Mjue mshauri wa Rais Magufuli anayedumaza uchumi

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
454
1,264
Mheshimiwa Magufuli unakuwa accountable na yanayoendelea Nchini kuhusu Uchumi kuporomoka tatizo lipo kwa kumsikiliza mshauri wako.

Mkuu wetu anaye mshauri wa Uchumi ambaye ni Philipo Mipango, Katibu Mtendaji wa zamani wa tume ya mipango na Waziri wa Fedha wa sasa.

Huyu ndo anayeleta yote yanayotokea sasa. Mkuu anamuamini sana. Hakuna cha zaidi alichofanya Mipango cha pale tume ya Mipango zaidi ya kugombaniana majukumu na Wizara ya Fedha na tume ya taifa ya takwimu.

Bwana Mipango, ni lini contractional fiscal policy zilisaidia kuinua Uchumi kwa Nchi inayoendelea kama Tanzania ambayo private sector bado ipo weak?

Kuna watu walimsaidia sana Mkapa na kikwete ambao Mkuu wa Nchi umewatoa. Dr. Likwilile huyu ni kifaa kamsaidia sana Mkapa kwenye kuandika papers na presentation mpaka nchi ikafutiwa Madeni na mashirika ya kimataifa.

Magufuli tunakuomba mtoe waziri wa fedha na huyu msaidizi wake Katibu Mkuu bado mdogo kwa majukumu hayo. Senior officer to katibu mkuu wa wizara sidhani katibu mkuu wa wizara sidhani kama ataweza kumchallenge mshauri wako (waziri)

Tunamlaumu Magufuli kuhusu kuyumba kwa uchumi, watanzania sasa hivi tupo kwenye recession( mdororo wa Uchumi).

Wafanyakazi wanapunguzwa sekta binafsi, biashara zimekwama, ujenzi umesimama.kila kitu mkwamo tu.

Sisi wananchi tunataka output.. Tunataka end results.. Blah blah sijui Viwanda vimeongezeka hatutaki. Viwanda vya kufikilika hivyo.

Magufuli sisi wengne tumekuchagua binafsi tunakumbuka uwezo wako kwenye wizara ya ujenzi. Kama mwananchi wa kawaida najukumu la kukukosoa na kukushauri kwakuwa Nchi yetu inafuata misingi ya demokrasia.

Naheshimu pia mamlaka ya Rais uliyonayo but hiyo haituzuii kukukosoa na kukushauri ukiwa km Rais wetu uliyepatikana kwa kura zetu.

Mtoe mipango abakuharibia Nchi. Sera anazokushauri haziwezi kuwork katika dunia ya tatu.

Dr. Philip Mipango ni lini contractional fiscal policies zilisaidia kwenye developing countries??.

Siyo kila mtu anapiga kelele kuhusu hali mbaya ya mtaani alikuwa anapiga dili.

Note; tafsir ya contractional fiscal ni kuongeza + kupunguza government expenditure! Recession hakuepukiki

Matumizi ya Kiswahili: EAC igeni mfano wa AU, Magufuli kaonesha Njia

Attack za CCM Mtandao vs. CHADEMA Mtandao - JamiiForums
 
Uko sawa kabisa, ila tatizo la Mkuu binafsi ni kwamba mwenyewe hapendi watu matajiri, na kila Siku anataka waishi kama mashetani, kumbe inatakiwa ajue 100% ya masikini mlo wao unategemea matajiri, that mean, matajiri wakiishiwa pesa basi ujue utazika masikini wote kwa njaa,
 
Bure kabisa, we humuoni zito? Hata hivyo huenda hana kosa bali anaeshauriwa
 
Watu wanatofautiana kuna waliotaka ushauri na washauri wa BRN ue/waendelezwe. Na kweli BRN pasenti yake ni kubwa kwenye bajeti ya taifa.

Na washawasha!
 
unamsingizia bure tu bwana yule mwenyewe ndio tatizo hana uwezo wa kuongoza ana uwezo wa kutawala tu ndio maana anatawala tu ila hawezi kuongoza , 2020 sio mbali tutajuana tu safari hii hata wakiiba na sisi tunaiba ,safari hii wao ndio wanaibiwa
2020 sio mbali?, labda kwako, sisi wengine tumemchoka kabisa tunataka hata kesho atoke, aende akalime mashamba yake
 
Aggressive fiscal policy ndio tatizo kubwa la Tanzania ya Dr. Magu.

Over time, tax base ita-shrink na atajikuta na vyanzo vichache sana vya kukusanya kodi coz biashara nyingi zitakufa au kudorora.

Kabla mambo hayajawa mabaya zaidi, JPM inabidi abadili fiscal policy ili iwe pro-growth. Hiyo mikodi yake haiko sustainable kiuchumi.

Ikumbukwe kuwa kiviwanda bado tuko nyuma sana. JPM inabidi afanye kazi ya ziada kuboresha hali hii. Mbaya zaidi idadi kubwa ya viwanda vya Tanzania vinategemea soko la ndani ambalo limeathiriwa sana na kuanguka kwa uwezo wa walaji kununua bidhaa na huduma.

Aidha, kote duniani serikali ndio chanzo kikuuu cha kuchochea mzunguko wa fedha katika uchumi. JPM kafanya makosa makubwa mawili katika eneo hili. Mosi, kuondoa pesa ya serikali kutoka mabenki binafsi kumechangia pia tatizo la mdororo wa mzunguko wa fedha mtaani kwani fedha hizi zilitakiwa zifikie sekta binafsi kwa njia ya mikopo. Tayari mabenki yameshaanza kulalama ukata.

Pili, serikali ya JPM imeziamuru taasisi na mashirika yote ya umma kufanya kazi zenyewe kwa zenyewe kwa kadri inavyowezekana. Mfano, matengenezo ya magari ya serikali lazima yafanyikie TEMESA, vikao kufanyikia kwenye kumbi za serikali badala ya kumbi za mahoteli binafsi nk. Hii ina maana kwamba pesa ya serikali inazunguka ndani kwa ndani na inatoka nje ya serikali kwa uchache sana. Hii inadumaza au kuua sekta binafsi sana ambayo ndio chanzo cha kodi kwa serikali na chanzo kikubwa cha ajira kwa watanzania wengi.
 
Back
Top Bottom