DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,688
John, ninao ushauri mdogo kwako, siasa hizi za kutunga hadithi zimepitwa wakati sana, sasa ukindelea nazo itabidi uingie kwa jina lako ili tukujibu kwa uongo wako, ukishindwa nitakusaidia kuweka jina na picha, then tuongee kama wanaume na si kutunga hadithi za kipuuzi kama hizi halafu unadhani umejificha kama mbuni. Nimeshangaa kama na M naye umemuinbiza kwenye hili badala ya yeye kufanya kazi za ofisi ya Makamu, ambazo kwakweli ni nyingi na zinahitaji muda...... Be carefull na uongo usiokuwa na mashiko...
MMhhh Nape inamaana MVUA GAMBA ni John,au?ebu tujuze manke ukichelea mwana kulia utalia wewe.Uhitaji kumtisha kama unauhakika ni yeye mweke wazi watu wamjue yafunguke mengi toka kwa wengine kutisha huku bila kufanya kweli ndiko kuliwaponza wakina Mwakyembe na Mwandosya.Wanaume uwa awatishani kama ni kuexpose fyatuka ukijifungia wenzio watakumaliza kisha unaanza kulalama wamekuchezea faul.Ndio madhara ya kuficha ficha hata mambo ya kipumbavu yasiyo na msingi chama chako kinayahimiza kuficha matokeo yake wenye hira wakiyanyaka wanayachezesha mpaka Ukweli unageuka uongo na uongo unageuka ukweli.
Kitabia za makabila kuna baadhi ya makabila uwa tunayaita hayana break,ukimyumbisha Mwanaume wa kikurya atakuja moja kwa moja mbele ya uso wako na marafiki zako na kukupa ukweli utake na usitake ndio kisha kwambia.Wanyiramba wanaume ni waungwana sana lakini ni jasiri na wenye msimamo usioyumba.
I hope wewe bado kijana,siasa zako hazipawi kuwa za kuficha ficha mambo tena haswa muhmimu, zama zako ni za uwazi,na siri siku hizi aiwekwi hadharani kujadiliwa, siri inafungiwa kwenye kuta nne na mwisho wake ni huko huko kwenye kuta nne,ikisha fika uku kwenye FJ sio siri tena.Ukishafika JF na mada yako jua hiyo mada sio siri tena Nape.
Its time know you need to change,utoke kwenye style ya Mababu na Baba zako ndani ya CCM,waonyeshe kuwa wewe ni kizazi kipya chenye kuitaji ukweli na sio nazi kuambiwa kuwa ni dafu.Ukiendelea na tabia ya kucopy na kupaste toka kwa mababu zako wa CCM hakika wewe na hicho chama chako wote mtakumbana na kaa la moto kwenye koo toka kwa Wananchi.
Ebu jaribu kuvaa viatu vya Watanzania vijana kuanzia miaka [15-45] angalia maisha yao vijana wa Tanzania mitaani Dar es Salaam nyumbani kwa mama yako Singida na Tanzania ulioizunguka hawajui kesho yao itakuwaje.Vijana wengi wamepoteza matumaini angalia tukio la Mbeya isingekuwa KIJANA MWENZIO SUGU,hakika hali ingekuwa tete mpaka sasa. Jitolee kweli kweli kusimamia kile unachokiamini na waonyeshe wazee hao kuwa ndio unavyoamini,zile tabia za kinafiki za wakubwa kupigiwa makofi uku wakishabikia na kueneza uongo zimekwisha kwa kizazi cha sasa. Kwa kuwa utawalaghai leo kesho keshokutwa wanataka majibu,ukiwabishia wanakuibukia.
Ukiwafuata na kukubali kila wanachokuambia kesho itakucost wewe na si wao kwa kuwa wengi wao ni mababu na hawana cha kupoteza ila wewe unaebaki na sisi vijana tutakubana kukuuliza ulikuwa na wale mababu ulishiriki kutufisha hapa tulipo sijui utawajibu nini wadogo zako na vijana wenzio wa Tanzania ambao sasa hivi wanakaribia asilia 60% ya Taifa zima.Ila ukijisimamia kama Mtu huru [Free and Independet Man] na sio Mr NDIO MZEE wote watakili kuwa na wewe ni kidume na ndipo wenye akili wanakuamini na kukusaidia.Huna sababu ya kuwa mwoga,kwa kuwa siasa kwako wewe iko kwenye damu kama Makongoro au Watoto wa Kawawa na kujiamini ni dhahili kuwa mtoto wa mwanajeshi hakufundishwa nidhamu ya woga.
Funguka utusaidie tupate kuunga A na B kujua wenye hira na Taifa hili, acha siasa za CCM za kizamani nyie vijana haswa wewe unapaswa kuwa chachu ya mabadiliko na kuanza kuonyesha mabadiliko kutoka kwenye zama za kila kila jambo kuwa siri eti lijadiliwe kwenye ngazi za chama uku,mnaongeza ufa wa matatizo kwenye Taifa.
Ni vyema kujibu maswali muhimu ya wananchi wakati sahihi.Mfano kwa sasa hatujui kama ni kweli au umetungwa uongo kuwa NAPE Katimuliwa DODOMA,na kweli baad ya muda tunamuona Katibu wa Chama ndie anaetoa taarifa za vikao na si Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya UMMA.
Umekuja JF sikuona wewe kuleta taarifa makini kuwa jamani kutokuwepo kwangu na hayo yanayosemwa dhidi yangu kwa uchachee najibu ifuatavyo moja mbili tatu.Lakin umeibuka na shutuma kama mpita njia.Ndio wewe humu JF umeingia kama NAPE NAUYE lakini pia umetumia jukwaa hili kufikishia umma wa Watanzania taarifa muhimu za chama chako cha CCM.Hivyo tunapokuona humu tunakuona kwa sura Mbili au Kofia Mbili,moja kama Nape Moses Nauye na nyingine kama Kiongozi wa CCM wa Itikadi na Mawasiliano ya umma na JF ni moja ya ya Jukwaa la Umma.
Kwa kuwa chama chako hakina ID humu JF ndani, ili kutoa ufafanuzi pale tunapoitaji kujua jambo toka kwenye chama chako basi ujio wako humu utupatia nafasi ya kujua na kukupa maswali yetu.
Hivyo funguka tujue hata kama kuna waliokusemea kuwa ulikuja kutetea masters yako Mzumbe Dar,wale si wewe wale ni wao tuliitaji kusikia toka kwako.Nilichosikia toka kwako mpaka sasa ni aina ya lawama kuwa kilichotamkwa kukuhusu wewe A,B,C ni uzushi.
Yaah tunajua uko kwenye vita,nawe unabudi kufungua silaha zako vinginevyo vita itakushinda na lawama utazibeba ukiziangatia bado kijana mdogo ambae unamiaka 35 mbele ya kutumikia Taifa lako sambamba na kina SUGU, na TINDU LISSU bila kujali unatoka chama gani.