Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,590
- 8,726
Gembe amethibitisha tetesi kuwa JK is behind all of these games against his successor..
Kumbe Mkapa bado anatafuna mali ya Umma..!Hawa wanawaonea, si mkuu Pinda alishasema majuzi Iringa vijana wasisite kumwita fisadi mtu yeyote anayetafuna mali ya umma! sasa hii imekaaje ina maana hawa Polisi wanakiuka maagizo ya mkuu Pinda?
Gembe, Watanzania wamekata tamaa baada ya kuona sheria hazitoi suluhu katika malalamiko yao dhidi ya aliyofanya Mkapa. Baya zaidi ni mfumo wa kutafsiri na kutekeleza sheria ambao kwa siku nyingi umehoziwa na wenye dola kiasi kwamba hata ulie machozi ya DAMU kama hawataki huwezi kufanya lolote (huwezi kutafsiri tofauti watakavyo au kubadiri)!!Tujenge Hoja na siyo kusema Mzee alipata hiki na kufanya hivi,Je sheria zinasema Vipi kuhusu kushtakiwa kwa Rais Mstaafu??na kama Haiwezekani nini kifanyike ili jambo Ambalo wengi mnalitaka litimie??
Sasa tukiendelea kulindana tutafika?...mkapa angemfanyia hivo mwinyi tungefika ..hivi mnayajua yaliyokuwamo kwenye ripoti ya warioba jamani!!!..ingefunuliwa mwinyi asingepona....dereva gani anaangalia nyuma tu...si tutagonga jamani!!!
Kitila,
Swali gumu sana hili. Nimekuwa napiga vita swala la polisi kutumiwa na viongozi wa serikali (hata wastaafu) kwa mambo ya ajabu kama haya kwa muda sasa hapa.
Ni makosa makubwa, inaonekana walitaka hao vijana wasifie tu na kupiga vigelegele kuwa mkubwa kapita.
Pambaffff kabisa!
Mkuu nimekupata kabisa na nakubaliana na wewe
Lakini tatizo linakuja hapa, wananchi wanapofikia kuchuakua maamuzi yao mikononi ujue wamechoka na matatizo
Na sema haya kwa sababu, huyu jamaa kaamua kukaa kimya pamoja na shutuma zote bila kueleza ukweli, na wala serikali haijafanya lolote ili huyu jamaa aeleze ukweli wake kwa wananchi
Pili kwa nchi kama ya Tanzania, usitegemee kama kuna sheria au haki itatendeka kwa Viomgozi hao wa serikali, Pinda alisema mafisadi wanapesa sana hivyo kuwashughulikiwa ni ngumu sana na inaweza kusababisha serikali kuyumba
Kwa maana hii hakuna lolote litakalofanyika kwa huyu Fisadi BEN, so what next ni wananchi kufanya kama wanavyofanya kwa wananchi wengine walio wezi ambao wanapigwa na mawe mpaka kufa
Na ukweli ni kuwa kama kiongozi alifanya madudu wakati wa uongozi wake ni lazima afuatiliwe, hii kasumba ya kusema eti tusiangalie nyuma ni mbovu kabisa na itasabisha wizi zaidi, kwa sababu watajua wakimaliza hakuna wakuwauliza madudu yao
Mimi naona sawa kabisa kwa hayo yaliyotokea na hii ndio iwe kampeni ya kuwazomea na mengine yanayowezekana kufanyika kwa vibaka na wezi wengine yafuate pia, kama serikali inawaogopa na kuwaacha wakikla na kutanua na pesa zetu angali wananchi wanakufa kwa shida kibao, then what
Solution ndio hiyo mpaka serikali itakapoona umuhimu wa kufuata sheria kwa wananchi wote bila kujali, kiongozi, pesa, na mengineyo
mkapa angemfanyia hivo mwinyi tungefika ..hivi mnayajua yaliyokuwamo kwenye ripoti ya warioba jamani!!!..ingefunuliwa mwinyi asingepona....dereva gani anaangalia nyuma tu...si tutagonga jamani!!!
nchi inaelekea ndiko siko kwa kuteka akili za wenye akili nyepesi!!!!
Hili nim jizi tuu linapaswa hata kumwagiwa kinyesi maana limenifanya nashindwa kupata milo miwili kwa siku na badala yake napata nusu mlo kwa siku.
Kuna mwenye taarifa kuhusu hao vijana kama wameachiliwa ama bado wanashikiliwa na polisi na wapo kituo gani?
Mbona polisi hawakujitokeza kumkamata Dr slaa alipomwita Mkapa na Kikwete wote mafisadi? huu ni uonevu wa wazi walipaswa kumkamata Slaa na Lissu kwanza ndipo na wengine wafuatie wasiwanyanyase hawa vijana waliowasababisha wao kujikuta wapo kijiweni.
aaaaaaaaaaaa.... mshkaji unaniangusha TAJA JINA LA HOTEL WE DARE TO TALK OPENLY
Nchee Nkapa anakuja kunywa whisky hapa kwenye baa ya jirani yangu chacha ntakwambia ni baa gani ,kwani huwa siku hizi anakunywaga uswahilini , ajue kuwa JF ina mkono mpana sana.
KUKIRI UDHAIFU NI USHINDI. NA HUWA UNAKUWA HURU. KUNYAMAZA KUNA LETA UTATA MKUBWA WA MAWAZO KATIKA JAMII INAYOKUZUNGUKA. JK AMEOMBA TUMUACHE MZEE WA WATU APUMZIKE KWA KAZI NZURI ALIYOTUFANYIA WATZ. MIMI NAKUBALI MH JK. ILA TUNAMUOMBA BEN KAMA MTANZANIA MPENDA HESHIMA NA KUHESHIMIWA, AJITOKEZE AJIBU TUHUMA ZILIZO MBELE YAKE. NI MTU WETU TULIEPEWA NA BABA WA TAIFA, TUTAMSIKILIZA ILA SIO LAZIMA TUAMINI ATAKAYO SEMA. KUKAA KIMYA KUNAENDELEA KUMVUNJIA HESHIMA KATIKA JAMII YA WATZ. MWANZO NDIO HIYO YA KUZOMEWA BARABARANI. WHAT NEXT KAMA HAKUNA KAULI KUTOKA KWAKE??? KAMA STATE HAITAKI AJIELEZE KWA WATZ, BASI MSEMAJI WA STATE ASEME KWA NIABA YAKE ILI TUJUE WHAT IS CROPPING UP!!!
Nchee Nkapa anakuja kunywa whisky hapa kwenye baa ya jirani yangu chacha ntakwambia ni baa gani ,kwani huwa siku hizi anakunywaga uswahilini , ajue kuwa JF ina mkono mpana sana.
Hili ni sawa,Ila tuliwazomea sana Mawaziri kipindi kile wanapita kutetea suala la buzwagi baada ya agizo la Mhe. Lowassa,Ila nini tulipata??nini kiliibadilika.
ikaja Mwaka huu,tukafanikisha Kumng'oa Karamagi,Lowassa ,Msabaha pamoja na kuangauka na wanasiasa wazee na waliofanya maovu katika serikali zilizopita,Mhe. Mramba na wengine.Je ni nini tulipata??
tukapigana kwa dhati na moyo mmoja,Chenge akadondoka,Je nini kimebadilika??
tumekuwa washaniki wa kufungwa magoli ya kisigino,na sasa tunashabikia hili la Mkpa,Je ndiyo itasaidia kuondoa Umasikini?Je ndiyo janja ya Serikali ya awamu ya nne kuwanyamaizsha wanachi??tuko tayari kwa haya mpaka lini??
Maswali sita nimeuliza ila la msingi ni kujipanga na kutumia haki tuliyonayo kuahkiksha tunaweka serikali iliyo makini na siyo serikali ya Unafiki iliyojaa urafiki ulio na Mashaka,na zaidi ya yote kinachoniskitisha ni urafiki wa Waandishi wa habari an wanasiasa,umetoka wapi??
tutafakari.