Mjue nyoka mwenye sumu kali Barani Afrika

Mjue nyoka mwenye sumu kali Barani Afrika

Ukikuta koboko wanapigana usiwafukuze utakuwa mtu moja mwenye bahati sana,kwasababu moja akiumia mwingine anaenda kumtafutia dawa na kumletea mwenzake, ukimfatilia huyo anakwenda kufata dawa utakuwa umejua dawa ya Sumu ya nyoka,inasemekana anachukua dawa aina tatu Ila chunga Sana asije akakuona unamfatilia atakukimbiza hadi akuume
Ahahah.......hizi story zinanikumbusha kipindi kile hakuna tv
 
Kumbe hana makuu eeh? Binadamu ndiye mchokozi?
Hana makuu ila ana hasira na sumu kali sana anaweza kuuwa hata familia nzima kama atashambuliwa, niliwahi kwenda sehem moja kijijin wanapo ozesha udongo wa dhahabu n katkat ya mapori usiku unaskia wanavolia wanasauti kal sana ukiiskia tu hofu lazma ikuingie , sasa hiyo night huwa tunawasha Moto kwaajili ya kuota kutokana na barid kali sasa hao viumbe wakishajionea hivyo wanasogea zao mbali kdogo japo hawaendi mbali ila hawaji kukushambulia labda ujipeleke mwenyewe ukawashambulie
 
Huwa namcheki sana NATIONAL GEOGRAPHIC mbona yeye huwa anawakamata na kutupa somo namna sumu yake inavyo athiri pindi anapokuuma.

Ni kweli ana sumu kali sana.

Lkn umeona watu wanavyomuelezea..? Kwamba anakimbiza watu
akikuamulia sijui anakuwekea kisasi atakusaka hadi akumalize!

Anaweza kukufukuza kutoka maporini, hata ukikimbia kwa gari utamkuta nyumbani kwako anakusubiri akugonge!

Sasa huyo tena nyoka au Komando Kipensi..!?
 
Ni kweli ana sumu kali sana.

Lkn umeona watu wanavyomuelezea..? Kwamba anakimbiza watu
akikuamulia sijui anakuwekea kisasi atakusaka hadi akumalize!

Anaweza kukufukuza kutoka maporini, hata ukikimbia kwa gari utamkuta nyumbani kwako anakusubiri akugonge! Sasa huyo tena nyoka au Komando Kipensi..!?
wabongo kwa kuongeza chumvi utawaweza,mtu hata kama kitu hana uhakika nacho anabwabwaja tu

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli ana sumu kali sana.

Lkn umeona watu wanavyomuelezea..? Kwamba anakimbiza watu
akikuamulia sijui anakuwekea kisasi atakusaka hadi akumalize!

Anaweza kukufukuza kutoka maporini, hata ukikimbia kwa gari utamkuta nyumbani kwako anakusubiri akugonge! Sasa huyo tena nyoka au Komando Kipensi..!?
watu wanakoleza mpaka inapitiliza sasa nyoka anapewa sifa ambazo hana
 
Kila kitu ni sifa, either iwe kubwa au ndogo ndiyo sifa yake.

Mfano: kobe anasifika kwa upole wake na mwendo wake wa taratibu. Hiyo ni sifa tayari.
So, ukubwa au udogo usikuumize kichwa.

Na nikisema maximum speed haimaanishi, ni speed kubwa bali niukomo wa juu wa speed wa kiumbe fulani. Na kila kiumbe anamaximum speed yake.
Wewe kubali tu umeandika pumba.

16km/h ndio useme "nyoka ana fastest speed" kwamba ana mbio sana, akakukimbiza huchomoki?

Ach ujinga. Kama hujui kitu funga kopo
 
anaweza kusimama robo 3 ya mwili wake!na akakuangalia usoni..

sumu yake aina ya neurotoxin yenye protin nyingi.
akikuuma sumu yake inaenda kushut down nervous system ambayo hupelekea kuparalyze kisha mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi na kufa ndani nusu saa au lisaa!

ni nyoka mpole sana na hujiepusha na wanyama wakubwa kumzidi ikiwemo binadamu...
sababu hata akikuuma hawezi kukumeza!kwann akukimbize!

ukimuona porini kwa bahati mbaya we shika njia yako na yeye ataenda yake sababu hapendi ugomvi usiomuhusu
Mhhh mbona inasemekana koboko ni nyoka anaependa shali kwa maana hata akiwa mdogo akikuona atakufuata ili mradi afanye ugomvi na wewe, tofauti na nyoka wengine wanapokuona hukimbia
 
Wewe kubali tu umeandika pumba.

16km/h ndio useme "nyoka ana fastest speed" kwamba ana mbio sana, akakukimbiza huchomoki?

Ach ujinga. Kama hujui kitu funga kopo
Sio mawazo yangu, bali ni watu walikaa chini wakafanya research then wakapata majibu.
Wewe ambaye ni intellectual weka facts zako, kwa maana facts sio taarabu.
 
Nyoka hadi kuuma mtu ni pale ambapo Hakuna jinsi labda umemkurupua so anajihami, porini nyoka au chui uwaona watu kabla hata ya sisi kuwaona na ujificha na wanajua kama umewaona au ujawaona kama ujawaona hawawezi kukudhuru, labda tu kama umeonyesha dalili za kutaka kupambana nao ni lzm wakushambulie haraka Ili wajihami. Ingekuwa wanaua hovyo watu kesi zingekuwa nyingi watu kuuwa porini, pili ukaa mbali sana na makazi au shughuli za binadamu Ili kuepuka kasheshe maana wanajua mwanadamu mtata mziki wake hawauwezi.
 
Namfuatilia sana yule jamaa. Yule mara nyingi anakamata vinyoka vidogo kwenye majumba ya watu.... Akikutana na yule mwenyewe aliyekomaa mziki wake si wa kitoto...
Mkuu nyoka hata awe mkubwa vp huwa anakamatwa tu,kimsingi nyoka ni muoga sana mpaka anafikia kiwango cha kushindwa kbsa kushambulia. Binafsi nimeshawauwa nyoka wakubwa bila upinzani wowote! Zaidi ya kujificha na kukimbia' kuna siku nilimshika ili kumzuia asikimbilie ndani ya nyumba ya mzee flni kule zenji.
 
Kwann watoto wadogo awaudhuriki na nyoka, sisi tunaita wanalindwa na malaika. Kitaalamu watoto ambao awajaota meno huwa hawana utambuzi wa mema na mabaya. Hivyo hawana hofu, hofu usababisha mapigo ya moyo kwenda mbio, na mwili unatoa kemikali fulani Ili ujilinde. Sababu mtoto hana hofu atoi hizo kemikali kupitia hizo kemikali sababu ya panic nyoka anakuwa ashapata alert kwamba huyu ni adui atakugonga sasa nyoka umuona mtoto ni SAwa na kitu tu au kama gogo.
 
Mkuu nyoka hata awe mkubwa vp huwa anakamatwa tu,kimsingi nyoka ni muoga sana mpaka anafikia kiwango cha kushindwa kbsa kushambulia. Binafsi nimeshawauwa nyoka wakubwa bila upinzani wowote! Zaidi ya kujificha na kukimbia' kuna siku nilimshika ili kumzuia asikimbilie ndani ya nyumba ya mzee flni kule zenji.
Uoga,hofu ya kifo na simulizi nyingi kuhusu nyoka zimepelekea wengi kuwaogopa nyoka.
Nyoka yeyeto iwe kobra, kiboko, nk anadhibitiwa vizuri tu na mwanadamu
 
KOBOKO (BLACK MAMBA) Nyoka pekee mwenye spidi ya kasi kuliko nyoka wote duniani, ni nyoka wa kwanza kuwa na sumu kali barani Afrika na ni nyoka wa pili mrefu mwenye sumu kali baada ya King Cobra anayepatikana India. Koboko anakuwa na kufika hadi urefu wa futi 14 na ana rangi ya kijivu na kahawia.

Sumu yake inau wezo wa kuua watu 20 kwa kuuma mara moja, koboko ni nyoka anapenda kuishi kwenye vichaka, vilima vyenye mawe mengi, mbugani na porini.

Ukikuta koboko wanapigana usiwafukuze utakuwa mtu moja mwenye bahati sana, kwa sababu mmoja akiumia mwingine anaenda kumtafutia dawa na kumletea mwenzake, ukimfatilia huyo anakwenda kufata dawa utakuwa umejua dawa ya sumu ya nyoka, inasemekana anachukua dawa aina tatu ila chunga sana asije akakuona unamfatilia atakukimbiza hadi akuume.

Kumuua nyoka huyu sio mchezo kwa sababu ni mwenye sumu kali sana na ni ambaye mwendo wake ni wa spidi ya kasi, ukifanikiwa kumuua hakikisha umemchimbia shimo refu na kumfukia kwa sababu mifupa yake ni Sumu ikikuchoma huponi.

Kuna ukweli na uwongo katika haya uliyo andika. Koboko hawafufuani hata siku moja na kupigana kwao ni nadra sana kwani hawaishi karibu karibu. Mmoja akijuwa sehemu aliopo kuna mwenzake basi atatafuta kila sababu aondoke wasikutane na kupigana na ikitokea wanadundana basi anayeelemewa atakimbia hiyo sehemu. Mimi ni mtaalam wa nyoka na nimeshashuhudia koboko wakipigana tena porini na si in captivity (kufugwa).
 
Sumu Kali sio tatizo, jee wangapi barani Afrika wameng'atwa na koboko kila mwaka ukilinganisha na Puff Adder?

Distribution ya Koboko hii hapa. Hapatikani TZ nzima, maeneo ya kusini koboko hamna.
Black Mamba Distribution.jpg


Distribution ya Puff Adder hii hapa chini.



Puff Adder Distribution.png



Kwa hivyo, licha ya yote, nyoka hatari zaidi barani Afrika ni Puff Adder. Nyoka anayeua wengi sana Africa ni Puff Adder
Puff Adderr camouflage.png


kwa sababu zifuatazo;

1. Anapatikana karibu kila mahali except Jangwa la Sahara.
2. Mfumo wake wa kuwinda ni kulala sehemu moja akiwa camouflaged hata kwa zaidi ya wiki mbili hadi pale windo litakapoingia kwenye 18 zake. Kwaio ni rahisi sana kukanyagwa na binadamu bila kujua. Hapo unang'atwa. yeye hupenda kulala njiani akiwa kwenye majani.
 
Back
Top Bottom