Mkakati wa Kumuhujumu JK na Lowassa

Mkakati wa Kumuhujumu JK na Lowassa

Tuna washikaji huko Idara ya Usalama wanasema Membe hana ushawishi unaoelezwa hapa ndani ya chombo hicho cha kijasusi. Wanasema, Membe hakuondoka huko kwenda kwenye siasa kwa kupenda bali mazingira ya kupungua kwa ushawishi wake kulichochea kutafuta mahali pengine pa kazi. unaposema membe anasaidiwa na watu wa Idara ya Usalama inatia mashaka.
 
Post imekaa kama tetesi na kama utaisoma kwa makini na kuipigia mistari utabaini imetungwa kukidhi matakwa ya kisiasa
 
Nimesoma kila post inayoelezea hujuma hii na naishia kuamini kuwa huu ni mkakati wa Lowassa na team yake kuwachafua wale aonao ni vikwazo kwenye kufanikisha nia yake ya kugombea urais 2015.

Lowassa anajua fika kwamba kizingizi kilicho mbele yake ni Mh Benard Membe pekee.

Hivyo Jitihada nyingi zaelekezwa kummaliza kisiasa ili kufanikisha nia yake na ndio maana sishangai wanavyojaribu kumgombanisha na JK jambo ambalo kwao litakuwa ni faraja japo naona ni gumu kidogo kutokea.

Simlaumu Lowassa kwa kufanya hivi kwani akili zake ndivyo zinavyomtuma japo wanaomfahamu Membe wanajua kuwa ubongo wake hauna matundu kama wa lowassa hivyo kujua nini anafanya.

CCM imejaa mapoyoyo wengi sana na lowassa ni mmoja wao.

Kama ni kutoa Rais basi naamini kabisa afaae ni Membe vinginevyo ni bora tukawapa upinzani na wao wakajaribu kuongoza nchi.

OTIS
 
Ni kweli tu@!
Huwezi kumtenganisha JK na EL. wote wanajijua hali zao na siri zao moja!!
Membe former strong TISS at work atawamaliza wote.
 
Nakumbuka maneno ya Mwl kuwa mpinzani wa kweli atatoka miongoni mwa wana CCM
 
Nimesoma kila post inayoelezea hujuma hii na naishia kuamini kuwa huu ni mkakati wa Lowassa na team yake kuwachafua wale aonao ni vikwazo kwenye kufanikisha nia yake ya kugombea urais 2015.

Lowassa anajua fika kwamba kizingizi kilicho mbele yake ni Mh Benard Membe pekee.

Hivyo Jitihada nyingi zaelekezwa kummaliza kisiasa ili kufanikisha nia yake na ndio maana sishangai wanavyojaribu kumgombanisha na JK jambo ambalo kwao litakuwa ni faraja japo naona ni gumu kidogo kutokea.

Simlaumu Lowassa kwa kufanya hivi kwani akili zake ndivyo zinavyomtuma japo wanaomfahamu Membe wanajua kuwa ubongo wake hauna matundu kama wa lowassa hivyo kujua nini anafanya.

CCM imejaa mapoyoyo wengi sana na lowassa ni mmoja wao.

Kama ni kutoa Rais basi naamini kabisa afaae ni Membe vinginevyo ni bora tukawapa upinzani na wao wakajaribu kuongoza nchi.

OTIS
WAPROTESTANT na WAISLAMU wa NCHI hii hawataki MKATOLIKI mwingine awe RAIS. Mwalimu na Mkapa wanatosha kwa sasa. Chaguo la Waprotestanti ni Lowasa. Tunagawana madaraka na vyeo kwa DINI na madhehebu yetu sasa.
 
Sitta alishawahi kusema kupingana na Lowassa ndani ya CCM haina tija kwa sababu JK ni dhaifu sana...nafikiri ananunua muda yeye na wenzake wachache watatoka..2012 mabadiliko na mageuzi ya ukweli yataanza
 
Katika vikao vya NEC mwezi huu Lowassa alinukuliwa akisema;

‎"Mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kumpigia simu Mheshimiwa Rais akiwa katika safari nje ya nchi alisema tusubiri kwani alikuwa amepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara. Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima?"

Kauli ya Chenge Airport kuhusu kumiliki akaunti yenye 1.2bn

"Hivi ni vijisenti tu."

Kupotea ghafla na kifo cha utata cha Daudi Balali.

Tunapata tafakaro mpya kuhusu nani hasa alihusika katika uozo huu?
 
Si unajua kwenye movie, jambazi kuu huwa linakufa mwishoni? Basi picha bado linaendelea.
 
Ni kama unauliza je Mwadui kuna Almasi a.k.a Diamond.
 
membe na sitta siyo marafiki wa kupanga mikakti mizito yeyote...thread ya kutunga ila kama fiction ina utamu wake
 
Ama kweli!!! UONGO MWINGINE UNAHITAJI UJASRI WA KIFISADI KAMA WAKO KKUTUNGA NA KUTKATA WATU WAUAMINI! NINAMASHAKA NA UJAZO WA UBONGO WAKO, TUKIUPIMA NA WAKUKU, WAKUKU UNAWEZA KUWA MKUBWA. POLE SANA, MTAHANGAIKA SANA!
Wana JF,

Baada ya kikao cha NEC dodoma Mh MEMBE alimwaaita wajumbe wa NEC wafuatao na Kufanya NAO kikao Nyumbani kwake wajumbe hao ni

NAPE NNAUYE
Capt CHILIGATI
LUSINDE maarufu kwa Jina kibajaji
Makongoro Nyerere
Mzee Samweli sita ambae alifatwa nyumbani kwake akiwa amejipumzisha
Ndg Wilson Mukama

Wajumbe hawa walikutana nyumbani kwa MEMBE baada ya kikao cha nec mzee sita aliwahi kutoka kwenda kupumzika baada ya SUMAYE kuongea.

Katika kikao hicho ukaandaliwa mpango madhubuti wa kupambana na kikwete kwakua hawa jamaa wanaamini Kikwete amewatosa na kuamua kujiunga na Lowasam

Makubaliano.

(1) Kutoa siri za kikwete na hapa hasa mali alizonazo Nje ya Nchi na hapa atakae fanya hii kazi ni Bwana Membe.

(2) Kutumia urafiki uliopo kati ya Membe na baadhi ya watu ndani ya idara ya usalama kufanikisha Mpango huu.

(3) Mzee Samweli Sitta aanzishe mazungumzo na CHADEMA ama CUF ili kuandaa mpango wa kujiunga na chama kimojawapo kati ya hivo viwili kwakuwa Sitta ameona kuwa hakuna njia ya kumzuia Lowassa kushinda ndani ya CCM.

(4) Kutokana IMANI na matumaini ambayo NAPE aliyokuwa nayo baada ya mkutano wa JK na wabunge wa CCM Dodoma, NAPE alimfata Bwana Mwigulu akiwa na Chiligati, Nape amedaiwa kumwambia Mwigulu "Bwana MKUBWA (JK) ameishaingia line ameelekea KIBLA tusaidie kesho tummalize huyu Lowassa, mzee anataka sisi katika kamati kuu tuanzishe, kaka usituangushe"

Baada ya hili kutotokea NAPE amedai atahakikisha analipiza kisasi kwa kuanika SMS walizo-chat na JK, kuonyesha JK alikuwa anamtuma.

Mpango wao unalenga kwanza kuonyesha JK haaminiki, Pia wanadai kwakuwa amewasaliti watamuanika.

PIA Mbunge Ismail Aden RAGE akiwa uwanja wa Ndege wa Tabora Juzi katika VIP akiwa amefatana na Mbunge wa Bukene Selemani Zedi alinukuliwa akisema, "Nimeongea na Mzee Sitta amesema njia pekee ya kupambana na Lowassa na Kikwete ni Nje ya CCM, mimi najiandaa kuondoka" haya ni maneno ya sita ambayo Rage aliyanukuu kwa Selemeni Zedi na Rage akasema Nadhani mzee Sitta yupo Sahihi acha aende JK na Lowassa wote ni Mafisadi.

Wana JF, chanzo cha habari hizi ni mtu aliyekuwa katika vikao hivo vya Dodoma na Membe na Nape walikutana Protea wakiwa na Jack Gotham na Balozi wa heshima wa Comoro. Walikutana kuendelea kupanga mikakati, kumekuwa na Vikao vingi sana ambavyo vimeanza kufanyika, na Membe sasa na yeye anjipanga kuanza kutumia makanisa; hivi karibuni na yeye atakua na Harambee ktk kanisa Katoliki Magomeni.

Kwahiyo mnyukano CCM ndo umeanza sasa waliokuwa watu wa Kikwete sasa wanaanza mipango ya kumhujumu na kuanza kutoa siri za mali zake zilizopo Uarabuni.

Nawasilisha
 
Nimeongea na Jack Gotham na kumuuliza kama alikuwa na kikao chochote kama ilivyoripotiwa ktk JF, ameniambia kuwa jana alikuwa yeye ni mmoja wa wana Kamati ya Maandalizi ya Harambee ya Kanisa Katoliki Magomeni. Jana kulikuwa na kikao cha Kamati, na alikutana na vijana wawili ktk Hoteli moja ambayo Kamati hiyo ilikutana, na akawaambia kuwa anaenda kwenye kikao hicho. Ameniambia atanitajia majina yao na namba zao za simu, na mazungumzo yao walipokutana. Inaonekana amesikitika sana.
 
Nakumbuka maneno ya Mwl kuwa mpinzani wa kweli atatoka miongoni mwa wana CCM
Mkuu acha kuwa mvivu wa kufikiri, hilo unalosema tayari lilishatokea, kwani haujui kwamba Dr Slaa alikuwa CCM? kama unadhani kuna mwingine basi wewe huna tofauti na wale wayaudi wanaosubiri Yesu azaliwe, wakati Yesu alishazaliwa.
 
Nimeongea na Jack Gotham na kumuuliza kama alikuwa na kikao chochote kama ilivyoripotiwa ktk JF, ameniambia kuwa jana alikuwa yeye ni mmoja wa wana Kamati ya Maandalizi ya Harambee ya Kanisa Katoliki Magomeni. Jana kulikuwa na kikao cha Kamati, na alikutana na vijana wawili ktk Hoteli moja ambayo Kamati hiyo ilikutana, na akawaambia kuwa anaenda kwenye kikao hicho. Ameniambia atanitajia majina yao na namba zao za simu, na mazungumzo yao walipokutana. Inaonekana amesikitika sana.

Jack Gothan ...TISS operative ...Membe campagne team........Along with Nape...ambaye amehamia toka kwa Mwandosya....

Nape hizo message za KIkwete unaziweka live lini?
 
Ama kweli!!! UONGO MWINGINE UNAHITAJI UJASRI WA KIFISADI KAMA WAKO KKUTUNGA NA KUTKATA WATU WAUAMINI! NINAMASHAKA NA UJAZO WA UBONGO WAKO, TUKIUPIMA NA WAKUKU, WAKUKU UNAWEZA KUWA MKUBWA. POLE SANA, MTAHANGAIKA SANA!
Nape,
Na wewe ukitoa majibu kama haya, kwa hadhi na nafasi uliyonayo katika jamii na CCM tunashindwa kuutofautisha ubongo wako na wa huyo unayemjibu. Baadhi yetu tunafahamu una wakati mgumu ndani ya CCM. Usitukatishe tamaa kwa kuwa mapambano haya yanahitaji watu NDANI na NJE ya CCM.
 
Back
Top Bottom