Mjue nyoka mwenye sumu kali Barani Afrika

Mimi huwa sielewagi kabisa hasa kuhusu black mamba aka koboko nasomaga makala zake huku jamii forum ni za kutisha mpaka nashangaa.
Mkoa wa Kilimanjaro kuna huyu nyoka na huwa wakaazi wake hawamuogopi kabisa wakimuona lazima wamuue, mimi nimeuwa nyoka wengi sana disign hiyo. Pia kuna green mamba kwa kichaga huita usale, nyoka huyu ni vigumu kimuua kwa kuwa anapaa na kuruka umbali mrefu, kumuuwa mpaka umuotee akiwa amejininginiza juu ya majani anaota jua ndio umpige na fito ama kumkata na panga.

Kiukweli sijawahi kuogopa nyoka katika maisha yangu, siku zote nikiwaona nyoka nilikuwa nawakimbiza hata kuwauwa bila ya kujali ni aina gani ya nyoka mpaka chatu tumeua, kwa sasa jamii forum imenifanya nianze kuogopa nyoka tena sana, but ukinirudisha kwenye maeneo yangu ama kukabiliana nae hakika ata akiniuma na mimi lazima nitamuua hakuna namna atanizidi ujanja
Siamini kama koboko unaweza kuuawa kizembe kiasi hicho
 
Dah! Kiukweli hakuna kiumbe hai nakiogopa hapa duniani kama nyoka! Sijui ni kwa sababu tu ya ile dhana ambayo tulijengewa tangu tukiwa wadogo!

Yaani katika hili, sina tofauti na wale jamaa zangu wa Dar wanao ogopa Panya Road na Popobawa!
Itotoni nimeua sana cobra wale weusi ambao huchanua kichwa kama mwiko.
 
Vice versa,...nyoka ni kiumbe humble na mpole na mwoga kuliko viumbe vingne vyote..na ndomana anaish kwa kujificha sana akiogopa kifo..huwez mwona kizembe kama unavyoona mende au kuku...ni sabab anajua akionekana tu ni anauwa..na ndomana muda wote huwa anajificha jificha maskin ya mungu.
Kumuua nyoka siyo habari wala hasara, ila sasa yeye ukuue wewe
 
anaweza kusimama robo 3 ya mwili wake!na akakuangalia usoni..

sumu yake aina ya neurotoxin yenye protin nyingi.
akikuuma sumu yake inaenda kushut down nervous system ambayo hupelekea kuparalyze kisha mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi na kufa ndani nusu saa au lisaa!

ni nyoka mpole sana na hujiepusha na wanyama wakubwa kumzidi ikiwemo binadamu...
sababu hata akikuuma hawezi kukumeza!kwann akukimbize!

ukimuona porini kwa bahati mbaya we shika njia yako na yeye ataenda yake sababu hapendi ugomvi usiomuhusu
Comment yako inatisha sana mzee baba
 
Kwann watoto wadogo awaudhuriki na nyoka, sisi tunaita wanalindwa na malaika. Kitaalamu watoto ambao awajaota meno huwa hawana utambuzi wa mema na mabaya. Hivyo hawana hofu, hofu usababisha mapigo ya moyo kwenda mbio, na mwili unatoa kemikali fulani Ili ujilinde. Sababu mtoto hana hofu atoi hizo kemikali kupitia hizo kemikali sababu ya panic nyoka anakuwa ashapata alert kwamba huyu ni adui atakugonga sasa nyoka umuona mtoto ni SAwa na kitu tu au kama gogo.
Gogo linalojitikisa, au siyo?
 
Ukitaka kujua mziki wake jifanye kama unataka kumdhuru....

Amin amin nakuambia chini ya nusu saa utakuwa umeshakuwa historia. Nyoka ana kisirani na roho ya kikatili kama Hittler.

Usithubutu kumfanyia masihara huyu nyoka laanakum kabisa...
 
Sasa nyoka kukimbia speed ya binadamu huoni kama ni speed kali kwa hicho kiumbe? Tatizo mnataka kulinganisha na speed ya cheetah ndo mseme ana speed kali.
Mbona Kuna binadamu tu tunapepea mpaka 38km/h!
Sasa hiyo 16 si ndogo sana?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom