issa ramadhani
JF-Expert Member
- Nov 11, 2014
- 1,319
- 260
Kuna mdada alikuwa anachangia sana humu JF, nilitokea kupenda sana uandishi na michango yake na nikajikuta naanza kumPM. Alikubaliana nami na tukapanga siku tukutane, alikuja na usafiri wake mpaka pale tulipoahidiana tukutane, lakini yeye alitangulia kufika kabla yangu.
Mimi nilifika baada kama dakika ishirini hivi kwa usafiri wa daladala.Nilipofika nilimkuta kaagiza kinywaji na akaniambia na mimi niagize chochote ila nilimkatalia kwa sababu nilikuwa nimebakiwa na 3000 tu ya nauli. Basi akaniuliza vipi mbona umechelewa kufika? Nikamjibu ninapoish ni mbali kidogo, akaniambia sawa na pole sana.
Basi baada ya muda na kupiga stori nying akaniaga akaniambia nataka kuondoka nawahi nyumbani na mimi nikamjibu sawa. Basi wakati anaondoka nilijua atasubiria boda boda, kumbe ana mgari aina ya V8, akaingia ndani akawasha akaondoka.
Wallah sikumpigia tena simu kwa sababu mimi sina hata baiskel na wa magari nitawaweza, nikasema bora aende zake maana akija kwangu ninapoish na jinsi kulivyo ataniaibisha JF zaidi.