Mkangara aingizwa mkenge 'kabang'

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,371
7,141
Katika muonekano wa FIFA shirikisho za vyama vya mpira katika nchi mbalimbali ni mali ya vyama vya soka na wadau wengine katika nchi hizo, wala shirikisho hizo sio mali ya serikali. Sasa serikali inapoingilia na kufanya uamuzi kuhusu shirikisho hizo ni sawa na kuzigeuza kama idara za serikali. Jambo hilo historia inaonyesha fifa hawalikubali.

Waziri Amos Makala ameonekana kushabikia sana hoja potofu za kina Wambura na Malinzi na nadhani waziri ameshauriwa vibaya kuhusu uamuzi wake kufuta katiba ya TFF ya 2012. Mbele ya FIFA si waziri tu hawezi kuchukua hatua kama hiyo hata serikali hairuhusiwi.

Taratibu za TFF chini ya uongozi wa Tenga zimesukwa vizuri kuwazuia wababaishaji na Makanjanja kugombea uongozi katika TFF. Hao jamaa ni hodari wa kuzungusha maneno ndio maana wanampoteza akili hata Dr. Mkangara msomi mzuri.

Mtu kama Wambura aliondoka FAT bila kukabidhi ofisi licha ya kuombwa arudi kukabidhi ofisi na kuweka sawa mambo. Kwa ufupi alinyea kambi lakini hivi leo kila kukicha anataka uongozi TFF.
 
Sijui kwa nini huyu Wambura na mwenzake Malinzi hawataki kuachana na TFF badala yake wangejikita kukuza vipaji, kufundisha soka safi na pengine kuanzisha vilabu vyenye mafanikio makubwa kuzishinda hizi timu kongwe. They proved failure long time ago, lakini bado wataka madaraka kwa udi na uvumba, duh hapo ndo ninapochoka na viongozi wa hizi nchi zetu.
 
Namuamini sana Tenga. Ni mtu makini, hakurupuki na amemudu nafasi yake vyema. Kiujumla, amejitahidi kuijenga TFF na kuifanya kuwa ni taasisi ambayo imerudisha heshima katika soka ya Tanzania. Sasa serikali itafanya makosa makubwa sana inapoanza kuingilia taratibu za uendeshaji wa soka letu. Wababaishaji kama akina Wambura wasiruhusiwe kurudi na kuuharibu mfumo mzuri wa uendeshaji soka ambao tayari umeshasukwa. Wao walikuwa kwenye hatamu za uendeshaji wa chombo hicho muda mrefu, na sote ni mashuhuda wa nini kilichotokea miaka ile, vurugu tupu. Hawana jipya, watuachie TFF yetu. Mhe. Waziri Mkangara awe makini sana na watu hawa, wasanii na waganga njaa; wanaotaka kuingia TFF kuchumia tumbo badala ya kusimamia na kuendeleza soka.
 
Hoja za kwamba MALINZI hana uzoefu wa miaka mitano. Ndo hovyo kabisa..Tenga anataka kufanya TFF ni taasisi yake binafsi na kutaka kumpachika Mgombea wake abake pekee katika uchaguzi. Sijawahi kuona sehemu amabayo Malizi alikuwa failure.
nahisi umetumwa.
 
Nilikuwa namshangaa sana Maulid Kitenge Na huyo mwenzake wanavyoshabikia hatua ya serikali! Mambo ya FIFA yanajulikana! Tenga si mbabaishaji hata kidogo wall si king'ang'anizi wa madaraka! Angeweza hata kugombea tena sababu FIFA wanamkubali lakini kwa uungwana wake ameamua kuwaachia wengine! Hawa watu wanaojiita watu wa mpira kumbe ni watu Wa kitafuta maslahi tu! Wengi wao mpango wa 60% unawahusu! Mama wa watu kaukwaa mkenge!
 
Poor Dr Mkangara siasa za futzbal zitamtia dosari na kumchafua, amekurupuka kufanya maamuzi kuhusu katiba ya TFF; bora angemtafuta Prof. Kapuya ampe uzoefu wake na yaliyomkuta enzi za FAT ya Muhidin Ndolanga na genge lake la kina Mikaili Wambura na Ismail Rage!!

FIFA will never buy that rubish!! Waziri akiwa mbishi mpira wa Tanzania kwa her!, vyama vya mpira sio shirika la serikali na wala serikali haina ubavu wa kuisukuma FIFA, Tanzanian soccer will be the looser! wake up Dr, Mukangara!!
 
Lakini hata mm nashangaa kwann mabadiliko ya katiba ya 2012 yaipitishwe bila AGM..nadhani hapo ndio TFF na hasa Tenga atajiharibia mazuri yote aliyofanya..nadhani ktk kikao kijacho ndio kiwe cha kubadilisha katiba and then uchaguzi ufanyike baadae..
 
Hili jambo mtu anaweza kulitazama ktk mitazamo mingi tu.

Kwanza inawezekana watanzania tulizoea na kuridhika na jinsi FAT ilivyokuwa inaendeshwa.Pengine ilikuwa inaendeshwa vizuri zaidi ndio maana ilipoingia TFF ikafanya kazi tofauti na FAT ndio maana tunaona kama sheria zinakiukwa na kuona kama kuna upendeleo na ubaguzi fulani.Na ndio maana watu wanalalamika kwa kuona baadhi ya wanachama wananyimwa haki kugombea nafasi wanazostahili.Maana imekuwa kinyume na mazoea tuliyokuwa nayo.

Lakini pia inawezekana TFF imekuwa bora zaidi ya FAT kwa kuweka taratibu/sheria nzuri zaidi kiasi kwamba zimeweza kuwabana wababaishaji ambao kama ingekuwa ni enzi za FAT wangeendelea kugombea na kuongoza hata kama hakuna mafanikio yoyote kisoka yanayoonekana.Maana sheria ni msumeno haitajali umaarufu wa mtu,bali itaangalia historia ya utendaji wa mhusika ktk nafasi mbalimbali huko nyuma.

Sasa hapa ndipo busara inahitajika zaidi.Tunahitaji kupambanua yote mawili,je ni TFF imekuwa dhaifu kulinganisha na FAT, au ni kwamba tumezoea na kuridhika na jinsi FAT ilivyokuwa ikiendesha soka letu?

Lakini pia ukiangalia upande mwingine wa shilingi.Je ni nani mdhibiti wa TFF hasa pale inaoonekana kutenda kinyume na utaratibu? Je tukae pembeni kuangalia na kulalamika tu? Ni kweli serikali kwa sheria za FIFA haina ruhusa ya kuingilia utendaji wa TFF,lakini je,ikiwa TFF itakiuka utaratibu,itawajibishwa kwa nani? Na pengine kutokana na utaratibu wa unaoongoza mashirikisho yetu ya michezo,inawezekana viongozi wakautumia kunajisi maendeleo ya michezo yetu.

Kituko kingine ni kwamba,inawezekana kweli Mama Mkandara alikuwa hajui utaratibu wa FIFA? Mshauri wake ni nani? OK,sasa ameishajua ameenda kinyume na huo utaratibu,na TFF ni wazi wameishatupilia mbali ile order ya waziri,what is next? Nashukuru nimemsikia Tenga akiomba kukutana na waziri ili kushauriana,fine;waziri kapata fundisho gani hapa?!

Mwisho,naamini Wambura ni mwanasheria,anashindwaje kuifikisha TFF kwenye ngazi ya maamuzi iliyo juu ya TFF kwa mujibu wa utaratibu wa FIFA? Inapotokea anachukua uamuzi wa kudai haki yake kwa kukiuka utaratibu uliowekwa na FIFA na wakati huo anataka kuiongoza TFF ambayo inaongozwa kwa mujibu wa sheria za FIFA,hapa inaleta picha gani? Na sisi bila kujua au kwa makusudi tunajifanya hatujui,tunamuunga mkono,hii nayo ikoje? Wambura inawezekana kweli ana haki ya kugombea,hatukatai,lakini hiyo haina maana kwamba turuhusu utaratibu tuliojiwekea kuvunjwa.
 
Kuna kitu kinaendelea kati ya Dr Mkangara na Makala. Nadhani mama huyu anaogopa kufunikwa!!
 
Ni kweli Wambura na Malinzi wote walikuwa FAT tumeona madudu waliyo yafanya,ni sawa wana haki ya kugombania tena Tff.
Ila kwa utaratibu huu,tutakuwa tunachangia kurudisha soka letu nyuma,kwa maana tayari tunafahamu,uongozi wa wambura na malinzi,ni kwamba ni mbovu na ndio waliochangia sana migogo ndani ya soka,sasa tunataka tena kuwarudisha,hatuoni hapo tutakuwa hatuitendei haki Tff?
 
Katika muonekano wa FIFA shirikisho za vyama vya mpira katika nchi mbalimbali ni mali ya vyama vya soka na wadau wengine katika nchi hizo, wala shirikisho hizo sio mali ya serikali. Sasa serikali inapoingilia na kufanya uamuzi kuhusu shirikisho hizo ni sawa na kuzigeuza kama idara za serikali. Jambo hilo historia inaonyesha fifa hawalikubali.

Waziri Amos Makala ameonekana kushabikia sana hoja potofu za kina Wambura na Malinzi na nadhani waziri ameshauriwa vibaya kuhusu uamuzi wake kufuta katiba ya TFF ya 2012. Mbele ya FIFA si waziri tu hawezi kuchukua hatua kama hiyo hata serikali hairuhusiwi.

Taratibu za TFF chini ya uongozi wa Tenga zimesukwa vizuri kuwazuia wababaishaji na Makanjanja kugombea uongozi katika TFF. Hao jamaa ni hodari wa kuzungusha maneneo ndio maana wanampoteza akili hata Dr. Mkangara msomi mzuri.

Mtu kama Wambura aliondoka FAT bila kukabidhi ofisi licha ya kuombwa arudi kukabidhi ofisi na kuweka sawa mambo. Kwa ufupi alinyea kambi lakini hivi leo kila kukicha anataka uongozi TFF.
Wewe unamuona wambura tu ndio tatizo?
Yeye tenga ni kwa nini anataka kulazimisha Nyamlani agombee peke yake ilhali Malinzi alikidhi viwango vyote vya kugombea na alitimiza vigezo vyoote.lakini Tenga kwa kuhofia madudu yake kufahamika endapo ataingia mtu tofauti na mtu wake Nyamlani asije adhirika.

Alafu hivi nipe ufafanuzi wa hili serkali inapomleta kocha kwa ajili ya trimu ya taifa ni sawa na hata rais anapomlipa mshahara kocha huyo hapo bado ni sawa,ila unapofika wakati wa kupeana muongozo hapo tenga ndio anakuwa mwana FIFA zaidi
 
Pamoja sana. Wapo watu wanaishi katka mpila wa tanzania kwa kutumia akili za tenga bila ya wao kujiongoza na ku jbalance ili waone upande wa pili wa shilingi. Wao wanacho fahamu 'Tenga huwa hakosei'
 
Wewe unamuona wambura tu ndio tatizo?
Yeye tenga ni kwa nini anataka kulazimisha Nyamlani agombee peke yake ilhali Malinzi alikidhi viwango vyote vya kugombea na alitimiza vigezo vyoote.lakini Tenga kwa kuhofia madudu yake kufahamika endapo ataingia mtu tofauti na mtu wake Nyamlani asije adhirika.

Alafu hivi nipe ufafanuzi wa hili serkali inapomleta kocha kwa ajili ya trimu ya taifa ni sawa na hata rais anapomlipa mshahara kocha huyo hapo bado ni sawa,ila unapofika wakati wa kupeana muongozo hapo tenga ndio anakuwa mwana FIFA zaidi
Kama kuna mtanzania bado anamwona TENGA ana matatizo na siyo Kiongozi... basi watanzania tumerogwa na mchawi wetu kesha kufa na funguo kabla hajafa alizitupia baharini! Poor Tanzania, poor Tanzanians shame on YOU!! Mkiona tunashabikia timu za nje na vyama kama FA ya uingereza msituite siyo wazalendo ile hatuwezi kuvumilia UKAKASI kama huu!!
 
Hoja za kwamba MALINZI hana uzoefu wa miaka mitano. Ndo hovyo kabisa..Tenga anataka kufanya TFF ni taasisi yake binafsi na kutaka kumpachika Mgombea wake abake pekee katika uchaguzi. Sijawahi kuona sehemu amabayo Malizi alikuwa failure.
nahisi umetumwa.
kwanini uchaguzi uliopita alikuwepo?
 
Ni kweli Wambura na Malinzi wote walikuwa FAT tumeona madudu waliyo yafanya,ni sawa wana haki ya kugombania tena Tff.
Ila kwa utaratibu huu,tutakuwa tunachangia kurudisha soka letu nyuma,kwa maana tayari tunafahamu,uongozi wa wambura na malinzi,ni kwamba ni mbovu na ndio waliochangia sana migogo ndani ya soka,sasa tunataka tena kuwarudisha,hatuoni hapo tutakuwa hatuitendei haki Tff?
washindwe kweye kula
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom