laana kubwa iliyo wakumba wana CCM akiwemo Chenge ni kwenda Butiana na kuzuru kaburi la Mwalimu wakiajiamini kwamba kafa hana madhara kwao tena .They made a huge mistake na madhara ni haya .Nakwambia huu ni Mwanzo tu .Mengi utayasikia .
Mr Lunyungu, umewakilisha kauli pana na yenye kina. "Wakiajiamini kwamba kafa hana madhara kwao tena" ...
Ndio uzuri wa Wapumbavu! Hawana maono! Hawana kina cha tafakari! Muda wakutosha ukipita wataonyesha upupu, wanadhibitisha ujinga wao. Wanajitokeza wazi na kujidhihirisha kwa kile wanachotaka kujificha..huku wakifkiri wamekificha kwa ujanja mkubwa na hawaonekani..Thanks God the principal works.
Falsa aliyoiishi na kuifundisha Mwalimu...Technicaly speaking inahitaji solid about 40 years kujikita ndani ya jamii ili iibuke kwa nguvu zote yenyewe.
Mbegu ilishaoteshwa...ndio kosa mafisadi walilolifanya. Kwa upofu wao wangezuia Mwaimu asifanye vile vitu vyake alivyovifanya.
Watu wengi hawakumuelewa kabisa wakati huo... but Now they r crinying for the principals and facts alizoziamini Mwalimu. Kila mwananchi analilia MIIKO YA UONGOZI...Thamani ya UTU nk ambayo basicaly ndio wimbo kulilia kuondoshwa kwa mafisadi!
Ukikiuka kwa kasi kabisa dhana na falsafa ya Mwalimu unachopata ni Ufisadi unaoendelea kwa kasi nchini.
Unapolilia kwa nguvu zote kuuondosha ufisadi... kwa namna fulani unamfanya Mwalmu kuwa Hai kuliko alipokuwa hai kimwili.
Kama mtu sio kipofo anawezakuona kuwa TAIFA LA TANZANIA KWA KIWANGO KIKUBWA SASA HIVI LINAELEKEA KUTAWALIWA NA FALSAFA ZA MWALIMU TENA KWA VITENDO ZAIDI YAALIPOKUWA HAI KIMWILI.
Kile alichokuwa anakiwaza na kutaka kila mwanchi akitekeleze..ni KILIO NDANI ya haya maandamamano na makelele yanayosikika bunguni na kwenye vyombo vya habari.
Neno "RUKSA" basicaly haliendani na dhana ya "UTU" na kujitegemea. Kusitiri utu wako,wa familiia yako na wa Taifa Kila kitu hakiwezi kuwa ruksa. MIIKO NA MAADILI na hata wakati mwingine maadili kuwa makali ndio chimbuo la Kutunza na kujenga Utu. Hapa Rais Mwinyi ajutie alichokifanya kama mwanzo wa jahazi kuyumba.... Hii Mbegu itakuja kuwa na kukomaa na kuwa jambo kinyume na utu na madili yake.
Kimsigi MKAPA, atajilaumu kuingia kichwa kichwa kwenye kuvunja Dhana nzima Ya UTU wake, wa Familia Yake na Ya Taifa..alipoibeba na kuitumia Dhana ya RUKSA iliyo antidote ya UTU...Bila kuisaili.
Ruksa Ikakomaa na kukamilikia pale Zanzibar Kwa Kuua MIIKO ya UTU WA VIONGOZI NA kuwa RUKSA katika kukiuka na kuvunja Maadili kwa viongozi....!
Hapo ndipo Mkapa akonyesha Ruksa katika Kutumia madaraka Kufanyia YOTE YANAYO MSUTA LEO HII, HILO LIKAZAA wote hao waliojiuzulu na watakao jiuzulu...karibni!
But Yote haya yatatibiwa kwa kilio kikuu cha Watanzania kwa MIIKO YA UTU ndani ya Taifa...ambayo ndio Kanuni kuu ya UTANZANIA.
Kwa mfano..Nani anaona Kitu kinyume na utu kwenye azimio la Arusha....Nauliza.Lilikikua nini katika kulinsda utu na Ubinaadamu.
Na atakaye pinga kanuni ya UTU amejikana utanzania ahame au ataumbuliwa tu.....Mbegu inakomaa alikuwa na tumuulize alikuwa wapi wakati mbegu inakuwa na kukomaa! Ukifanya ufisadi kama hua unaofanywa hapatanzania sasa ndani ya nchi nyigi za kiafrika unaweza usipate matatizo kama haya hapa nyumbani kwani hawana "Mbegu inayokomaa" ya kuwasuta na kuwaangamiza kama inavyotoke hapa Tanzania
Kuna wengi wameona hilo na wanarejea kwenye mstari!
Ole wa wale wasioona na wanaendelea kukiuka UTU na maadili yake katika Uongozi, elimu, afya, uchumi, makuzi ya kifalia nk. Yote haya yana kauli mbiu kwenye falsafa ya Mwalimu.
Leo hii yanahitaika kama Mvua kwenye ukame wa kiangazi kikali!
Mtu Ayapinge haya hadharani tumuone atakavyo sambaratika!!!!
Na walivyo wapuuzi hawatakubaliana na haya tunayosema hapa, Hivyo ni hakika watasambaratika na ndio ushindi tunao usubiri karibuni!