Serious matter as this should not be mixed with celibrity; where you can talk UGORO-hapa watu wanakata vitu vya akili mnaleta mizaha; tumerogwa na nani?
Originally Posted by Sikonge
Nilikuwa najua nikivaa nguo za kawaida na siyo Joho ni kuwa SIKO UCHI. Mhhhh, maadamu sijawahi kuvaa JOHO, nimegundua kuwa tangu nizaliwe niko uchi. Nimefurahi kujua, ngoja nikanunue leo nguo (joho) ili nisiwe uchi.
Serious matter as this should not be mixed with celibrity; where you can talk UGORO-hapa watu wanakata vitu vya akili mnaleta mizaha; tumerogwa na nani?
Umejiroga mwenyewe. Mwenzako anaongea serious issues. Soma kwa makini na elewa points zake.
Ongea point; dont spin and think of redirecting the issue;Yes serious issue in B-grade celebrity understood;
NO ONE ABOVE THE LAW; NA NCHI HAITATIKISIKA ILA WAO MAFISADI WATATIKISIKA NA KUPATA PRESHA KAMA WAZEE WA VIJISENT YANAYOWATOKEA LAKIN TANZANIA WILL REMAIN; NYERERE KAIACHA ISIWE HAWA MAFISADI-EBO
Mkuu Field Marshall ES;
Heshima mbele; Kwa hili la Mh. Mkapa naomba nitofautiane na wewe na Niwe kwenye kambi yakina Gembe etc!!! Kama nilivyosema Katiba haijazuia afunguliwe kesi akiwa amefanya kosa kama yeye binafsi.
Hoja yangu imejikita kwenye Utengamano wa Taifa!
Nchi hii ambayo inasifika kwa utulivu... (yes, nimesema utulivu sijasema amani) ni miongoni mwa nchi ambazo ziko vulnerable sana na mambo fulani fulani... hivyo amani kupotea haraka sana sio jambo la ajabu hapa Tanzania. mifano ya vulnerabilities nyingi za nchi yetu ni issue ya Dini, Siasa etc. Wakati mambo kama Ukabila na Usehemu mtu anapotoka hayana nguvu ya kuporomosha taifa... isipokuwa tu... sehemu kama unaongelea Unguja na Pemba
Mifano ya Mataifa yaliyopata misukosuko kwa kumshitaki Rais mstaafu ni Zambia... etc.
Best Practices:
Majirani zetu walikuwa na uhalali mkubwa sana wa Kumshitaki Mh. Daniel Arap Moi, ambaye alikuwa na kashfa nzito sana tena sana... lakini hawakufanya hivyo kwa ajili ya mstakabali wa Taifa lao.
Kumshitaki Mh. Rais Mstaafu Mkapa... sio jambo rahisi, kumbuka wanadamu wana mioyo... na kumbuka Jamii yetu... inaweza kugeuzwa kimawazo kirahisi sana huenda kuliko jamii nyingi sana... rejea uchaguzi wa 2005(Imani waliyokuwa nayo Wananchi juu ya Mh. Kikwete); 1995(Imani waliyokuwa nayo wananchi juu ya Mzee wa Kiraracha);
Ikumbukwe kwamba Mh. Mkapa alikuwa na Record nzuri ya utendaji... ikumbukwe pia Marais hawa wawili wanatoka Dini tofauti, ikumbukwe akitokea Mchungaji au Sheikh... akapandikiza kwamba hili linafanyika kwa chuki... ya dini, waaumini wataitikia AMEN/AMIN. hapatakalika hapa nchini kwetu.
Mwisho tujadili namna ya kumfanya mtanzania afanye kazi angalau 4hours a day, ili ajitosheleze kwa chakula na aweze kuwa taxable... ana eventually awezekuwa pensionable.
Mwisho:
Ni jambo lililo wazi kwamba at least mlioko hapa kwenye jamvi hili mna uelewa mzuri zaidi kuliko waheshimiwa wengine ambao hata kompyuta hawajawahiiona... of course wapo wachache wazuri zaidi, sasa kama sisi tunataka kutoana macho,,, pamoja na kwamba hatuonani je... kwa watu mitaani itakuwa je? Matusi yaliyoandikwa already hapa kuhusu hili suala... maneno kama mpuuzi,etc... ni miongoni mwa viashiria kwamba hili si jambo rahisi.
Mungu Mbariki Mkapa apumzike vyema Rais Wetu Mstaafu!
Mungu Ibariki Tanzania.
Kama tulikuwa tunawaza pamoja mkuu.Jamani,amani ya tanzania iko delicate sana linapokuja suala la imani.Kumkamata Mkapa siyo sawa na kumkamata Mgonja,Yona au Mramba.Mkapa bado ana influence kubwa sana kuanzia ndani ya ccm na taifa kwa ujumla.Na wakuu mjue kwamba hii kamatakamata tu iliyoanza imeshazua manung'uniko mengi sana ya chinichini.Kuna watu bado wanaona huku si kudeal na ufisadi bali ni kafara inayofanywa kwa watu fulani kwa uonezi pale mtu kama Karamagi anapokingiwa kifua na wakulu ili asiburuzwe mahakamani.
Na hebu tuwe macho wakuu na hawa wanasiasa waliokosa sera wamebaki kuviziavizia tu.
Amani yetu haiko delicate, amani yetu utakuwa delicate pindi mafisadi kama Mkapa na wenzake wakiachwa huku wakiwa wametubia mabilioni ya pesa zetu. Tanzania hatuna tabaka katika sheria zetu, mafisadi na wezi wote ndani ya nchi yetu hawana tofauti mbele ya pilato hata kama walikuwa na nyadhifa kubwa kiasi gani. Msilete dhana isiyokuwapo eti amani yetu iko delicate hivyo mafisadi waachwe waendelee kupeta tu. Nchi yetu haipati maendeleo yoyote yale kutokana na waroho wa utajiri wa haraka haraka kama akina Mkapa, halafu mnatafuta visingizio visivyokuwa na vigezo vyovyote vile kwamba amani yetu iko delicate kwa hiyo waachiwe waendelee kula mali waliyotuibia bila kuguswa.
Mkuu,nisome vizuri.Nasema amani iko delicate linapokuja swala la imani.Kama watu wa imani fulani wanadhani wanaonewa katika jambo fulani na wa imani nyingine kupendelewa basi hapo mwisho wa siku hapatakalika kwa vyovyote.
Nilimaanisha hivyo.
NB:
..kuhusu Karamagi kusaini mkataba wa madini ambao si mzuri, je mkataba huo una tofauti gani na mikataba mingine ya madini? huu mkataba aliosaini Karamagi una kama miaka 2 hivi. kama ni hasara sidhani kama ni kubwa kuliko mikataba ambayo imekuwepo muda mrefu.
..kwa nini ashitakiwa Karamagi peke yake, na siyo mawaziri wengine wa madini na nishati waliopata kusaini mikataba ya madini? kuwakumbusha tu baadhi ya mawaziri waliomtangulia Karamagi na kama ifuatavyo: Jakaya Kikwete, Andrew Shija, Abdalah Kigoda, Maokola Majogo, Daniel Yona, Dr.Msabaha.
Issue ya Karamagi ni Rahisi sana, watoa hoja walitaka ashitakiwe kesi ya Rushwa ati kisa kusaini mkataba London... lakini kisheria ikaonekana ni upuuzi... kwa kuwa hakuna sheria iliyowahi sema kwamba Mkataba usainiwe Lithuli street au Magogoni street, au ndani ya nchi!!!
Kuhusu ushauri, ilionekana pia amefuata ushauri aliopewa... issue nyingine ni kwamba tatizo lilikuwa sheria iliyoko... sio yeye... in short hajaenda tofauti na sheria ya madini ya 1998... ambayo wabunge wenu wanaolala bungeni muda wote waliipitisha na kusainiwa na mh. Rais wa Jamhuri.
Mkapa asipelekwe maakamani!
Mkapa aanze kutafuta lawyer tu, kama alifikiri Watanzania tutanyamaza kimya kwa ufisadi mkubwa uliofanyika akiwa madarakani na yeye kuhusika kwa namna moja au nyingine ikiwamo mabilioni ya EPA, Kuuza nyumba za serikali kwa hasara ya $200 millioni, kusaini mikataba ya uchimbaji dhahabu isiyo na maslahi, kuwaleta net group bila idhini ya Watanzania, ununuzi wa ndege ya Rais, rada, magari na helicopters za jeshi, kukwapua mgodi wetu wa Kiwira na kufanya biashara akiwa Ikulu basi ameula wa chuya. Tumechoka na mafisadi wanaojivisha ngozi ya uongozi ili kuifisadi Tanzania mchana kweupe.
Mkuu utakuwa unakosea sana kuhusu suala la muheshimiwa kufanya biashara akiwa Ikulu. Yule bwana hakuchaguliwa kwenda ikulu kuwa CEO wa biashara zake binafsi; biashara aliyotakiwa kwenda kufanya pale ni kuwapatia faida wale waliompeleka ambao ni wananchi. Kama alikuwa na haja sana ya kuwa mjasirimali, basi angeendelea tu na biashara zake bila ya kuja kwetu sisi kutaka kura.Yeye kama raia wa nchi, kama ulivyo wewe na mwingine, anao uhuru wa kufanya atakacho ikiwemo biashara. Sheria haimzuii kufanya biashara. Na wale wanaosema alifanya akiwa Ikulu, alitakiwa aende wapi ndiyo akafanye?
Kama tulikuwa tunawaza pamoja mkuu.Jamani,amani ya tanzania iko delicate sana linapokuja suala la imani.Kumkamata Mkapa siyo sawa na kumkamata Mgonja,Yona au Mramba.Mkapa bado ana influence kubwa sana kuanzia ndani ya ccm na taifa kwa ujumla.Na wakuu mjue kwamba hii kamatakamata tu iliyoanza imeshazua manung'uniko mengi sana ya chinichini.Kuna watu bado wanaona huku si kudeal na ufisadi bali ni kafara inayofanywa kwa watu fulani kwa uonezi pale mtu kama Karamagi anapokingiwa kifua na wakulu ili asiburuzwe mahakamani.
Na hebu tuwe macho wakuu na hawa wanasiasa waliokosa sera wamebaki kuviziavizia tu.
Mkuu utakuwa unakosea sana kuhusu suala la muheshimiwa kufanya biashara akiwa Ikulu. Yule bwana hakuchaguliwa kwenda ikulu kuwa CEO wa biashara zake binafsi; biashara aliyotakiwa kwenda kufanya pale ni kuwapatia faida wale waliompeleka ambao ni wananchi. Kama alikuwa na haja sana ya kuwa mjasirimali, basi angeendelea tu na biashara zake bila ya kuja kwetu sisi kutaka kura.
Hatukumuweka pale kama BWM, alikuwa pale kama Rais wa jamhuri ya Muungano wa tanzania, na kama ukipitia katiba ya nchi, inaeleza vizuri tu ni majukumu gani rais wa nchi anatakiwa afanye, biashara binafsi halimo, hivyo kila biashara ya kujinufaisha kama Benjamin Mkapa ilikuwa ni batili....Just a common sense tu hapo.
kujibu kauli yako: Hivi wewe unadhania finance and support kubwa ambayo Lowassa and company waliyompatia Jk kwenda ikulu ilikuwa bure bure! Tatizo Lowassa ni kumba kumba na mrafi wa ghafla ghafla. Ile bond tungeishangaa after 10 years.
Juzi juzi Jk and company wamekodisha TRC kwa wahindi kwa mkataba fake. Reason kubwa- ni kuwa wataalamu wa reli waliwadanyanga investors kuhusu halisi halisi ikiwemo uhai wa mabehewa/engines na kwahiyo wahindi hawakuandaa fungu la kutosha kwa kuendeleza hayo (very stupid)!. Matokeo yake Pinda kuepusha aibu anawabeba wahindi wazi wazi kwa kisingizio cha kuwasaidia wafanyakazi ambao ni wajibu wa RITES huku waalimu na wanafunzi vyuo vikuu wanaambia hakuna hela!. Je hizi hela za kuwapa wahindi wanazichukua wapi na kwa mpango upi? Je tunahitaji kumshitaki JK na Pinda wake baada ya dakika 90 kwa huu uhuni?! Bado hatujui hatma ya Richmond, Buzwagi, ATCl etc zote hizi zikiwa ni JK creation. Tutahitaji kuwashitakia hawa after their tenure?
Kwa hiyo, Kuhusu huyu "Serious man, Ben", wabongo ni Jazba na wivu tu kama kawaida yetu. Sheria zote za TZ zinasema kila mtu hana kosa mpaka apatikane nalo. Sasa hili la kusema Ben kaiba nani katoa hukumu na wapi? Halafu ni nani kasema Mramba na Yona wameisababishia serikali hasara? Hakuna hata mmoja mpaka itakapoamuliwa na mahakama kuwa ni hivyo. Inaweza kula kwa serikali tukala hasara zaidi. Until then, let is shut up and work hard for our prosperity!