Kwanza nakubaliana na wewe waziri Mpango abadilishwe nafasi hiyo! sina tatizo na usomi wa hadhi ya doctorate lakini pengine tusitizame title tu na makaratasi (vyeti) tuvuke hapo kama nchi, kwa nafasi za juu kama mawaziri na makatibu wakuu ni wakati sasa tuwe na mfumo unaotizama uwezo wa mtu zaidi ya vyeti na titles!! lakini niwe tofauti kdg na wewe kwamba Mpango hakutuma maombi kuwa waziri wa fedha, lakini nina uhakika hata Rais inawezakana wala hakuwa anmjua Mpango, viko vyombo vimepewa jukumu la kuscout watu ambao watatufaa km taifa hao ndio tuwalaumu kwa sababu hawafanyi kazi yao sawasawa!! ni wavivu..! si kweli ni Mpango tu kati ya watanzania wote aliyeonekana anaweza kuwa waziri wa fedha kwa kipindi hiki..! wenye jukumu hili wakifikiri nje ya box watapata wengi tu na mmoja wao anaweza kutufaa sana. Sikubaliani na wewe pia kuretain watu ambao wamelisaidia taifa hili kwa namna moja au nyingine kama Likwelile alitufaa juzi na jana inatosha tupate wengine. kazi nyeti kama hizo ni vizuri na inafaa kuwa na akiba ya kutosha ya watu kwa nafasi hizo, binadamu tumewekewa ukomo kwa kila jambo, umri, akili, umbo nk hiyo ndiyo principle ya alietuumba, inawezekana Likwelile alitufaa jana likin km tunaendelea kudhani atatufaa na leo tunajidanganya. Kwa hiyo kwa kifupi si Rais wala Mpango wa kulaumiwa, tuwalaumu hao tuliowapa jukumu la kupick team ya kumsaidia Rais, na mara nyingi tu wamefeli assignment hii imeshakuwa kawaida kwao kufeli feli ni kama sasa wanafanya kazi ya uganga wa kienyeji (kupiga ramli) hawana uhakika na wanaowafanyia vetting kama wanafaa au la..pengine kati ya mambo ambayo katiba yetu iyaseme kwa future ya nchi yetu, usaidizi wa Rais uwe na ukomo, Rais anapomaliza muda wake kikatiba wasaidizi wake pia hasa pale ikulu nao wapishe watu wengine wapya! GOD HAS MADE NO SUPERMAN!!!