Pasco_jr_ngumi
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 1,802
- 284
mmmmmmm........ siasa ni kula au kuliwaaaaaaaaaaa.....grrrrriiiiiiiiii@#$&%%$$##@1
Hatubishani, wewe eleza unavyomjua Lowassa/Membe nami nakueleza navyomjua Membe na Lowassa.
Na nimekwambia Membe anaishi kama Waroma wanavyoishi, CCM nchi nzima kila mtu anatafuta kujitajirisha yeye afanye nini? wakati Azimio la zanzibar linawapa ruksa!... Na ndio sababu hatutaki rais anayefuata atoke CCM hata kama akiwa Shein ambaye ni mbora zaidi yao wote lakini naye kisha kavuta kitu kidogo vile vile. Hatutafuta saint kwa sababu hakuna kati yao msafi, isipokuwa mwenye uzalendo hata kidogo ama kutumia akili ya uongozi. Vinginevyo, hata siku moja mtu hawezi kuwa msafi kwa kuoga tope. Membe na wengine wote wanayakoga maji machafu..
Nachosisitiza mimi ni kwamba huwezi kabisa kumlinganisha Lowassa na Membe kwa hali yoyote ile ktk uongozi wa nchi. Lowassa ni hamna kitu anaweza kuwa mfanya biashara mzuri sana na tukajiuliza kati ya yeye na Papa Msoffe nani zaidi, lakini sio uongozi wa nchi. Katika historia ya Tanzania yeye ndiye waziri mkuu wa kwanza kujiuzulu kutokana na scandal za ufisadi na hakuwa hivyo tu hakutakiwa hata wakati wa Nyerere wakati kulikuwepo na matajiri wengi ndani ya chama...Unataka mifano gani zaidi.
Pesa za Libya ndio zimekuwaje?..alienda kuiba huko au?
Kinachoshangaza ni Salim Ahmed Salim pamoja na kuaminika ni mtu safi ni kama hayupo kabisa! Hatajwi! Sijui kwanini hatajwi!Ni kweli inawezekana kabisa,lakini haiwezekani asiwe mkatoliki au muislam!hao ndio watawala wa hii nchi,habari ndio hiyo,hatuwezi kuwapa nchi watu tusiowajua waje kujaribu kisa eti safari hii "zamu yao" no way!
Rais wa 2015 atatoka Kaskazini!.
Ya nani haikujaa damu? Lowassa!... mkuu wangu Membe anaishi kama Waroma wanavyoishi. Membe alipigwa vita sana wakati wa Mkapa na limejaliwa kukutana naye uso kwa uso akiwa hapa Canada. Ni kichwa na nakuhakikishia ni watu wachache sana mimi naweza kuwapa sifa kama hizi. Lakini sio Lowassa ambaye tangu ameingia na JK, watu wasiopungua sita Muhimu sana kwa taifa wameisha ondoka duniani kwa scandal zake tu. Na alleged atrocities hizi haziwezi kuwa coincidences mahala ambapo kuna compiling evidence zinazo m-link yeye..
Ebu jiulize Lowassa leo hayupo madarakani, kama Uwaziri mkuu, Warioba aliwahi kuwa, Malecela, Salim, Sumaye lakini mbona wote hawa waliondoka bila scandals kama zake na wamekaa kimya isipokuwa yeye ambaye hana madaraka yoyote ya kiserikali leo lakini duh... kacheza hadi kapewa wenyekiti wa kamati bungeni.. Anawatishia watu na uganga wa Loliondo, sumu na kadhalika huyu binadamu kweli..
Membe na Libya hata mimi namuunga mkono, ni msimamo wa nchi na protocal na code of African Union kupinga nchi za magharibi kuingilia maswala ya Africa. Na nchi zote za kiafrika zilitakiwa kupinga uvamizi ule hata kama ilikuwa lazima tungetoa sisi uamuzi wa mwisho. Hukubaliani na msimamo wa Tanzania hilo lako lakini ndiovyo ilivyotakiwa na kafanya kulingana na msimamo wetu.
Hoja ya Mashoga imetumiwa na Uingereza na sio Membe. wao ndio wamedai tutambue ndoa za Mashoga wakati wananchi wanakufa njaa, Ufisadi unatawala mikopo yao yote na tumeomba wazuie misaada lakini wakatuona hatuna maana kwa sababu wana interest zao kubwa nchini.. Wasione ubaya ktk Ufisadi unaotufilisi isipokuwa kwenye swala la ushoga ambalo yeye mwenyewe kama Conservative hakubaliani nalo - Huo sii unafiki kitu gani?
Kinachoshangaza ni Salim Ahmed Salim pamoja na kuaminika ni mtu safi ni kama hayupo kabisa! Hatajwi! Sijui kwanini hatajwi!
Nashauri tu memba wenzetu wengine kama wana uwezo mkubwa wa kutunga hadithi kama hizi ni kwa nini basi wasiandike vitabu vya hadithi ili wauze waingize pesa?
Yaani wewe mpaka kesho unaamini manabii wa uongo? Miujiza iliisha yesu alipoondoka duniani kama hujui hawa wote wanaojiita manabii wanamtumikia shetani hawana tofauti na sangoma.Ukienda kwa mganga hukosi la kuambiwa. Kama kweli atakuwa raisi Joshua alitakiwa amwambie hayo maono siyo yeye kuuliza eti nikigombea uraisi 2015 nitashinda? jibu ndiyo kwa joshua sianafanya biashara watu wanalipia huduma yake ulitaka amwambiaje. Nenda na wewe kamwambia huyo joshua miaka mitano ijao utakuwa hai au la uonejibu utakalopewa.
Wapenzi, msiiamini kila roho, bali ZIJARIBUNI HIZO ROHO, kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani (1Yohana 4:1).
Angalieni, mtu asiwadanganye, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao WATAWADANGANYA WENGI ... Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki. Kwa maana watatokea MAKRISTO WA UONGO nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate KUWAPOTEZA, kama yamkini hata walio wateule, Tazama, nimekwisha KUWAONYA MBELE (Mathayo 24:5, 23-25).
Yaani wewe mpaka kesho unaamini manabii wa uongo? Miujiza iliisha yesu alipoondoka duniani kama hujui hawa wote wanaojiita manabii wanamtumikia shetani hawana tofauti na sangoma.Ukienda kwa mganga hukosi la kuambiwa. Kama kweli atakuwa raisi Joshua alitakiwa amwambie hayo maono siyo yeye kuuliza eti nikigombea uraisi 2015 nitashinda? jibu ndiyo kwa joshua sianafanya biashara watu wanalipia huduma yake ulitaka amwambiaje. Nenda na wewe kamwambia huyo joshua miaka mitano ijao utakuwa hai au la uonejibu utakalopewa.
Wapenzi, msiiamini kila roho, bali ZIJARIBUNI HIZO ROHO, kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani (1Yohana 4:1).
Angalieni, mtu asiwadanganye, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao WATAWADANGANYA WENGI ... Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki. Kwa maana watatokea MAKRISTO WA UONGO nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate KUWAPOTEZA, kama yamkini hata walio wateule, Tazama, nimekwisha KUWAONYA MBELE (Mathayo 24:5, 23-25).
JK na Lowasa wana MoU kama ile ya aliyekuwa WM wa Uingereza Tony Blair na waziri wake wa hazina Gordon Brown. Sema tu KATIBA yetu ya sasa hairuhusu mpangilio kama ule wa Uingereza. Juzi kwenye vikao vya CCM mliona MoU hii inavyotekelezwa kwa umakini na umahiri mkubwa. Labda Mwalimu afufuke kwa sasa. Vinginevyo akina Membe wana shughuli pevu na ndio maana hata hii thread tayari iko humu.Sidhani kama Kikwete anaweza kuungana na Lowasa tena, hata kama hawakukutana barabarani. Sidhani kama swala la mali ni muhumu sana sasa hivi. Tunajua zipo na it is just a matter of time zitarudi. Muhumu ni wazidi kutifuana kusudi iwe rahisi kuwaondoa, watu wenye uchungu na nchi yao watwae madaraka. Lakini kama wakiungana tena kina Membe and Co. wana uwezo wa kupambana na Lowasa?. Kama hivyo ndivyo ilivyo Lowasa anaweza kuwa Rais 2015? Kuna mtu anafahamu procedure za kutafuta uraia wa Botswana?
Asante Mungu kwa kunifanya nizaliwe nje ya Uislam.Faiza, ahsante sana kwa kunipigia simu na kunitaka nitoe maoni yangu katika hili. Kwa kuwa sina muda mrefu wa kuwepo jamvini ntaingia moja kwa moja kwa nnayoyaona,
Nampa hongera hapo juu aliesema "Lowassa at work". Hivi mnafikiri toka Lowassa alipowachia madaraka ya Uwaziri mkuu alikuwa kakaa tu bure, anangoja nini hatma yake? Hapana. Hajakaa bure.
Lowassa alikuwa yuko "very busy" usiku na mchana na hakuwacha niwa au hila yoyote au hata kanukta kadogo kukapitia katika kujua ni vipi atarudisha heshima yake. Haya ni matokeo ya kazi yake kubwa aliyoifanya, na anarudisha heshima yake kwa njia yoyote anayo ijua. Kaanza na kawaweka sawa waandishi, akawawweka sawa makada, akwaweka sawa mawaziri (hata Sitta kwa sasa yupo nae), usishangae ukisikia na Anna Makinda nae ni mdau.
Tishio kubwa kuliko yote katika kurudisha hadhi yake ni mtu mmoja tu, nae ni Membe, huyu Bernard Membe. Kwa kuwa Membe ana akili kupita kiasi na anafata nyayo za Kikwete, kwa kuanzia kajijenga nje ya nchi ambapo anajua kuwa humu ndani hata afanye nini, nje kama hawamtaki hatofanikiwa. Membe kwa sasa ndio kikwazo cha Lowassa, goli la Lowassa si kurudisha hadhi tu, kurudisha hadhi na kuujulisha uma kuwa yeye ni zaidi ya waziri mkuu. Na menbe gali lake ni kuwa rais wa nchi hii, na kwa kichwa na maarifa aliyokuwa nayo anaweza kuupata urais kiulaini kabisa, tatizo ni maskini na hana fedha na Lowassa anatumia fedha kuhakikisha anakubakika.
Hayo ni maoni kwa yangu kwa ufupi. Samahani jamani, huku nilipo inabidi nialale mapema niamke mapema tunatumia Generator la umeme na imebaki dakika tano kuzimwa na mimi sijamaliza mengi na dakika dakika zina yoyoma. Maasalaam.
Faiza, inshalla naja mjini week end inayo kuja, nakuja kula chakula cha mchana kwako, Ijumaa baada ya salaa, naomba el forno.