Sawa. Mimi napata shida kidogo.
Miradi tunayoianzisha ni ya fedha nyingi sana, lakn ndio hapo tafakuri ya kina ilipotufikisha? Angalia hii miradi na nitafafanua kiduchu:
1. Flyovers Ubungo na Tazara
2. Rail - SGR
3. Umeme Stigler gorge
4. Ndege 6- Bombadier
Fly over ya tazara itahamisha foleni pale tazara kuileta Gerezani wkati wa asubuhi na jioni kuanzia karakata hadi Banana hapatapitika. Tumefanya nini sasa? Tatizo limebaki pale pale!
Fly over ya Ubungo - kuanzia manzese hadi magomeni na hata fire hakutapitika kutakuwa na foleni ya kutisha na wakati wa jini kimara hakutaendeka. Hatuitaji elimu kubwa sana kubaini haya niyoandika hapa
Rail - SGR - Private sector ya nchi hii iko hoi sana, Hakuna mipango ya kuvutia FDI. Bila mizigo ya kutosha ni hasara sana kuwa na hizo Train.
Stiglars Gorge - Kwa hali tuliyo nayo huo umeme utakamilika kwa vizazi vijavyo kama tutabahatika kupata awamu zenye watu wenye upeo kinyume cha hapo tusahau kwa awamu za aina hii.
Bombadier 6 - sawa kuwa na ndege, nani anapanda hizo ndege, tulikuwa na tatizo kiasi gani la ndege hapa nchini wakati wananchi wengi hawatumii huo usafiri?
Mipango ni mizuri lakn nini kilitakiwa kuanza? Tungeboresha maendeleo ya watz (social devt) kwanza na baada ya hapo ndiyo ifuate maendeleo ya vitu (Econ devt)
Nimekuelewa kuwa unapata shida mkuu, mimi niko pale pale kwamba tunajaribu kuangalia matokeo kwa muda mfupi kwamba:-
Stieglers Gorge itafaidisha vizazi vijavyo na siyo sisi tuliopo hapa na hata ikiwa hivyo tutakuwa bado tumefanya la maana leo,lakini kuhusu muda wa Mradi huu ungefuatilia aliyeupigia chapuo huu mradi anautegemea kwa muda upi na kwa malengo gani.
Kwamba hautasaidia nchi yetu kupata umeme wa Uhakika na kushusha gharama za Umeme ambazo zitashusha gharama za Uzalishaji viwandani na matumizi ya majumbani kwa maana ya Wananchi wataacha matumizi ya Miti km nishati ya kupikia?Na kutoa matokeo chanya ya Ulinzi/ Uhifadhi wa misitu?
Kuhusu SGR kweli nayo ujaji wake hautaokoa muda ktk Usafirishaji wa mizigo na abiria ambao sasa watakuwa wamerahisishiwa USAFIRI wao na Mizigo kutoka na kwenda mji wa KIBIASHARA wa Bandari Dar as Salaam?
Halkadhalika kuhusu ndege pia kulaumu ujaji wake kwamba pesa zimeenda pasipo nayo si sahihi kumbuka ukijumlisha kuwa watanzania hawapandi ndege kimtazamo nayo haiko sawa Tanzania sasa iko kwenye ushindani wa kibiashara na ktk Upande kwa miaka mingi kilituangusha ni ndege kwa maana hata kwenye sekta ya Utalii,Watalii huliangalia suala la USAFIRI wa Anga siyo kwamba ashuke Dsm halafu aendako aende kwa basi ndiyo maana kuna Upanuzi wa Viwanja na Ujenzi wa vipya kwa maana gani tuna mikoa hapa nchini ina Uzalishaji na fursa kubwa ila shida ikawa usafiri wa Uhakika ndege zitasaidia kutoa abiria wa kuunganisha kutokea nchi nyingine na kuletwa hapa na kupelekwa kwingine ambapo hii ilitegemewa nchi jirani.
Flyovers kwamba zitaleta foleni hili ni mtazamo lakini muhimu ni kungoja ziishe tuone changamoto ambazo pia zitapata majibu, maana hata Ujenzi wa Barabara zaMwendokasi zilileta Usumbufu lakini leo hii imekuwa haueni kwa wakazi wa Nje ya Jiji waliokuwa wanajihimu saa10 alfajr kwenda mjini sasa muda umepungua,na hata magari wengi huyaacha Kimara mwisho hii kiuchumi binafsi imewabeba wamiliki ambao kwenye suala la nishati ya mafuta Siku za kazi limewaondoka kiuchumi hili wengi hata wasomi hawaliangalii yaani uchumi wa mtu mmoja mmoja kuwa umebadilika kwa hayo mabasi tu ni kwa vile Waafrika huwa huwa hatuna rekodi za matumizi kwa mwezi nk.
Maendeleo ya Watu hayaji bila kuweka sawa Maendeleo ya Vitu vya kuleta Maendeleo.
RELI,NDEGE,AFYA,BARABARA &UMEME ni muhimu,hasa ikiwa uwezo upo KAMA SI LEO NI LINI?
Bado tuna Upanuzi wa BANDARI ambao utasaidia kuongeza MELI KUBWA ambazo zilikuwa haziji hapa kutokana na kuwa na Mlango na Kina Kidogo?
Ni suala la kuwapa Muda tu wenye dhamana.
Bila shaka UKAMILIFU wa haya yataleta mageuzi makubwa ya KIUCHUMI tuyategemeayo.
Nionavyo TULICHELEWA MNO.
Sent from my SM-G532F using
JamiiForums mobile app