Mjue "Mbokoo" kibaka aliyewahi kuitikisa Kigamboni-Dar kabla ya kudhibitiwa kwa mbinde na Polisi

Asee ni kweli mbokoo alikua hatari sana ila hakua mkorofi kabisa mchana kwa mtu ambae humjui ni ngumu kufahamu labda mwili wake ulivyo ndo unaweza kuhisi ila yy alikua mkorofi kwa vibaka wenzake, hakua na mwili wa kutisha sanaa ila amejengeka kimazoezi ya karate ambayo alianza kujifunza pale pale navy akiwa na lugu ambaye uyu ndo sifa nyingi wanampa mbokoo..
Ukiwa ferry upande wa mabaharia uku kushoto wana hucheza sana kamari sasa mbokoo ndo ilikua akifika anakauli yake "wana mnachezea ela wakati sisi tunazitafuta " apo wakati anasema hivyo anazichukua tayari sasa piga hesabu miili ya mabaharia afu wananywea yy hua anamtaka yule atakaye leta shobo wa kwanza, na iyo ishu ya wanajeshi nayoifahamu mm ilikua beach ndiyo aliwapiga akidai majamaa wanajisikia mtaani akasepa na gwanda zao akazitupa junction ya tiper uko.. Jamaa ni mkimya anasmile muda wote kukuita bro ndo kawaida yake hata kama amekuzidi umri, mtu wa totoz sana kwakua ni bishoo kuhusu ukorofi mara nyingi anao uyu lugu kumpiga mtu yyte kwake n kitu poa sana mda wowote..
Kuhusu kutumia dawa hii ina % kubwa ni kweli kwasababu jamaa mkikaa nae story mbili tatu akiaga haipiti dakika 5 defender hii apa, ila si kweli kwamba akipigwa hasikii hua wanapishana sana kauli na lugu(mafaali wawili) hata kama anampigaga ila unaona na yy jinsi shida anayopata.
Kuna siku alikuja kwenye p.table akapita dem mzuri kinoma mbokoo akawa anajificha flani ivi, baada ya dem kupita akatoa story kwamba, alivamia nyumba flani karibu na fray luis(bondeni) kwa kishua flani ivi ndo amechukua ela anataka kusepa akakutana na uyo dem..dem akamwambia mbokoo ebu tucheze kidg afu ndo usepe kidgo utolee jasho ulichoiba,, asee kumbe dem yupo fiti ile mbaya ikambidi akimbie tuu..ukimuona tr wake mbokoo huwezi amini mkimya mpole sikuizi hataki kufundisha tena weng wanakua wezi..
Mbokoo ilikua ukimwambia bro sina kitu kama ni muhimu lazima akusaidie, ila lugu ni mkorofi sana ata kama anakufahamu anaweza kukukaba.. Jamaa anapenda wanawake sana na adi anakamatwa zanzibar ilikua yupo na madem bar,,pia maaskari walizidi kumchukia alivyompiga mwenzao vibaya mnoo adi walimuuliza umepata ajali gani kumbe ni mbokoo
Kigamboni tunamfahamu kama DUDE.
Nakumbuka kuna siku npo na mama tukapishana nae alivyomsalimia mama kwa ustaarabu maza akasema vijana wachache wastaarabu kama hawa tulivyofika mbele nkamwambia ndo mbokoo(DUDE)
Story ya mbokoo na mwana wa keko siku nyingine__

Muandiko sio muhimu sana wakuu.
 
kwa waliokulia Kimara ya Dar enzi hizo Kuna jamaa aliitwa Omary Kundinga,..alisumbua Sana kipindi hicho miaka ya 90 Hadi 2000 mwanzoni

Kundinga sasa hivi anapiga debe mida ya jioni pale kimara upande wa gari za kwenda Mbezi siku hizi amekwisha kawa mpole kama teja tangu amefungwa ametoka mnyonge sana ingawa enzi zake alisumbua sana, alikua nakaa sana mnarani kwa akina Simbani
 
hahaha jamaa nakumbuka enzi hizo alikuwa anakuja na fuko lake la Nazi za wizi anawataiti walimu wote ofisini wanunue Sasa ole wako usinunue,alikuwa pia anatusave Sana wachelewaji tukiwa tunapewa adhabu alikuwa akija anaruhusu wote tusepe na mwalimu anapewa on your aache ukuda wa kutukamata

Mkuu utakua umesoma shule ya msingi Mavurunza
 
Back
Top Bottom