Mjue nyoka mwenye sumu kali Barani Afrika

Mjue nyoka mwenye sumu kali Barani Afrika

Unamzidi ni kweli je unaweza hold kwa muda gani above that speed? Utakimbia kwa 22kph kwa umbali gani maana kumbuka huyo mshenzi hachoki anakuungia mwanzo mwisho[emoji23][emoji23][emoji23]
Binadam ndo kiumbe mwenye akili dunian hao viumbe wengine Kama nyoka ni mapunguani tu hawez kumaliza hizo km 16 bado anakufata tu labda awe nyoka alietumwa na waswahili ila nyoka wengi ukimkimbia na yeye anakukimbia kwakifupi Mungu alituumba tuogopane ila tuuwane inapobidi
 
Namfuatilia sana yule jamaa. Yule mara nyingi anakamata vinyoka vidogo kwenye majumba ya watu.... Akikutana na yule mwenyewe aliyekomaa mziki wake si wa kitoto...
Usimchukulie powa yule jamaa, wale nyoka wanatoka maporini kuja majumbani kwa watu kufuata joto na chakula (panya na vyura). Kwa hio wale ni nyoka wa porini kama walivyo wengine, sio wa kufugwa.
 
Mkuu nyoka hata awe mkubwa vp huwa anakamatwa tu,kimsingi nyoka ni muoga sana mpaka anafikia kiwango cha kushindwa kbsa kushambulia. Binafsi nimeshawauwa nyoka wakubwa bila upinzani wowote! Zaidi ya kujificha na kukimbia' kuna siku nilimshika ili kumzuia asikimbilie ndani ya nyumba ya mzee flni kule zenji.
Aisee we jamaa nimetokea kukuogopa. Nyoka mshenzi yule awe mwoga??
 
KOBOKO (BLACK MAMBA) Nyoka pekee mwenye spidi ya kasi kuliko nyoka wote duniani, ni nyoka wa kwanza kuwa na sumu kali barani Afrika na ni nyoka wa pili mrefu mwenye sumu kali baada ya King Cobra anayepatikana India.

Koboko anakuwa na kufika hadi urefu wa futi 14 na ana rangi ya kijivu na kahawia.

Sumu yake inau wezo wa kuua watu 20 kwa kuuma mara moja, koboko ni nyoka anapenda kuishi kwenye vichaka, vilima vyenye mawe mengi, mbugani na porini.

Ukikuta koboko wanapigana usiwafukuze utakuwa mtu moja mwenye bahati sana, kwa sababu mmoja akiumia mwingine anaenda kumtafutia dawa na kumletea mwenzake, ukimfatilia huyo anakwenda kufata dawa utakuwa umejua dawa ya sumu ya nyoka, inasemekana anachukua dawa aina tatu ila chunga sana asije akakuona unamfatilia atakukimbiza hadi akuume.

Kumuua nyoka huyu sio mchezo kwa sababu ni mwenye sumu kali sana na ni ambaye mwendo wake ni wa spidi ya kasi, ukifanikiwa kumuua hakikisha umemchimbia shimo refu na kumfukia kwa sababu mifupa yake ni Sumu ikikuchoma huponi.

Kwani nyoka ana mifupa ?
 
Mimi huwa sielewagi kabisa hasa kuhusu black mamba aka koboko nasomaga makala zake huku jamii forum ni za kutisha mpaka nashangaa.
Mkoa wa Kilimanjaro kuna huyu nyoka na huwa wakaazi wake hawamuogopi kabisa wakimuona lazima wamuue, mimi nimeuwa nyoka wengi sana disign hiyo. Pia kuna green mamba kwa kichaga huita usale, nyoka huyu ni vigumu kimuua kwa kuwa anapaa na kuruka umbali mrefu, kumuuwa mpaka umuotee akiwa amejininginiza juu ya majani anaota jua ndio umpige na fito ama kumkata na panga.

Kiukweli sijawahi kuogopa nyoka katika maisha yangu, siku zote nikiwaona nyoka nilikuwa nawakimbiza hata kuwauwa bila ya kujali ni aina gani ya nyoka mpaka chatu tumeua, kwa sasa jamii forum imenifanya nianze kuogopa nyoka tena sana, but ukinirudisha kwenye maeneo yangu ama kukabiliana nae hakika ata akiniuma na mimi lazima nitamuua hakuna namna atanizidi ujanja
 
Dah! Kiukweli hakuna kiumbe hai nakiogopa hapa duniani kama nyoka! Sijui ni kwa sababu tu ya ile dhana ambayo tulijengewa tangu tukiwa wadogo!

Yaani katika hili, sina tofauti na wale jamaa zangu wa Dar wanao ogopa Panya Road na Popobawa!
 
anaweza kusimama robo 3 ya mwili wake!na akakuangalia usoni..

sumu yake aina ya neurotoxin yenye protin nyingi.
akikuuma sumu yake inaenda kushut down nervous system ambayo hupelekea kuparalyze kisha mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi na kufa ndani nusu saa au lisaa!

ni nyoka mpole sana na hujiepusha na wanyama wakubwa kumzidi ikiwemo binadamu...
sababu hata akikuuma hawezi kukumeza!kwann akukimbize!

ukimuona porini kwa bahati mbaya we shika njia yako na yeye ataenda yake sababu hapendi ugomvi usiomuhusu
Au Ndio maana Biblia inasema Tuwe na busara kama nyoka?!!
 
Mimi huwa sielewagi kabisa hasa kuhusu black mamba aka koboko nasomaga makala zake huku jamii forum ni za kutisha mpaka nashangaa.
Mkoa wa Kilimanjaro kuna huyu nyoka na huwa wakaazi wake hawamuogopi kabisa wakimuona lazima wamuue, mimi nimeuwa nyoka wengi sana disign hiyo. Pia kuna green mamba kwa kichaga huita usale, nyoka huyu ni vigumu kimuua kwa kuwa anapaa na kuruka umbali mrefu, kumuuwa mpaka umuotee akiwa amejininginiza juu ya majani anaota jua ndio umpige na fito ama kumkata na panga.

Kiukweli sijawahi kuogopa nyoka katika maisha yangu, siku zote nikiwaona nyoka nilikuwa nawakimbiza hata kuwauwa bila ya kujali ni aina gani ya nyoka mpaka chatu tumeua, kwa sasa jamii forum imenifanya nianze kuogopa nyoka tena sana, but ukinirudisha kwenye maeneo yangu ama kukabiliana nae hakika ata akiniuma na mimi lazima nitamuua hakuna namna atanizidi ujanja
Siku kam face koboko uone shoo yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom