Mkapa huwa unatafuta nini Karagwe, Kagera?

Mkapa huwa unatafuta nini Karagwe, Kagera?

Naomba kujua hasa kwa vijana wa ufipa hivi ni kweli msimamo wa babu Slaa na chama chenu uko palepale kwamba mkishika dola mtaruhusu utengenezaja wa gongo kisheria????
cc yeriko & ben-saa12 jioni

Ndiyo tutaruhusu. Na kodi itatumika kupeleka lami na huduma bora za jamii mpaka kwenu. Tutaweka viwango vya gongo vinavyozidi konyagi na viroba, kampuni zinazobebwa na Masisiem.
 
Wewe hata kufuga bata hapo nyumbani kwako umeshindwa, umebaki kumuongelea muwekezaji.

Acha umbea, fanya yako.
 
Karagwe kuna watoto wakali sana huenda ndo huwa anawafuata
Wewe ni --------. Akili yako inazunguukia kwenye chungu and it is growing in a centripetal way.
Yule rais mzima ni mtu wa kuhangaika na vicheche. mxczy yako.
 
Wivu Wa kike

Ingawaje sikubaliana na mtoa mada kuhusu conclusion yake, lakini pia sikubaliani na jinsi unavyopingana naye. Conclusion ya aina yake ni mbaya kwa kutoa tuhuma bila kuwa na ushahidi; jambo hili linaweza kuchukuliwa hatua za kisheria, lakini ubaya wa conlusion yako ni mkubwa sana kwa vile unanyamazisha kabisa effort yoyote ya kumtuhumu mtu aliyefanya makosa ya kujitajirisha kwa mgongo wa umma kwa vile tuhuma za namna hiyo hata kama zina ushahidi ni rahisi kuzitafsiri kuwa ni matokeo ya wivu, vinginevyo kwa nini mtuhumu asinyamaze amwache mwenzake afaidi! Nadhani mtazamo huo siyo mzuri kwa jamii. I stand to be corrected!
 
Mafisadi ya kizungu wakija tunasema wawekezaji wazawa wakitaka kuwekeza mafisadi,cjui mnataka nn nyie raia fikiria namna utakavyopata hela na uishi na familia ucmfikirie mtu anaishije
 
Hivi Mkapa hana watoto? Maana dili zake uwa anapiga mwenyewe sio kama raisi wetu wa sasa!
 
Ukosefu wa maadili ya uongozi uliashamiri kuanzia hapa...Waziri wake mmoja aliitwa mbilinyi alimega keki ya taifa enzi hizo ikambidi kujiuzulu,tokea hapo hadi sasa sijawah kosa sikia madai ya viongoz kujimilikisha mali.Viongozi wetu mkumbuke mliapa kwa misahafu na wengine kwa biblia,mkumbuke kuna sehemu tutaenda kutoa hesabu ya matendo yetu yote tunayotenda hapa duniani,endeleni kuzidisha ugumu kwa maisha ya watanzania kwa makusudi ya kuneemesha family zenu na za rafk zenu.Ila Mungu ni wa haki viapo vyenu mlivyoapa vitawahukumu siku moja.Mwenye masikio na asikie rudisheni mali mlozijimilikisha isivyo halali kwa watanzania
 
Naomba kujua hasa kwa vijana wa ufipa hivi ni kweli msimamo wa babu Slaa na chama chenu uko palepale kwamba mkishika dola mtaruhusu utengenezaja wa gongo kisheria????
cc yeriko & ben-saa12 jioni

Ukizungumza kitu kama hiki ambacho wewe si mtaalamu ni bora angalau uanze na utangulizi ili watu wakuelewe na uwashawishi hoja yako. Ili upate jibu lako, nijibu maswali haya:
1. Je wajua ni asilimia ngapi ya watanzania masikini wanaopenda pombe kali wana uwezo wa kununua konyagi, jd, gordon nk

2. Je wajua pombe kali nilizotaja yaani konyagi, jd, nk ambazo mtanzania huyu hawezi kununua ni sawa na na gongo ila tu ni kuwa gongo in vitu (impurities) ambazo watengenezaji wake masikini hawana utaalamu wa kuvitoa.

3. Je wajua pamoja na madhara yanayotokana na impurities kujulikana na gongo kupigwa marufuku bado watanzania hawa wanakunywa na kupata hata kupofoka macho nk?

4. Je wajua waliopewa dhamana ya kuhakikisha gongo haiuzwi wanajinufaisha wao kwa kuchukua rushwa kwa wanywa na wauza gongo na kuacha madhara na umasikini uendelee?

5. Je wajua kuruhusu gongo kwa kuwapa utaalamu rahisi kuondoa impurities kutafanya gongo iwe sawa na konyagi, jd nk na yenye kiwango kinachotambulika, na hivyo kuzuia madhara yanayotokana na gongo? Kitu kama hiku kilifanyika pia Uganda, walipewa mitambo rahisi kabisa.

6. Je wajua kuruhusu gongo kutafanya watu kutojificha tena wakati wa kutengeneza na kuuza na hivyo pombe itakuwa safi na hata serikali itaweza kukusanya kodi ya pombe kama zilivyo bia, konyagi nk?

Wanywa gongo ni watanzania tena masikini kuliko wanywa konyagi, jd, gordon nk. Ningekuelewa kama ungesema tupige marufuku pombe kwani pombe (alcohol) ina madhara kwa ujumla wake kiafya ila kumbeza mtu anayetaka kuwasaidia watanzania masikini kiuchumi na kiafya ni ujuha na kuonyesha kiwango kidogo cha uchambuzi wa hoja.
 
Tarehe 26 Desemba Mkapa alikuwa Karagwe na alisali kanisa la St George mjini Kayanga. Alhamisi kuu hii amesali kanisa hilo hilo. Na mwezi wa saba mwaka jana alikuwa Karagwe ikiaminika kwamba alikwenda kwenye msiba wa rafiki yake Balozi Ruhinda. Kwa ujmla tangu aondoke madarakani ameenda Karagwe mara nyingi sana.

Kuna uvumi ambao haujawahi kukanushwa kwamba wakati wa utawala wake alijibinafisisha kiwanda cha Kagera Sugar na kwamba anamiliki zaidi ya hekta elfu 40 za mashamba ya miwa. Na kwamba alipokuwa rais aliwahi kuchelewa kuhutubia mkutano wa hadhara Karagwe kwamba alikuwa na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kilichofanyika Kagera Sugar, kumbe alikuwa anakagua mashamba yake.

Hivi tunavyoongea yupo Karagwe amelala KDRDP anapopendelea kulala. Hutoka pale kusalimia kwa Balozi Ruhinda na marehemu Balozi Tibandebage. Maswali ni mengi kuliko majibu, Mkapa huwa anatafuta nini Karagwe?

Watanzania tunamambo ya ajabu sana. Kwani KARAGWE inatofauti gani na Dar? mbona mimi hupenda kwenda Morogoro kutembelea marafiki zangu? na nikiwa huko J2 lazima niende kusali, kwanini kufuatiliana kwenye mambo binafsi? tabia hii tutaiacha lini?
 
Swali lako umeshajijibu na wala sioni tatizo kama uzalishaji unafanya vizuri zaidi.
 
Kwanza napenda ufute kauli yako kuwa Balozi ruhinda ni marehemu, huyu Balozi yupo hai, na ukae ukijua ni Best friend wa Mkapa, yaani wakupika na kupakua
 
Watanzania tunamambo ya ajabu sana. Kwani KARAGWE inatofauti gani na Dar? mbona mimi hupenda kwenda Morogoro kutembelea marafiki zangu? na nikiwa huko J2 lazima niende kusali, kwanini kufuatiliana kwenye mambo binafsi? tabia hii tutaiacha lini?

wivu wa ki uke wenza
 
Kwani kagera hai~hitaji wageni? Na wawekezaji?we tanzanian, we are free karibu uwekeze songea!

Anakaribishwa Mtwara pia (Nyumbani kwake Mkapa) aje awekeze. Huku sasa hivi kuna utajiri mkubwa sana, aachane na mawazo ya mashamba ya miwa, sisi huku tunajipanga na fursa zitokanazo na Gesi na Mafuta. Aache kufuatilia mambo ya watu; anatakiwa kukumbuka kwamba kila anapotoa pumzi moja basi na muda wake wa kuivuta pumzi hiyo ndio unavyozidi kupungua. Aacha kushangaa...!
 
wivu wa ki uke wenza

Mwenye wivu wa ki uke mwenza ni ww ambaye unapenda kufuatilia maisha binafsi ya watu. Mzee wa watu BEN MKAPA ameshastaafu anaamua kutembelea marafiki zake watu mnaanza kumfuatilia mara amelala Hotel fulani yote hayo ya nini? kama siyo ujinga ni nini? "Instead of discussing issues, we're discussing about people" tuache majungu. Wewe unadhani watu wakianza kukufuatilia maisha yako binafsi utafurahia? mnafiki mkubwa.....
 
Mwenye wivu wa ki uke mwenza ni ww ambaye unapenda kufuatilia maisha binafsi ya watu. Mzee wa watu BEN MKAPA ameshastaafu anaamua kutembelea marafiki zake watu mnaanza kumfuatilia mara amelala Hotel fulani yote hayo ya nini? kama siyo ujinga ni nini? "Instead of discussing issues, we're discussing about people" tuache majungu. Wewe unadhani watu wakianza kukufuatilia maisha yako binafsi utafurahia? mnafiki mkubwa.....
kwan nimekwambia wewe au mtoa mada
 
Back
Top Bottom