Mjue "Mbokoo" kibaka aliyewahi kuitikisa Kigamboni-Dar kabla ya kudhibitiwa kwa mbinde na Polisi

Alikuwa anazo nguvu na uwezo kama kuliko Tembo? anaweza kupambana na Simba peke yake??, anaweza kuua Nyati kwa mikono mitupu?

Hao wanyama wote, Tembo, Simba na Nyati mbele ya risasi hawakohoi sembuse Mtu mmoja mwenye Sifa kidogo za ajabu (peculiarity) ndiye atambe mbele ya Risasi?

Kuna mnyama mmoja, nadhani ni "honey Badger", huyu ukimpiga mkuki au Panga au kitu chenye ncha kali hakitoboi ngozi yake, huyu ndiye mnyama mwenye ngozi ngumu kupenyezeka kuliko wanyama WOTE,, lakini mbele ya Risasi ngozi yake haifui dafu, Risasi inapenya kama kupenya kwenye karatasi.

Risasi ni habari nyingine, huyo Mbokoo anaweza kutodhuriwa na vitu vingine kama kisu, panga nk, lakini sio Risasi, Risasi inapenya katika mwili wa binadamu yeyote.
Watu wanamfananisha Mbokoo na hisia za Kinjekitile Ngwale ambaye pia falsafa zake zilifeli mbele ya njugu. Aliwaaminisha misukule wake kwamba mkwasa usingewadhuru wakiita maji...majii matokeo yake walidondoka kama Nzige waliopikwa dawa ya Rungu!
 
nyie watu wa Dar siwaelewagi kama mlikua mnawakimbia komandoo yoso watoto wadogo.ndio maana ata wasanii wenu walivyowazingua wasanii wa chuga wakaamua kuja dar hukohuko kuja kuwatuliza!

Dar hakuna kitu hakuna wababe ni story tu tena huko kigamboni kinondoni magomeni nk.naweza tembea mwenyewe vijana wamekua walaini sana
Wewe kama Mbabe tunakutupa mitaa ya keko tu! Hio bangi yako ya Chuga itaisha ndani ya muda mchache sana. We ukisikia Dar unahisi ni kinondoni tu kwa mabishoo?
 
Wewe kama Mbabe tunakutupa mitaa ya keko tu! Hio bangi yako ya Chuga itaisha ndani ya muda mchache sana. We ukisikia Dar unahisi ni kinondoni tu kwa mabishoo?
Keko hakufai kabisa,
Niliwahi kubananishwa na watoto wadogo wawili kwenye chochoro za KEKO MACHUNGWA wanadai niwape Simu na pesa.

Nkaona dharau hizi, almanusra niwatie makofi watoto wale.

Ile nmemkunja mmoja Koo,

Kumbe wana backup ya njemba 4 vipande vya watu. Gafla wakatokea

Dah! Nlkua mpole ghafla.

Elfu 18 ilinitoka pale pale Kama faini, Simu ilinusurika coz mmoja wa zile njemba tuliwahi kufahamiana K'KOO enzi hizo yeye akiwa bodaboda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa mitaa ya mbeya simike huko alikua anaitwa jairo na mwenzie chanda,alafu umkute na semeni hao sasa huyo jamaa wa kigamboni mngekuta kavalishwa kanga na piko kachorwa kabisa.hata waliishia wapi sijui.

Singida huko kuliku na Tembo Senge mtoto wa mtemi Senge na Mdogo wako akaibuka badai Selemani Senge hao watu nyie sikieni tu sijui Nao sijui wako wapi.
Ila hao wanaoneaga warembo waje wafanye utukutu Apo Airwings wapite tu pikipiki karibu na ukuta wakutane na vyuma
 
Wewe kama ni mhalifu usijaribu kutia maguu yako Zanzibar, nakuhakikishia hautatoka labda ukiingia unyooshe mikono kuwa unabadilika. Cheza michezo yako bara na sio hiki kisiwa.Muulizeni Makame atawaambia sababu...
Unapigwa uku una chabwa
 
Mkuu mbokoo alikuwepo. Mimi story zake nilizisikia na kushuhudia vurugu miaka ya 2013. Ila sio zote Kama za mtoa mada

Sipingi kama hakuwepo, napinga hizi habari zake, haya matukio yake ni makubwa ilifaa hata Dar nzima tumjue, sasa iweje mie mkazi wa Kigamboni na nisimsikie, nimelenga kusema mtoa mada apunguze chumvi kidogo.
 
Back
Top Bottom