Faiza, ahsante sana kwa kunipigia simu na kunitaka nitoe maoni yangu katika hili. Kwa kuwa sina muda mrefu wa kuwepo jamvini ntaingia moja kwa moja kwa nnayoyaona,
Nampa hongera hapo juu aliesema "Lowassa at work". Hivi mnafikiri toka Lowassa alipowachia madaraka ya Uwaziri mkuu alikuwa kakaa tu bure, anangoja nini hatma yake? Hapana. Hajakaa bure.
Lowassa alikuwa yuko "very busy" usiku na mchana na hakuwacha niwa au hila yoyote au hata kanukta kadogo kukapitia katika kujua ni vipi atarudisha heshima yake. Haya ni matokeo ya kazi yake kubwa aliyoifanya, na anarudisha heshima yake kwa njia yoyote anayo ijua. Kaanza na kawaweka sawa waandishi, akawawweka sawa makada, akwaweka sawa mawaziri (hata Sitta kwa sasa yupo nae), usishangae ukisikia na Anna Makinda nae ni mdau.
Tishio kubwa kuliko yote katika kurudisha hadhi yake ni mtu mmoja tu, nae ni Membe, huyu Bernard Membe. Kwa kuwa Membe ana akili kupita kiasi na anafata nyayo za Kikwete, kwa kuanzia kajijenga nje ya nchi ambapo anajua kuwa humu ndani hata afanye nini, nje kama hawamtaki hatofanikiwa. Membe kwa sasa ndio kikwazo cha Lowassa, goli la Lowassa si kurudisha hadhi tu, kurudisha hadhi na kuujulisha uma kuwa yeye ni zaidi ya waziri mkuu. Na menbe gali lake ni kuwa rais wa nchi hii, na kwa kichwa na maarifa aliyokuwa nayo anaweza kuupata urais kiulaini kabisa, tatizo ni maskini na hana fedha na Lowassa anatumia fedha kuhakikisha anakubakika.
Hayo ni maoni kwa yangu kwa ufupi. Samahani jamani, huku nilipo inabidi nialale mapema niamke mapema tunatumia Generator la umeme na imebaki dakika tano kuzimwa na mimi sijamaliza mengi na dakika dakika zina yoyoma. Maasalaam.
Faiza, inshalla naja mjini week end inayo kuja, nakuja kula chakula cha mchana kwako, Ijumaa baada ya salaa, naomba el forno.