Waziri Jenista Mhagama Awashukuru PPRA kwa Misaada ya Washiriki wa Maafa Hanang'

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

WAZIRI Jenista Mhagama AWASHUKURU PPRA KWA MISAADA YA WASHIRIKI WA MAAFA HANANG'

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Ununuzi na Udhubuti wa Umma (PPRA) kwa kutambua na kuungana na Serikali katika kuwashika mkono waathirika wa maafa ya Maporomoko ya Tope na Mawe ya Hanang Mkoani Manyara kwa kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 16.1 ambazo wamekabidhi hii leo tarehe 28 Disemba, 2023 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo Mhe. Mhagama amewashukuru kwa namna walivyochangia fedha hizo huku akiendelea kutoa wito kwa wadau na wananchi kuendelea kuchangia hasa vifaa vinavyoweza kusaidia katika zoezi la kurejesha hali ikiwemo vifaa vya ujenzi

"Kipekee nawashukuru watumishi wote wa PPRA kwa mchango wenu na niwahakikishie utatumika kama ilivyokusudiwa," alisema Mhe. mhagama

Aidha alieleza kuwa kwa sasa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na zoezi muhimu la kurejesha hali kwa wana Hanang ili kuwapa maisha yenye ubora na furaha na kuhakikisha Watanzania wenzetu wanaendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo kama ilivyopaswa.
 

Attachments

  • 414859761_351410060850677_1640764922412849166_n.jpg
    414859761_351410060850677_1640764922412849166_n.jpg
    123 KB · Views: 2
  • 414857960_351410130850670_7379698448979632962_n.jpg
    414857960_351410130850670_7379698448979632962_n.jpg
    114.6 KB · Views: 2
  • 415220198_351410170850666_3736251763017534915_n.jpg
    415220198_351410170850666_3736251763017534915_n.jpg
    110 KB · Views: 2
  • 414860489_351410200850663_2035337772308577070_n.jpg
    414860489_351410200850663_2035337772308577070_n.jpg
    111.6 KB · Views: 3
  • 414859761_351410060850677_1640764922412849166_nmkl.jpg
    414859761_351410060850677_1640764922412849166_nmkl.jpg
    123 KB · Views: 3
Back
Top Bottom