The Khoisan
Platinum Member
- Jun 5, 2007
- 18,747
- 18,504
Aliyofanya Mkapa (1995-2005)
A: Positives
7. Kufutwa kwa madeni ya nje HIPC
8. Kuongezeka Foreign Direct Investment- Gold Minig etc
10. Muafaka wa CUF na CCM
Kufutwa madeni sijanona faida yake zaidi ya kuwasaidia Watawala wetu waeendelee kukopa na kutumia vibaya mikopo kwa kuingia mikata hewa na kuifukarisha nchi yetu zaidi na zaidi pia kutuongezea madeni tu.
Swala hili inabidi ulitupe kwa JK na serikali yake kwa sababu ndiyo waliobenefit. Nafikiri Muungwana alitumia kujengea zile shule ambazo EL anatamba nazo na nyingine wakafanyia safari za kutafutia ma-investors.
Kuongezeka kwa FDI labda lakini kwenye Madini hata Muungwana anajua tumeliwa, ingawa alikuwepo na ndo maana anawapigia magoti wawekezaji wafikiri kukubali turekebishe mikataba hiyo.
Hapa nakubaliana nawe. Lakini JK hawezi kumunyoshea mtu kidole kwa vile naye alikuwa kwenye cabinet iliyohusika na haya mambo. Lakini mbona mikataba mpy anashindwa kurekebisha mpaka wanaisaini nje ya nchi kutuficha?
Sula la Mwafaka yalikuwa ni Mazingaombwe na Maigizo ambayo CCM wanaelekea kuyarudia tena, wanavuta-vuta hadi 2010. Fukurto linazidi kuwa kali. Si wasikia kauli za Makmba na Kingunge? BWM hakufanya kitu na Muungwana ameamua kuanzisha Mwafaka mpya ingawa kina Kingunge na Makamba wanafanya usanii.
Wandugu,
Kutokana na majadiliano hayo hapo juu if we are to rate our leaders in a scale of performance both domestically na internationally!
1. Mafanikio scale % ungetoa ngapi? (0-100%)
2. Mapungufu scale % ungetoa ngapi (0-100%)
3. Mark Time Position (no change)
4. Neutrality position- no comment
A: Nyerere Mafanikio 70%, Mapungufu 50%. I would rate him as a good nation builder, and Pan Africanist. Internationally ametotoa Tz kimasomaso- hata leo many admire him! He was a good president!
B: Mwinyi. Mark Time Position (no change). Mzee ruksa alifungua milango- though hakuwa na uwezo yeye binafsi. Inflation ilifikia 20%!
C: BWM: Mafanikio ningempa 60% na mapungufu 40%. Alikusanya kodi, alidhibiti mfumko wa kodi kufikia 4.5% alirudisha confidence ya Wafadhili. Internationally alitutoa kimasomaso kama Tume ya Blair, UTANDAWAZI n.k. So I would conclude pamoja na mapungufu yake he was a good president though not successful!
D: JK Mafanikio....%??? Mapungufu......%????. He is still serving indications have shown some more secondary schools been built!
So far naona kwa Tanzania, Nyerere na BWM, I will rate them better than Mwinyi and JK.
All in all the country is still poor economically but we are still one peaceful nation respected by many other nations!
Hii assessment inaonekana inalenga kiudini sana kuliko reality, haitufai, kwa sababu wizi wake ulikuwa mkubwa saana kuliko input.
ukisikiliza hiyo interview ya Shaka Sali na Kikwete eg kwenye issue ya madini sisi tunapata 3% muwekezaji anachukua 97% sasa sijui Raisi gani mwenye akili atafanya hivyo. So atleast Kikwete anataka angalau tupate 30% as corporate tax
. Viongozi wa kuwasema kwa sasa ni Nkapa na sasa Kikwete, Alhaji for techinical reasons na za wakati ule mwenyewe anasema walikuwa wanafungua madirisha hewa safi iingie nitamwacha, labda wasaidizi wake ndio wakushughulikiwa. Lakini Nkapa kaingia kaona makosa ya wenzake Mwl na Alhaji , alikuwa in a better position ya kutofanya makosa na kama ni kufanya madogo madogo sio ya kuuwa watu na uchumi wa nchi kwa kuumilikisha kwa watu wa nje. na vita ya uchumi ni ngumu kuliko ya silaha, ndio maana kila siku tunadaiwa mabilioni kwa ajili ya kandarasi mbofu mbofu.kama ya city water, net group etc. au leo mwambie barrick aondoke uone shughuli yake, maana hiyo pesa hatuna, hivyo tuna kuwa watumwa from our own making, barrick akisema no production tunalia akisema sijui nini tutafanya, au leo umuondoe kaburu tbl, utaona hiyo hela utakayo lipa au leo aseme hakuna production ya kinwaji, maafa yatakayo kuwa ktk budget
Ukiwa kiongozi wa Nchi inabidi uonyeshe uongozi wako bila ya woga na siku zote unapotete maslahi ya nchi yako wananchi watakuwa nyuma yako....Wakati mwingine unatamani kulia kwa madudu yanayoendelea katika nchi yetu. Watu wanakula mchana kweupe bila hata woga wala kunawa. Wamuogope nani!!!!! 😕
Nyerere kwa kiasi fulani alifanikiwa na ukilinganisha na marais wa nchi nyingine za Kiafrika alifanikiwa sana....Sera za vijiji vya ujamaa pia zilikuwa nzuri ili kuharakisha upayikanaji wa huduma bora kama maji, zahanati, elimu n.k. lakini utekelezaji wake ulikuwa hafifu.........
Neno la wiki.Mzee BM kweli aliamua kudumisha mila..kufanya umachinga mpaka Ikulu.