni nauli hata mshkaji ukimwambia baadaye nitumie mia tano kwa mpesa au tigo pesa nimepungukiwa angekutumia.....mnachosha sana,imagine siku ya kwanza hata kinywaji hutaki kuagiza tena umepewa go ahead, angelipa....tatizo mna madharau pia....kama ambavyo kitaa hawafanani hata JF wametofautiana,ukienda jiandae kwa lolote.
 
Dah ungejaribu tu mkuu bahati yako yaweza kuwa ulivyokuwa unafikilia siyo kabisa,,,,,muombe mkutane tena.
 
Muwe na confidence basi V8 lisikutishe wewe mjini hapa watu wana leseni lkn hawana magari lkn kutwa wana drive barabarani. Uliza wanayapata wapi. Nna jirani yangu daily anakuja na ndinga mpya Vogue, escalade, prado yaani full kindumbwendumbwe kazi hana lkn mademu wakali wote anawabwenga. So gari wala si kitu cha kuniogopesha
 
Hao ni size yangu bwa mdogo hebu nipe wajihi wake ni mzuri, tukianzia sura, kifua chake kikoje tumbo lake vp lipo flat ama kitambi na vp kuhusu nyonga! Bila kusahau kota na miguu, tafadhali nijulishe na mimi nijaribu bahati yangu
 
Pole ndugu.....japo mimi naona kuna matatizo mawili
1. Kukosa kujiamini
2. kwenda kukutana na rafiki wa kike bila maandalizi

kwa mila zetu ukimuomba rafiki yako mkutane hasa kwa mara ya kwanza ujue bili Ina kuhusu. Kwa hiyo ni jukumu lako kuweka eneo la kukutana linalo endana na kipatocha chako.
Shukuru mungu hakukuachia bili kwani ungeadhirika.....
 
Aisee kwahiyo mtoa mada wewe ni mkurugenzi gari bovu?
 
Huna hela umeambiwa agiza kinywaji nayo unaona tabu? sasa na elfu tatu yako si hata maji madogo tu ungekunywa kama ni nauli hata mshkaji ukimwambia baadaye nitumie mia tano kwa mpesa au tigo pesa nimepungukiwa angekutumia.....mnachosha sana,imagine siku ya kwanza hata kinywaji hutaki kuagiza tena umepewa go ahead, angelipa....tatizo mna madharau pia....kama ambavyo kitaa hawafanani hata JF wametofautiana,ukienda jiandae kwa lolote.

ila unajua nilivyokuwa nadhan ni mtu wa kawaida,na angekuwa hivyo nisingemuacha lakn huyu mim si level zake
 
ww mwehu kweli mm mwaka juzi nilikuwa na mdada yupo vizuri kwa kipato na kanizidi miaka kumi na moja lakini nilipiga vocal mtu mzima...inategemea umeingia kwa gia gani...
 
Hao ni size yangu bwa mdogo hebu nipe wajihi wake ni mzuri, tukianzia sura, kifua chake kikoje tumbo lake vp lipo flat ama kitambi na vp kuhusu nyonga! Bila kusahau kota na miguu, tafadhali nijulishe na mimi nijaribu bahati yangu

ni mzuri sana,amekamilika kila idara,kuanzia sura,mpaka chini.kiukwel anavutia na anahaki ya kupendwa na kila amuonae.
 
Nakusikitikia.

Una mtazamo potofu sana, tena mno.

Wapo wanawake wa aina TATU.

1) Wanaojiamini, wenye kupenda watu wanaofanana nao, kwa kipato, kwa "ngazi" ya kijamii (social standing), na elimu

2) Wanaojiamini, wenye kupenda watu wa aina yoyote

3) Wanaojiamini, wenye kupenda watu wenye pesa tu, haijalishi ana sura nzuri au mbaya, amesoma au hajasoma

Mpaka ukaweza kumshawishi huyu dada kuja kukutana na wewe mahala hapo TAYARI ulikuwa umeshashinda. Tatizo, WEWE HUJIAMINI.

Unadhani kwamba angeweza kupajua mahala unapoishi angekudharau? Pole. Imekula kwako.

Umekata tamaa mapema na hilo aliliona. Alikukaribisha kinywaji, ukakataa. Kosa la kwanza. Akasema anawahi, ukamwacha aende mpaka kwenye gari yake. Hata kumfungia mlango wake hukufanya. Hata kumbatio lake hukulitaka.

Mwanaume wa aina gani wewe, legelenge, usiyejiamini?

Endelea na mtaji huo, tuone kama hata hao wa Mbagala watakuheshimu.

Pole.
 
nimekaa nimetafakari nikagundua huyu jamaa ni muongo grade 1 maana huwez kwenda kuonana na mtu siku ya kwanza ukaenda na buku tatu sio kweli kabisa
 
Back
Top Bottom