kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,426
- 7,213
Katika muonekano wa FIFA shirikisho za vyama vya mpira katika nchi mbalimbali ni mali ya vyama vya soka na wadau wengine katika nchi hizo, wala shirikisho hizo sio mali ya serikali. Sasa serikali inapoingilia na kufanya uamuzi kuhusu shirikisho hizo ni sawa na kuzigeuza kama idara za serikali. Jambo hilo historia inaonyesha fifa hawalikubali.
Waziri Amos Makala ameonekana kushabikia sana hoja potofu za kina Wambura na Malinzi na nadhani waziri ameshauriwa vibaya kuhusu uamuzi wake kufuta katiba ya TFF ya 2012. Mbele ya FIFA si waziri tu hawezi kuchukua hatua kama hiyo hata serikali hairuhusiwi.
Taratibu za TFF chini ya uongozi wa Tenga zimesukwa vizuri kuwazuia wababaishaji na Makanjanja kugombea uongozi katika TFF. Hao jamaa ni hodari wa kuzungusha maneno ndio maana wanampoteza akili hata Dr. Mkangara msomi mzuri.
Mtu kama Wambura aliondoka FAT bila kukabidhi ofisi licha ya kuombwa arudi kukabidhi ofisi na kuweka sawa mambo. Kwa ufupi alinyea kambi lakini hivi leo kila kukicha anataka uongozi TFF.