Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA ahamia CCM, Nape asema Zitto ameogopa kwenda Igunga

Warofo

Member
Mar 15, 2011
77
62
NA BASHIR NKOROMO, SINGIDA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameshushia kilio tena kwa CHADEMA baada ya Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Singida Mjini, Nakamia John kuhamia CCM.

Nakamia ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, alitangaza kuhamia CCM na kukabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Nape katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Urughu, jimbo la Iramba Magharibi mkoani hapa.

"Kama unakumbuka Mheshimiwa Nape, mimi ndiye nilikuvalisha gwanda la CHADEMA ulipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wetu mkuu kule Dar es Salaam, leo hii nimeamua niwe nawe katika chama makini CHama Cha Mapinduzi", alisema Nakamia na kuongeza.

"Ukiwa nje ya CHADEMA unaweza kudhani ni chama makini sana, lakini ni chama cha udikteta ukiokithiri, kisicho na utaratibu unaoeleweka, chenye viongozi wa ngazi za juu ambao wanapenda kila wanalotaka liwe hata kama haliwezekani".

Aliwataka Watanzania ambao bado wanadhani CHADEMA kina manufaa kuachana nacho haraka wasiendelee kugeuzwa mtaji wa maandamano ambayo alisema viongozi wa chama hicho huyapanga kwa lengo la kukusanya fedha kwa manufaa yao.

"Ninyi mnadanganywa kila siku eti nguvu ya umma, kumbe mnapumbazwa na kuacha kufanya kazi za maendeleo badala yake wanawapanga katika maanadamano, wanawapiga picha za video kisha wanapeleka kwa wafadhili kuombea fedha za kula wao ninyi mkiendelea kufa njaa", alisema Nakamia.

Akimpokea, Nape alimpongeza na kuwataka Watanzania wengine kuiga alivyofanya Nakamia akisema kwamba kila anayekiunga mkono CHADEMA asidhani kuwa atapata manufaa yoyote kimaendeleo.Akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Urughu, Simon Tyosela, Nape aliwataka wakazi wa Kata hiyo kuhakikisha wanampigia kura mgombea huyo wa CCM ili aweze kusimamia miradi yote iliyopangwa kutekelezwa katika eneo lao.

Nape alionya wananchi kutofanya makosa, akisema endapo wataacha kumchagua mgombea wa CCM wakampigia wa CHADEMA watambue kwamba wamekataa maendeleo kwa kuwa yale yote yaliyopangwa kutekelezwa yapo ndani ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachotawala.Uchaguzi mdogo unafanyika kwa lengo la kukidhi taratibu na sheria tu za nchi, lakini kimsingi hakuna kinachoweza kubadilishwa katika mipango ya maendeleo."Baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana, wananchi walichagua ilani ya kijani (ya CCM) kwamba ndiyo itekelezwe kwa miaka mitano hadi uchaguzi mkuu mwingine, kwa vyovyote vile anayefaa kupewa kujumu kusimamia lazima awe wa CCM", alisema Nape.

"Wewe unatambua kuwa sera zinazotekelezwa kwa sasa hadi miaka mitano ni za CCM na mipango yote iliyopo inatekelezwa chini ya ilani hiyo, unachagua mgombea mwenye ilani nyingine ambayo haina kazi, unataka kusimamisa au kuendeleza maendeleo kweli?" alihoji Nape.Alisema anao uhakika kwamba mgombea wa CCM taibuka na ushindi na alichokuwa akifanya juzi, si kuzindua tu kampeni bali kuandaa sherehe za mgombea huyo kutawazwa kuwa diwani wa kata hiyo.

"CHADEMA walishashindwa hata kabla ya uchaguzi kufika, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alishaliona hilo mapema ndiyo maana hakuweza kuja kuzindua kampeni za chama hicho hapa kama alivyokuwa amewaahidi." alisema Nape na kuongeza."Zitto aliposikia tu kuwa mimi nitakuja hapa akaona basi biashara imeingia ruba, akaamua kuingia mitini, kwa hiyo kwa kuwa hakuja hapa sitafanya kampeni maana imeshakwisha".

Aliwataka wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Tyosera na pia kuhakikisha wanazilinda kura hizo.Nape aliwataka Umoja wa Vijana wa CCM kuunganisha nguvu zao kuhakikisha siku ya uchaguzi kina mama na wazee wanakwenda kupiga kura bila kutishwa na yeyote hasa CHADEMA ambao alisema wana tabaia ya kukodi watu kutoka nje ya jimbo kuzuia wazee na wanawake kwenda kupiga kura.

Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Urughu unafanyika kufuatia Tyosera ambaye alikuwa diwani wa CHADEMA kujiuzulu na kuhamia CCM, na baada ya kuhamia CCM amegombea katika kura za maoni na kuongoza kwa kura nyingi.Akizungumza Tyosera alisema aliamua kuhama kujiuzulu na kuhamia CCM kwa sababu wakati akiwa diwani kwa tiketi ya CHADEMA kila akiwa katika baraza la Halmashauri alijiona kama kunguru ndani ya yangeyange.


===============
-- Regards;-Bashir Nkoromo
Senior Photo/Journalist
Uhuru Publications Ltd,Publishers of Uhuru, Mzalendo and Burudani tabloids
Cell; +255 498008, +255 789 498008
P O Box 9221, Dar es Salaam.Tanzania
email: nkoromo@gmail.com, bnkoromo@yahoo.com.
-------------------------------------------------------Blog:Chachandu Daily Nkoromo Daily Blog
 

Mkuu wa chuo

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
7,532
5,204
sasa masnitch kama hao wakipigwa watasema nini, huwezi hama kimya kimya bila kuwaponda makamanda! Wote tunajua chama cha magamba hakifai, sasa kama snitch akiwa anaongea mambo ya hivyo inatia hasira kwa kweli...
 

NEW TANZANIA

Senior Member
Aug 15, 2011
101
25
Hela za dogo Mohd Dewji at work! It's time for CDm kuanza kumuanika Mohd Dewji na utajiri wake ambao unatokana na ufisadi na wizi kutoka kwa Watz.

umenena mkuu
hao ndio kenge wenye kwenye msafara wakionyshwa pesa wanakuwa kama machizi wanasahau hata familia
hata mashoga wangine ni matokeo ya kupenda pesa za bure
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,776
6,544
Hela za dogo Mohd Dewji at work! It's time for CDm kuanza kumuanika Mohd Dewji na utajiri wake ambao unatokana na ufisadi na wizi kutoka kwa Watz.

dogo kapewa chake, kwa kuwa alidhani atatoka ndani ya chadema na kaprove failure, kaamua kuingia CCM aidhani ndiko maisha mazuri yanakopatika.

hii ni kweli, kwani viongozi wa chama cha ccm, maslahi yao c haba ukilinganisha na wanachama wake hasa wale walio vijijini.

Afadhali amejiona ni gamba, bora ahamie kwa magamba wenzie
 

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
................Siasa uchwara na majitaka...mimi naongezea hayo maneno ya bosi wao Rostam...hizi zaidi ya kuwa siasa uchwara na majitaka ni siasa uharo...
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,776
6,544
sasa masnitch kama hao wakipigwa watasema nini, huwezi hama kimya kimya bila kuwaponda makamanda! Wote tunajua chama cha magamba hakifai, sasa kama snitch akiwa anaongea mambo ya hivyo inatia hasira kwa kweli...

mnyime udahili
 

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,337
Karibu tena nyumbani Nkamia, tangu awali nilijua wewe ni mtu makini sana huko ulipokuwa ulipotea njia, sasa tunawasubiri watu makini uliowaaacha huko kurudi nyumbani. Baba ni Baba tu.
 

MPG

JF-Expert Member
May 12, 2011
483
53
Amepewa pesa na majambazi CCM,ni bora kahama mapema mana hawa ndiyo wasaliti wakubwa wa Taifa hili wakishirikiana na majambazi CCM kuwarudisha nyuma kimaendeleo watanzania.
 

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,602
329
Nape hana lolote hawezi kujilinganisha na Zitto Kwabwe hata siku moja maana IQ ya Nape iko chini sana (uwezo wa kujua mambo na kujenga hoja na uelewa wake uko chini mno), hawezi kutoa hoja zenye maana mbele za watu! Kama hii ndo CCM baada ya kujivua magamba basi tusubiri 40 yao 2015 maana kilishakufa tayari
 

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,602
329
Habari kama hizi kuna watu zawaumiza sana...na bado...

Unaumia wewe mwenyewe bana sisi tunaongelea ukweli. Sasa hivi CCM wanaumia mno kuliko wakati mwingine wowote na watapeleka listi yao yote Igunga wanayoiamini na ndio mwisho wao. Chadema ikiamua nani atasimama?
 

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,602
329
Karibu tena nyumbani Nkamia, tangu awali nilijua wewe ni mtu makini sana huko ulipokuwa ulipotea njia, sasa tunawasubiri watu makini uliowaaacha huko kurudi nyumbani. Baba ni Baba tu.


CCM ni baba ndiye aliyezaa umasikini Tanzania na tutamgoa tu kwa gharama yoyote
 

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
641
Hela za dogo Mohd Dewji at work! It's time for CDm kuanza kumuanika Mohd Dewji na utajiri wake ambao unatokana na ufisadi na wizi kutoka kwa Watz.
Ukiona mpinzania anahamia CCM ujue anatamaa ya kupata pesa za mafisadi na pia ili mambo yake anayofanya kwa njia za panya ya nyooke.watu wa taifa hili wengi wamelogwa na CCM na hawauoni umaskini wao na hata wakiuona hawatambui.Tunahitaji Chadema ikomboe taifa letu.
 

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
641
CCM ni baba ndiye aliyezaa umasikini Tanzania na tutamgoa tu kwa gharama yoyote
Tena ccm inamuda mfupi wakufutika kabisa hapa tanzania bara tuombe Mungu asimamie ili tuandike katiba mpya na kuwa na tume huru ya NEC si watakimbilia wapi mafisadi makubwa hayo
 

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,602
329
Hata Yesu alipokuja Duniani walimkataa kuwa ndiye mkombozi, vivyo hivyo CDM wanaikataa kuwa ndo mkombozi wa watz lakini amini nawambieni sisi tunaamini ndo atakuwa mkombozi wetu tanzania. Mabadiliko hayaji kirahisi na hata Libya Gadaff hakupenda kuachia nchi kirahisi, Ivory coast, nk ndo ilivyo nasi tusikate tamaa mpaka kieleweke.
 

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,089
7,836
nape kujilinganisha na zitto ni kichekesho . huyo anaekimbilia chama kinachokufa tunamtakia kila la heri labda nia yake kubwa ni kuhudhuria maziishi yake.halafu kuna wanasiasa uchwara sana kila anaeingia cdm anataka awe kiongozi tena mkubwa .nenda ccm bwana utapewa ukuu wa mkoa bado mikoa mitano haijatangazwa.vipi yule mwenzio wa mbeya kapata kitu au alipotezewa siku ileile alivyohamia?
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom