Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA ahamia CCM, Nape asema Zitto ameogopa kwenda Igunga

Kuna mikoa hata ukisikia mwenyekiti wa CDM kahamia CCM wala haushtuki kwa kuwa watu wake bado hawajajitambua. Mfano Singida ndio mkoa ambao unaongoza kwa shida ya maji Tanzania baada ya miaka 50 ya uhuru. Nasikia wanaopata ajira ya ualimi vijijini mkoani Singida huwa wanashauriwa akipata mshahara wa kwanza anunue either Punda au Baiskeli ya kuchotea maji then anunue godoro na vitu vingine. Kwao hawaoni kama hilo ni tatizo na hawahitaji ukombozi. CCM inapendwa sana na wasioelimika, Maskini na mbumbumbu pamoja na wajinga wachache wanaojipendekeza ili wapate fedha au madaraka au upendeleo wa ajira kama Mwita25. Hongereni watu wa Singida kwa kukumbatia Shida, na kukumbatia CCM
 
Dewji anatumia pesa nyingi sana kuwanunua wapinzani ili kujiwekea mazingira mazuri ya kuendelea kushikilia kiti cha singida mjini.

Pia anatumia pesa nyingi kuwanunua wapinzani walio mkoani singida ili kukisaidia chama chake, ili serikali yake iendelee kumuachia akifanya biashara zake za kimagumashi.

Anafahamu kwamba kuwepo kwa Tundu Lissu kwenye halmashauri ya wilaya ya singida ni pigo kubwa na kutokana na uwezo na ushawishi wake wananchi wataitupa mkono ccm kwahiyo silaha pekee iliyobaki ni kuwanunua tu. Lakini hii mimi naona ni short term solution, muda muafaka ukifika watu watakula mihela yake na kura hawatowapa.

Na hakuna sababu ya chadema singida kuwa na mshituko kwa sababu ya kuondoka kwa Nakamia, atapatikana kiongozi mwingine mzuri kama yeye ama hata zaidi yake, nchi hii ina watu wengi mahiri na makini, ni suala la kupeana nafasi tu.
 
Magamba bwana, . . . .katika msafara wa mamba na kenge wamo,. . . Huyo diwani ni kenge katika chama chetu makini, . . .!!!!!!!
 
kuhama kwake huyo bwana singida kunatusaidia nini ss wanaigunga. Nape huo ni utoto hujakomaa kisiasa. haja kutoa hoja nyepesi kwa mambo yanayohusu msikabari wa wananchi.
 
hata kama waTZ wote wangehamia CCM kwame sitaweza tena kuiamini CCM at any cost, hizo no porojo za kitoto za CCM

Mpwa tupo wote nafikiri ndio tutakuwa hatuna chama mimimna wewe !
 
Jamani Nape anampokea mtu wa Chadema then anamtaja Zitto .Jamaa ni mpuuzi sana .Katoka kwa Slaa anahamia kwa Ziito ? Soon Zitto atatia timu sijui atasemaje.Zitto anaingia kuua last minutes sijui atasemaje .Ma CCM bana wanataka kuwapangia Chadema hata namna ya kufanya mambo yao ? Ama kweli hawa wako kima Saburi sana nimeamini leo .
 
karibu tena nyumbani nkamia, tangu awali nilijua wewe ni mtu makini sana huko ulipokuwa ulipotea njia, sasa tunawasubiri watu makini uliowaaacha huko kurudi nyumbani. Baba ni baba tu.

sura yako kama b. Kidude?

Anyway, wewe ni kati ya wanyonyaji wakubwa. Tumekuvumilia, sasa tumefika ukomo. Siku zako zinahesabika.
 
poleni wanachadema, na hongereni wanaccm. mimi simo. but ccm to hell.

CHADEMA wape hongera, na wape watanzania pole. CCM, cdhani kama wanatakiwa kupongezwa kwani wamepokea gamba limgine lililokuwa CDM
 
NA BASHIR NKOROMO, SINGIDA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameshushia kilio tena kwa CHADEMA baada ya Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Singida Mjini, Nakamia John kuhamia CCM.

Nakamia ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, alitangaza kuhamia CCM na kukabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Nape katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Urughu, jimbo la Iramba Magharibi mkoani hapa.

"Kama unakumbuka Mheshimiwa Nape, mimi ndiye nilikuvalisha gwanda la CHADEMA ulipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wetu mkuu kule Dar es Salaam, leo hii nimeamua niwe nawe katika chama makini CHama Cha Mapinduzi", alisema Nakamia na kuongeza.

"Ukiwa nje ya CHADEMA unaweza kudhani ni chama makini sana, lakini ni chama cha udikteta ukiokithiri, kisicho na utaratibu unaoeleweka, chenye viongozi wa ngazi za juu ambao wanapenda kila wanalotaka liwe hata kama haliwezekani".

Aliwataka Watanzania ambao bado wanadhani CHADEMA kina manufaa kuachana nacho haraka wasiendelee kugeuzwa mtaji wa maandamano ambayo alisema viongozi wa chama hicho huyapanga kwa lengo la kukusanya fedha kwa manufaa yao.

"Ninyi mnadanganywa kila siku eti nguvu ya umma, kumbe mnapumbazwa na kuacha kufanya kazi za maendeleo badala yake wanawapanga katika maanadamano, wanawapiga picha za video kisha wanapeleka kwa wafadhili kuombea fedha za kula wao ninyi mkiendelea kufa njaa", alisema Nakamia.

Akimpokea, Nape alimpongeza na kuwataka Watanzania wengine kuiga alivyofanya Nakamia akisema kwamba kila anayekiunga mkono CHADEMA asidhani kuwa atapata manufaa yoyote kimaendeleo.Akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Urughu, Simon Tyosela, Nape aliwataka wakazi wa Kata hiyo kuhakikisha wanampigia kura mgombea huyo wa CCM ili aweze kusimamia miradi yote iliyopangwa kutekelezwa katika eneo lao.

Nape alionya wananchi kutofanya makosa, akisema endapo wataacha kumchagua mgombea wa CCM wakampigia wa CHADEMA watambue kwamba wamekataa maendeleo kwa kuwa yale yote yaliyopangwa kutekelezwa yapo ndani ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachotawala.Uchaguzi mdogo unafanyika kwa lengo la kukidhi taratibu na sheria tu za nchi, lakini kimsingi hakuna kinachoweza kubadilishwa katika mipango ya maendeleo."Baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana, wananchi walichagua ilani ya kijani (ya CCM) kwamba ndiyo itekelezwe kwa miaka mitano hadi uchaguzi mkuu mwingine, kwa vyovyote vile anayefaa kupewa kujumu kusimamia lazima awe wa CCM", alisema Nape.

"Wewe unatambua kuwa sera zinazotekelezwa kwa sasa hadi miaka mitano ni za CCM na mipango yote iliyopo inatekelezwa chini ya ilani hiyo, unachagua mgombea mwenye ilani nyingine ambayo haina kazi, unataka kusimamisa au kuendeleza maendeleo kweli?" alihoji Nape.Alisema anao uhakika kwamba mgombea wa CCM taibuka na ushindi na alichokuwa akifanya juzi, si kuzindua tu kampeni bali kuandaa sherehe za mgombea huyo kutawazwa kuwa diwani wa kata hiyo.

"CHADEMA walishashindwa hata kabla ya uchaguzi kufika, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alishaliona hilo mapema ndiyo maana hakuweza kuja kuzindua kampeni za chama hicho hapa kama alivyokuwa amewaahidi." alisema Nape na kuongeza."Zitto aliposikia tu kuwa mimi nitakuja hapa akaona basi biashara imeingia ruba, akaamua kuingia mitini, kwa hiyo kwa kuwa hakuja hapa sitafanya kampeni maana imeshakwisha".

Aliwataka wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Tyosera na pia kuhakikisha wanazilinda kura hizo.Nape aliwataka Umoja wa Vijana wa CCM kuunganisha nguvu zao kuhakikisha siku ya uchaguzi kina mama na wazee wanakwenda kupiga kura bila kutishwa na yeyote hasa CHADEMA ambao alisema wana tabaia ya kukodi watu kutoka nje ya jimbo kuzuia wazee na wanawake kwenda kupiga kura.

Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Urughu unafanyika kufuatia Tyosera ambaye alikuwa diwani wa CHADEMA kujiuzulu na kuhamia CCM, na baada ya kuhamia CCM amegombea katika kura za maoni na kuongoza kwa kura nyingi.Akizungumza Tyosera alisema aliamua kuhama kujiuzulu na kuhamia CCM kwa sababu wakati akiwa diwani kwa tiketi ya CHADEMA kila akiwa katika baraza la Halmashauri alijiona kama kunguru ndani ya yangeyange.

-- Regards;-Bashir Nkoromo
Senior Photo/Journalist
Uhuru Publications Ltd,Publishers of Uhuru, Mzalendo and Burudani tabloids
Cell; +255 498008, +255 789 498008
P O Box 9221, Dar es Salaam.Tanzania
email: nkoromo@gmail.com, bnkoromo@yahoo.com.
-------------------------------------------------------Blog:Chachandu Daily Nkoromo Daily Blog


Hakuna cha ajabu. Wako wengi hao waliopandikizwa katika vyama vya upinzani na hakuanza yeye. Kuna akina Augustino lyatonga Mrema, tumewaona akina masumbuko lamwai, tunawaona wengi ambao wanajitambulisha waziwazi kuwa wako upinzani kwa kazi maalum. Shibuda, zitto kabwe??!!!, na wapinzani "fake" kama akina james mbatia, dovutwa na wengine wengi. Wapinzani wa kweli wapo wachache sana walio wengi ni vibaraka wa chama cha magamba na wakati wa chaguzi kama huu unaoendelea Igunga ndiyo wanafanya kama alivyofanya huyo ili tu kuwayumbisha watu. Bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuikomboa nchi hii.
 
Nape kashindwa hata kumaliza masters aliyoianza hawezi hata kupata ajira yoyote nje ya ufisadi. Anajitamba kama m-b-wa mlamba mchuzi
 
TZ kuna vyama vya upinzani zaid ya 18, kwa nn ssem waiogope chadema tu, kila wachojiham utasikia Ooh cdm watu wa maandamano/wahun nkSasa tutawaonyesha kuwa chadema si wahun ni wtu makin na werevu!!sasa nape nae bwana anenda kumnadi sijui diwan kwann asiende kumnadi mbunge kule igunga? kishamuwakia!!! ahahahahahah!!!!!
 
hongera Nkamia!! Karibu nyumbani tujenge Singida yetu na Tanzania. Usihesabu muda mwingi uliopoteza CHADEMA kwani huu ndio wakati wa kuumbua uongo wote wa CDM!!
 
jamani huyu nakamia alisharudi ccm toka mwezi wa tano na hizi habari zilishaandikwa hapa.
hawa magamba hawana lolote wamerudia tena hii habari kwa sababu wamekabwa koo igunga wakakosa la kuandika.huyu nakamia alikuwa mganga njaa hapo singida na hakuwa lolote zaidi ya kwenda kulia njaa kwa dewji.
hajawahi kuisaidia lolote cdm mimi nilikaa nae pale stanley motel kila alichokuwa anaongea anaongelea yeye kupata helasasa huko ccm alikoenda ndipo kuna hela za ufisadi ataweza kupata alichokuwa anatafuta.
 
jamani huyu nakamia alisharudi ccm toka mwezi wa tano na hizi habari zilishaandikwa hapa.
hawa magamba hawana lolote wamerudia tena hii habari kwa sababu wamekabwa koo igunga wakakosa la kuandika.huyu nakamia alikuwa mganga njaa hapo singida na hakuwa lolote zaidi ya kwenda kulia njaa kwa dewji.
hajawahi kuisaidia lolote cdm mimi nilikaa nae pale stanley motel kila alichokuwa anaongea anaongelea yeye kupata helasasa huko ccm alikoenda ndipo kuna hela za ufisadi ataweza kupata alichokuwa anatafuta.
Hata mimi nimeshangaa hii habari ya zamani sana nafikiri Uhuru labda wamekosa habari za kuandika au kila wakigusa za Igunga wanakuta za moto wanakuta CCM afumaniwa CCM abaka wanashindwa kuandika.
 
CDM its a time no to direct uamsho to Singida Region like what has been done to lake zone. these fellows at Sthey really needs to be unfed the majitaka doctrines from Magambas. lets do it quickly
 
Back
Top Bottom