which includes you, me and mkapa!
Mkamap,
Mfano wako mzuri sana mkuu tena hapo nakupa pongezi..
Na ndio maana nimesema umeshindwa kuona wanachozungumza wana JF..
Alichofanya Mkapa ni kuwaozesha wale wajukuu kwa watu wenye fedha kisha ule mtaji akauweka benki na kutangaza maendeleo.. hao wajukuu ambao walikuwa miaka 8, 9 na 10..
Na kila naposoma maandishi yako yananipa hisia kwamba hata wewe ungefanya hivyo hivyo kwa sababu kusubiri mtoto wa miaka 8 apate elimu ya msingi, sekondary kisha sijui chuo kikuu loooh sii utakuwa umesha kufa?... kwa hiyo solution ni kuwaozesha mapema kabla hujafa..mnachotazama ni maisha yenu nyie vizee sio ya kizazi kijacho!..
Ndicho alichofanya Mkapa ktk maendeleo ya Tanzania... period!
Mkamapa hapo juu umemjibu nani?
Maana kama ulikuwa una alnalyze point uliuoitoa before bado sioni uhusiano wa wewe kuquote hiyo posting yako kwani maelezo ni yale yale na wala hakuna counter arguments ama hata further information or even analyisis.
Tanzania sio mbovu ila wabovu ni watanzania
Watanzania ni wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk
Leo hii ukianzisha biashara ya kuuza manyoya ya kuku wakaona unaendelea wengi watakujika kujipanga ulipo na wao wataanza kuuza mnyoya ya kuku natena wakilalama wewe mwanzirishi unawanyima wateja.
Hapa JF kuna wasomi wazuri ,hapa Jf kuna watu wenye uwezo kifedha lakini badala ya kujadili mambo ya kuinua wananchi pamebaki jukwaa la siasa tena lisilo na masilahi kwa taifa zaidi ya wanasiasa wachache .
Leo hii nilitegemea JF kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ na Tena wahadhili watapatikana humu na tena kwenda kuingia ubia Na Serikali/Bodi ya mikopo ya kwamba wanafunzi watakaosajiriwa walipiwe fee na ili kurahisisha uendeshaji.Hilo hakuna
Lakini akiamua kufanya hivyo JK utasikia wanafiki conflict of interest.Kufanya hatutaki akifanya mwingine confilict of interest kwa hiyo nani afanye sasa?? Kazi tunapiga siasa za zenye maslahi manono kwa wachache.
Serikali haiwezi kutuletea maisha bora ,maisha bora yataletwa na watanzania wachapakazi,wasio wanafiki na wenye upeo mpana.
Watanzania ni wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk
Leo hii ukianzisha biashara ya kuuza manyoya ya kuku wakaona unaendelea wengi watakuja kujipanga ulipo na wao wataanza kuuza mnyoya ya kuku natena wakilalama wewe mwanzirishi unawanyima wateja.
Hapa JF kuna wasomi wazuri ,hapa Jf kuna watu wenye uwezo kifedha lakini badala ya kujadili mambo ya kuinua wananchi pamebaki jukwaa la siasa tena lisilo na masilahi kwa taifa zaidi ya wanasiasa wachache .
Leo hii nilitegemea JF kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ na Tena wahadhili watapatikana humu na tena kwenda kuingia ubia Na Serikali/Bodi ya mikopo ya kwamba wanafunzi watakaosajiriwa walipiwe fee na ili kurahisisha uendeshaji.Hilo hakuna
Lakini akiamua kufanya hivyo JK utasikia wanafiki conflict of interest.Kufanya hatutaki akifanya mwingine confilict of interest kwa hiyo nani afanye sasa?? Kazi tunapiga siasa zenye maslahi manono kwa wachache.
Serikali haiwezi kutuletea maisha bora ,maisha bora yataletwa na watanzania wachapakazi,wasio wanafiki na wenye upeo mpana.
Mtaalamu_wake,
Mkuu binafsi nakubaliana na maelezo ya Mkamap na nadhani ndicho alichokuwa akisema MgonjwaUkimwi, lakini issue hapa ni UONGOZI wa Mkapa kama rais. Wananchi wote sio marais wanaoweza kujenga hoja ya Utawala kuwa questioned..Nini chimbuko la umaskini wetu ni uongozi Mbaya kwani Uongozi mzuri humtoa mtu ktk ubaya wa hali za wananchi na kuwa nzuri. Ni ubaya huo anaozungumzia Mkamap ambao Mkapa alityakiwa kuuona na kuunyoosha kama angekuwa kiongozi mzuri.. laa sivyo alikuwa akiongoza kitu gani kundi la malaika!
Wananchi wote pamoja na sisi wenyewe tuna makosa yetu kama raia, wananchi na tunaweza kulinganisha makosa yetu kwa kizazi kama wananchi lakini sio Watawala. Swala hapa ni Watawala mkuu!
Sote tunafahamu jinsi Ujamaa ulivyotugandisha kimaendeleo. Lakini ajabu ni kwamba hadi leo hii ndugu zetu wanashindwa kutafuta riziki zao isipokuwa kwa kusubiri misaada toka nje. Ni hali ambayo imejengwa na mifumo ya kitaifa.
Ebu jiulize, imekuwaje wananchi karibu wote kwa asilimia isiyopungua 60 kutegemea msaada toka kwa msamalia fulani hali ni mfumo huo huo unatumika ktk kuiendesha NCHI yetu..Tazama jinsi tunavyoabudu misaada ya IMF.
Taifa letu nitegemezi la misaada na raia wake ni tegemezi la misaada vile vile tofauti na wakati ule wa Ujamaa..Je, kila lawama zenu kwa hawa wananchi mbona mnashindwa kuziona kitaifa na kudai kwamba bila misaada tutakwama lakini hao ndugu zetu wanaodai misaada toka kwa ndugu zao mnawaona wao wazermbe!.. Je hivi kweli ukikata misaada nyumbani watu watakufa njaa? sidhani ila yawezekana ikawa ni msukumo mzuri wa wao kuanza kutafuta riziki zao vizuri, hivyo hivyo kitaifa..
Binafsi naamini kabisa kwamba kinachoendelea kitaifa ndicho kinachotafsirika kwa wananchi...Wamarekani walivyo ni sawa kabisa na mwenendo wa Taifa lao! Waarabu wanaishi kama tawala zao zilivyo, Wahiondi na hata wachina wote maendeleo yao yanatokana na tabia za maisha yao kutokana na kile kilichotangulia...
Mfumo wa serikali ndio humkunja samaki akingali mbichi..
Je wewe umejiweka kwenye kundi gani? kundi la wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk?
Umeanzisha maada ngapi za kujadili mambo ya kuinua wananchi humu JF?
Sio lazima watu wengine waanzishe maada za kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ kwani wewe pia unaweza kuanzisha halafu wengine wakakuunga mkono.
Ama kweli nyani haoni ......!