- Hapana magazeti ya Mengi ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumlipua Mkapa, baada tu ya kutoka urais, mambo ya Kiwira na ANABEN yalianiza magazeti ya Mengi na kumfanya Mkapa kuapa kwamba siku ya Mengi inakuja!
Respect.
IMESHAMJIA MKUU CHA MUHIMU AKAE MKAO WA TAMATI MAANA NGOMA IVUMAYO MKUU WA MEDANI ....
SASA TUSHAMFAHAMU VYA KUTOSHA KUWA YEYE NI NANI NA ANATUMIWA NA NANI.
JAMII ISHAMPUUZA KWANI AMEJINYANG'ANYA MWENYEWE HESHIMA ALIYOTUMIA JASHO LETU JINGI KUJIJENGEA.
MWANAHALISI SI GAZETI MAKINI TENA, NI HERI SASA HELA YA GAZETI HILO TUPATE MKATE WA FAMILIA ZETU.
MKUU WA MEDANI, MENGI NA TIMU YAKE WANAPASWA KUTAMBUA SINGLE IKIPIGWA MFULULIZO INACHUJA, KWA SASA TUSUBIRI TU BACK FIRE KWAO AS TENURE YA HUYO WANAYEDAI KAWATUMA INAPOELEKEA UKINGONI, 2015 SIYO MBALI KWA NAMBA ILA NI WAJINGA TU NDIO WANAOZUZUKA. MENGI 74 YRS OLD ANAJUA ANACHOKIFANYA KWA VIZAZI VIJAVYO LAKINI MUNGU SI ATHMAN KAMA MANDELA KAMUONA ZUMA ANAAPISHWA AKIRITHI MIKOBA NADHANI HAITAKUWA AJABU KWAKE KUMUONA AJAYE.
WASALAAM
Nadhani ni mara 7 Sabini, i stand corrected.....Hata hivyo kwasababu naamini sauti ya umma ni sauti ya Mungu,na watu hao hao ndiyo wanaowachagua na kuwatajirisha hao,(Kina RA nk)kwa baraka za wananchi,Then si Mungu ndiyo kawabariki? Again...I stand corrected....Unless Taifa la Tanzania ni Taifa la Shetani na si Mungu the argument inaweza kubadilika....Ni changamoto....Taifa la Kishetani?Sijapendezewa na hao wawili kuwaombea baraka. Anyway, tumeambiwa tusamehe 70 mara 70!!!
- Hapana magazeti ya Mengi ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumlipua Mkapa, baada tu ya kutoka urais, mambo ya Kiwira na ANABEN yalianiza magazeti ya Mengi na kumfanya Mkapa kuapa kwamba siku ya Mengi inakuja!
Respect.
IMESHAMJIA MKUU CHA MUHIMU AKAE MKAO WA TAMATI MAANA NGOMA IVUMAYO MKUU WA MEDANI ....
SASA TUSHAMFAHAMU VYA KUTOSHA KUWA YEYE NI NANI NA ANATUMIWA NA NANI.
JAMII ISHAMPUUZA KWANI AMEJINYANG'ANYA MWENYEWE HESHIMA ALIYOTUMIA JASHO LETU JINGI KUJIJENGEA.
MWANAHALISI SI GAZETI MAKINI TENA, NI HERI SASA HELA YA GAZETI HILO TUPATE MKATE WA FAMILIA ZETU.
MKUU WA MEDANI, MENGI NA TIMU YAKE WANAPASWA KUTAMBUA SINGLE IKIPIGWA MFULULIZO INACHUJA, KWA SASA TUSUBIRI TU BACK FIRE KWAO AS TENURE YA HUYO WANAYEDAI KAWATUMA INAPOELEKEA UKINGONI, 2015 SIYO MBALI KWA NAMBA ILA NI WAJINGA TU NDIO WANAOZUZUKA. MENGI 74 YRS OLD ANAJUA ANACHOKIFANYA KWA VIZAZI VIJAVYO LAKINI MUNGU SI ATHMAN KAMA MANDELA KAMUONA ZUMA ANAAPISHWA AKIRITHI MIKOBA NADHANI HAITAKUWA AJABU KWAKE KUMUONA AJAYE.
WASALAAM
Hivi wewe unamwakilisha nani? Mwananchi wa kawaida?
Ushauri wangu kwako ni kwamba kama una shida ya mkate halafu unatumia pesa yako kwenye internet kuja hapa JF ni ufukara wa kifikra....Kabla haujataka huo mkate wa mwanahalisi kwanini usitafute mkate wako wewe mwenyewe? Taifa gani hili tunajenga!
- Hapana magazeti ya Mengi ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumlipua Mkapa, baada tu ya kutoka urais, mambo ya Kiwira na ANABEN yalianiza magazeti ya Mengi na kumfanya Mkapa kuapa kwamba siku ya Mengi inakuja!
Respect.
IMESHAMJIA MKUU CHA MUHIMU AKAE MKAO WA TAMATI MAANA NGOMA IVUMAYO MKUU WA MEDANI ....
SASA TUSHAMFAHAMU VYA KUTOSHA KUWA YEYE NI NANI NA ANATUMIWA NA NANI.
JAMII ISHAMPUUZA KWANI AMEJINYANG'ANYA MWENYEWE HESHIMA ALIYOTUMIA JASHO LETU JINGI KUJIJENGEA.
MWANAHALISI SI GAZETI MAKINI TENA, NI HERI SASA HELA YA GAZETI HILO TUPATE MKATE WA FAMILIA ZETU.
MKUU WA MEDANI, MENGI NA TIMU YAKE WANAPASWA KUTAMBUA SINGLE IKIPIGWA MFULULIZO INACHUJA, KWA SASA TUSUBIRI TU BACK FIRE KWAO AS TENURE YA HUYO WANAYEDAI KAWATUMA INAPOELEKEA UKINGONI, 2015 SIYO MBALI KWA NAMBA ILA NI WAJINGA TU NDIO WANAOZUZUKA. MENGI 74 YRS OLD ANAJUA ANACHOKIFANYA KWA VIZAZI VIJAVYO LAKINI MUNGU SI ATHMAN KAMA MANDELA KAMUONA ZUMA ANAAPISHWA AKIRITHI MIKOBA NADHANI HAITAKUWA AJABU KWAKE KUMUONA AJAYE.
WASALAAM
Fedha atayolipwa Rostam Azizi na Mwanahalisi,wewe na genge lako mtapata mkate wa Familia?Kiishaa ahidi malipo kwa kazi yenu bure na nzuri??Katika ubinafsi wake Rostam ni nani wako??Rostam alipwe hizo Billioni kisha Mnyamwezi fulani kutoka kule Ulyankulu apate cha kuwafanya wanae wapande ngazi za choo???Hii naona imekaa kama Fisi asubirie mkono wa mwenye kutembea shto kulia ukatike apate BreakFast?????????? Du Mtasubiri kweli
Tutaluamu sana mwaka huu; na kulaumu sio suluhisho.
Toeni nini kifanyike, tatizo au wizi umeshatokea, TUFANYE NINI?
sheria si zipo? kwanini wahusika hawachukuliwi hatua, vinginevyo tutaendelea kuwapalilia viburi wahusika
Yona, familia ya Mkapa matatani
Mwandishi Wetu Mei 20, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
Ni kuhusu Kiwira
VIGOGO wengine wanaotuhumiwa katika kesi za kifisadi wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa baada ya uchunguzi dhidi yao kukamilika; huku kukiwa na madai ya kuwepo ulipizaji visasi katika uandaaji wa kesi hizo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya serikali na asasi zake nyeti zimethibitisha kwamba kesi zitakazofunguliwa nyingi zitawahusu watu ambao wamekuwa na misimamo tofauti kisiasa na kijamii na watu wenye nguvu hivi sasa ndani ya serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, miongoni mwa watuhumiwa ambao watafikishwa mahakamani ni wale wale ambao tayari wana kesi zinazowakabili; baadhi zikiwa tayari katika hatua mbalimbali mahakamani.
Raia Mwema inahifadhi baadhi ya majina ya watuhumiwa ambao bado hawajafikishwa mahakamani, lakini wanaotajwa kufunguliwa mashitaka yao na ambao wana kesi zinazowakabili ni pamoja na Daniel Yona ambaye alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Yona, ambaye aliwahi kuongoza wizara nyeti ikiwamo Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, tayari ameshitakiwa kwa makosa yanayohusishwa na misamaha ya kodi kwa kampuni ya uhakiki wa dhahabu ya Alex Stewarts Business Assayers ya Marekani, akiwa na wenzake, Basil Mramba aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Gray Mgonja. Mramba na Mgonja waliingizwa katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kabla ya kuondoka na hatimaye kushitakiwa.
Kwa mujibu wa habari hizo, Yona anaweza kushitakiwa sasa akituhumiwa kutumia vibaya madaraka wakati wa mchakato wa ubinafsishaji wa mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, ambao yeye akiwa Waziri wa Mkapa walihusika katika ununuzi wa mradi huo.
Hata hivyo imeelezwa kwamba Mkapa hatokuwapo katika mashitaka hayo na badala yake wanaotarajiwa kushitakiwa pamoja na Yona na familia yake, watu wanaotajwa kuwa karibu na familia ya Rais huyo mstaafu pamoja na watu wengine maarufu.
Mbali na Yona imeelezwa kwamba mmoja wa watumishi muhimu wa serikali wakati wa utawala wa Mkapa ambaye tayari ana kesi mahakamani ni mmoja wa watu watakaofunguliwa mashitaka mapya yakihusu upotevu wa fedha za BoT. Mtumishi huyo ambaye kwa sasa tunahifadhi jina lake naye anatajwa kuwa mtu wa karibu na Mkapa.
Kesi nyingine ambazo zimeelezwa kuwa katika maandalizi ya mwisho ni ile inayohusu tuhuma za rushwa kuhusiana na ununuzi wa rada ya kijeshi iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa takriban Shilingi bilioni 70.
Habari zinasema serikali imeajiri mtaalamu wa mambo ya sheria kutoka Uingereza ambaye amekuwa akikamilisha maandalizi ya kesi hizo kabla ya kukabidhi mamlaka husika kwa utekelezaji.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwapo kurushiana mpira kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuhusiana na mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa kesi hiyo, na kwa upande mwingine kati ya watendaji wa serikali ya Tanzania na wapelelezi wa Uingereza kutoka kitengo cha uhalifu mkubwa cha Serious Fraud Office (SFO).
Wanaotajwa katika kesi hiyo ni pamoja na mwanasiasa maarufu aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka kumi, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na wafanyabiashara Shaileth Vithlani na mwenzake Tanil Somaiya. Vithlani na Tanil walikuwa wamiliki wa kampuni ya Merlin International Limited, ya Dar es Dalaam, kampuni ambayo inahusishwa na biashara kadhaa na Jeshi la Tanzania zenye utata.
Katika sakata hili yumo pia Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Idriss Rashidi ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kwa upande mwingine wamo maofisa wa serikali ambao walihusika katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo.
Wachunguzi waligundua kwamba kiasi cha Paundi za Uingereza milioni 12 (takriban Sh bilioni 15/-) kililipwa katika akaunti ya Vithlani iliyopo Uswisi iliyotumika katika kufanikisha biashara hiyo wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa.
Hata hivyo, habari za ndani zimeeleza kwamba sehemu kubwa ya kesi zinazotarajiwa ama zilizokwisha kufikishwa mahakamani ni zile zinazowahusu watu ambao hawana watu wa kuwakingia kifua ama wale wanaotajwa kuwa na msimamo tofauti na watawala wa sasa kisiasa na kijamii.
Angalia wote walifikishwa mahakamani ni wale ambao wana tofauti na watawala wa sasa na wale ambao wana mahusiano mazuri wao wanaendelea kuwa salama hata kama kuna ushahidi wa aina gani. Mimi nimekusanya ushahidi wa kutosha lakini wakubwa zangu wamesita kupeleka jalada mbele, alisema ofisa mmoja wa chombo cha dola.
Ofisa huyo amesema hata baadhi ya watuhumiwa wa kesi za wizi wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) waliofikishwa mahakamani ni wale ambao waliwahi kuhusishwa na wanasiasa ambao wanatofautiana na watawala wa sasa ama rafiki zao.
Angalia Jeetu Patel ambaye pamoja na kuwa amesaidia sana katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, amejikuta akifikishwa mahakamani huku wenzake waliochukuwa fedha pamoja wakiendelea kuwa salama, alisema ofisa mwingine akiungana na mwenzake kuitaka serikali kutojenga matabaka katika uchukuaji hatua.
Tayari vyombo vya dola vimekuwa vikijenga hoja za kukwama kwa ushahidi kutoka nje ya nchi, huku vikifumbia macho ushahidi wa wazi uliopo nchini ikiwa ni pamoja na taarifa za ukaguzi na za wapelelezi wa ndani zilizothibitisha waziwazi kuwapo kwa jinai katika baadhi ya matukio yanayowahusu watu walio karibu na watawala.
Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea alisema ya kuwa, mwaka jana taasisi hiyo ilichunguza rushwa kubwa 10, na kwamba wanatarajia kufikisha mahakamani kesi nyingine tano kubwa hivi karibuni. Hata hivyo hakuzitaja.
Awali ilielezwa kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi, alikwishatoa kibali cha kushitaki angalau watuhumiwa watano wakubwa wakati watuhumiwa wengine kesi zao zikiwa katika hatua za mwisho, lakini TAKUKURU na Polisi walipata kigugumizi cha kuziwasilisha kesi hizo mahakamani.
Kumekuwa na taarifa kwamba pamoja na sheria kutolazimisha watendaji kuwasilisna na mamlaka ya juu kabla ya kufikisha kesi mahakamani, kumekuwa na kawaida ya kuwasiliana na mamlaka hizo kwa hoja kwamba, suala linalohusu haki ya mtu linapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa.
Kati ya watu wooote, huyu Idriss Rashidi ndio nasubiri kwa hamu kuona itakuwaje.
Katika sakata hili yumo pia Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Idriss Rashidi ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ...
Nataka nione kama kiongozi wa Tanzania atasema ninajiuzulu kwa sababu ya haya mashitaka.