Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI WA TAARIFA ZINAZOSAMBAA ZIKIHUSISHWA NA SERIKALI YA TANZANIA KUSHINDWA KUMLIPA MKANDARASI YAPI MERKEZI NA KUPELEKEA KUSHINDWA KULIPA MISHAHARA WAFANYAKAZI WA KITURUKIDar es Salaam, Tarehe 15 Agosti 2023
Kampuni ya YAPI MERKEZI inayofanya ujenzi wa reli ya yenye kiwango cha kimataifa (SGR) kati ya Dar es salaam - Isaka inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizotolewa kupitia mitandao ya kijamii na kituo cha televisheni nchini Uturuki, juu ya changamoto ya wafanyakazi wa kituruki wanaoshiriki kwenye ujenzi wa reli ya SGR chini ya Mkandarasi Kampuni ya Yapi Merkezi kutokulipwa mishahara kwa zaidi ya miezi saba (7) ikihusishwa na Serikali kushindwa kumlipa mkandarasi (YAPI MERKEZI).
YAPI inapenda kuutarifu Umma wa Watanzania na Raia wa Kigeni wanaoshiriki kwenye Mradi wa SGR taarifa hizo si za kweli. Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) haidaiwi na Yapi Merkezi na imelipa hundi zote zilizothibitishwa kwaajili ya kazi zilizokwisha tekelezwa na kukidhi viwango vya ujenzi wa reli ya SGR.
Hadi kufikia mwezi juni 2023 Serikali imelipa jumla ya Shilingi Trilioni 8.13 kwa YAPI Merkezi ambapo malipo yake kwa kila kipande ni kama ifuatavyo: Dar es salaam - Morogoro hundi 60 zenye jumla ya Shilingi Trilioni 2.55, Morogoro Makutupora hundi 59 sawa na Shilingi Trilioni 3.75, Makutupora- Tabora hundi 10 sawa na Shilingi Billioni 883.25, Tabora - Isaka hundi 4 na malipo ya awali sawa na Shilingi Bilioni 951.6.
YAPI inaomba radhi kwa changamoto zilizojitokeza na kuleta taharuki kwa watanzania.
Kampuni ya Yapi Merkezi kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania inaendelea kutatatua changamoto zilizojitokeza na kuhakikisha mradi wa SGR unatekelezwa na kukamilika kwa wakati.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano YAPI MERKEZI
Amisa Juma
Pia soma > Waturuki wanaojenga Reli ya SGR wapo katika mgomo, inadaiwa haijalipwa fedha zao