Mkandarasi Mkuu wa SGR ametusitisha kazi lakini hataki kutulipa stahiki zetu, 'tunachohitaji sasa haki itendeke'

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Kama ilivyo kawaida dhuruma na uonevu unaendelea kufanywa na Makandarasi Mkuu wa Reli ya SGR, Yapi Merkezi dhidi ya Wafanyakazi wa Mradi.

Leo tarehe 25 mwezi wa 11 baadhi wetu sisi Wafanyakazi tumeanza kuchoshwa na ubabaishaji wa Mkandarasi unaoendelea.

Hapo kuna Makundi mawili ya watu wanaodai Haki zao, kwanza wapo Wafanyakazi waliositishiwa mikataba ya ajira, Sheria au makubaliano ni kuwa ilitokea hivyo yule aliyesitishiwa ajira anatakiwa anatakiwa kulipwa stahiki zake ndani ya siku 7 lakini hilo halijafanyika.

Imeshapita zaidi ya wiki tangu wenzetu wasitishiwe ajira na wameona hakuna kinachoendelea ndio maana wameamua kuandamana hadi kwenye Ofisi za Yapi zilizopo Kilometa 421+ Ihumwa Camp.

Wengine ni sisi ambao tunadai malipo ya NSSF, walituambia Hadi kufikia Oktoba 15, 2023 watakuwa wametuwekea Fedha hizo lakini hadi leo kimya na hatuoni dalili.

Tunaomba Serikali iingilie kati kwa kuwa tunajua hata sisi kama tutaondolewa katika mkataba tukiwa hatujaingiziwa hizo Fedha tutapata ugumu kama wenzetuView attachment 2824770View attachment 2824769
IMG_20231125_152213_111.jpg
View attachment 2824768
 
Serikali unayoitaka iingilie kati ndiyo ipo nyuma ya anguko la mkandarasi unategemea nini?

Yenyewe wastaafu wake wa 2019 bado wanasotea mafao baada ya kulipwa pungufu sababu haikupeleka michango yao kwa ukamilifu huko PSSSF.
 
Back
Top Bottom