Inasikitisha sana kuona viongozi wakiifilisi nchi kwa kuitafuna ilihali wananchi wake wakiachwa maskini wa kutupwa ndani ya nchi yao!
Swala la JK kuruhusu Rais Mstaafu Ben Mkapa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kama mahakama kwa tuhuma kama hizi, hilo halipo.
Kama utakumbuka swala la Balale oooops! sorry Balal, ni kwamba kila kitu kwa maana ya ushahidi vilikuwa wazi, lakini cha kushangaza eti 'sirikali' yetu iliunda tume ichunguze ili itoe taarifa baada ya miezi sita.
Hii ilifanywa makusudi ili kupoteza muda na kuusahaulisha umma huku tume iliyopewa jukumu la uchunguzi ikiendelea kutumia fedha za wavuja jasho walio taaban!
Kwa maoni yangu mimi naona umma wa Watanzania ndio uamue kuwafikisha mahakani mafisadi wote. Umma ukiamua hakuna kinachoshindikana, lakini kutegemea JK amsulubu Nkapa oh sorry, Mkapa na wengine kwa kuruhusu kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, hiyo itakuwa ni ndoto ya mchana!
Tuanze mapambano sasa.