Mimi huwa sielewagi kabisa hasa kuhusu black mamba aka koboko nasomaga makala zake huku jamii forum ni za kutisha mpaka nashangaa.
Mkoa wa Kilimanjaro kuna huyu nyoka na huwa wakaazi wake hawamuogopi kabisa wakimuona lazima wamuue, mimi nimeuwa nyoka wengi sana disign hiyo. Pia kuna green mamba kwa kichaga huita usale, nyoka huyu ni vigumu kimuua kwa kuwa anapaa na kuruka umbali mrefu, kumuuwa mpaka umuotee akiwa amejininginiza juu ya majani anaota jua ndio umpige na fito ama kumkata na panga.
Kiukweli sijawahi kuogopa nyoka katika maisha yangu, siku zote nikiwaona nyoka nilikuwa nawakimbiza hata kuwauwa bila ya kujali ni aina gani ya nyoka mpaka chatu tumeua, kwa sasa jamii forum imenifanya nianze kuogopa nyoka tena sana, but ukinirudisha kwenye maeneo yangu ama kukabiliana nae hakika ata akiniuma na mimi lazima nitamuua hakuna namna atanizidi ujanja