Mjue Jini Mahaba: Fahamu mengi kuhusu jini mahaba

Mkuu rakims hivi viumbe ni imaginary tuu au ndio hawa 2naosimuliwa na wanasayansi aliens, dunia yao hawa viumbe ni hapahapa duniani au 2kiwaita ndio wanatoka huko kwnye sayari yao kuja duniani! Je hawa ndio wazungu wanawa2mia kufanikisha technology zao na mambo yao mengi
Mkuu hivi viumbe ni majini wao huishi dunia hii hii tuliopo isipokuwa wao hawaonekani na ukitaka kuwaona kuna njia za kuwatazama pia baadhi ya wazungu huwatumia hawa katika sayansi ya maendeleo lakini wengine pia huwatumia katika sayansi za uchawi wana maarifa kulingana na vile walivyokadiriwa na pia hawa sio aliens wao hao ni viumbe tofauti na hawa mkuu.

Rakims
 
hapo kwenye sababu za kumkumba mtu, namba 4 sijaielewa embu nifafanulie kidgo
Mtu anapoingia chooni na kuanza kujichua(punyeto) kama vile vijana wadogo wanapokuwa wanafanya hivyo au wale wenye kufanya mapenzi chooni ndio waathiriwa wakubwa wa viumbe hivi navyo hukaa nao muda mrefu sana.
Chooni tu peke yake kuna mashetani wengi sana ambao idadi yake haijulikani kinachojulikana wamo wa kike na wa kiume kuna utajo ukitaka kuwaona mabinti warembo sita humo unaweza kuwaona unaanza na "maridan maridan, baridan baridan........* na kuendelea hutokea mabinti warembo sita ambao ni mashetani nao wanaweza kumpa mtu anachotaka alama ya ujio wao ni choo kupanuka wewe ukiwa huo na ukimaliza mkataba nao panajifunga (USIJIFUNZE)

Upo utajo mwingine unaanza na Sor.........* hii utasikia jitu la miramba minne linahema kwenye kuta unaweza kuliambia likampige stoke yoyote atakae ingine choo chochote duniani na linaenda kufanya hivyo na inaaminika shetani hili ndio huwapa watu stroke wakiwa chooni, mbali na hapo mkuu yapo mashetani aina nyingi chooni ambayo hufanya kazi ya kudhuru watu

Nimekwambia haya ili kujibu swali lako kama bado sijajibu ulivyotaka uliza tena

Rakims
 
Mwisho wake ni mbaya tu maana sharti ulilokubaliana ndio hill utalivunja siku unajua kwanini! nimada pana siku nitawapa
Cha kuelewa ni kuwa katika viumbe ambao hawawezi kuishi kwa masharti wa kwanza ni binadamu hata umudu sharti kwa muda wa miaka kumi ipo siku utateleza tu hivyo ni mambo ya kujitenga nayo mbali

Rakims
 
Mkuu hivi viumbe ni majini wao huishi dunia hii hii tuliopo isipokuwa wao hawaonekani na ukitaka kuwaona kuna njia za kuwatazama pia baadhi ya wazungu huwatumia hawa katika sayansi ya maendeleo lakini wengine pia huwatumia katika sayansi za uchawi wana maarifa kulingana na vile walivyokadiriwa na pia hawa sio aliens wao hao ni viumbe tofauti na hawa mkuu.

Rakims


Wewe utaingia Jehanamu kwa Uongo, take care.
 
Uzi ulikua mtam sema zimeibuka kambi. Vinginevyo, endeleeni kutuelimisha. Mkuu Rakims na wengine mnaojua, vipi matumizi ya mnyama nguruwe katika kufukuza majini?
 
Uzi ulikua mtam sema zimeibuka kambi. Vinginevyo, endeleeni kutuelimisha. Mkuu Rakims na wengine mnaojua, vipi matumizi ya mnyama nguruwe katika kufukuza majini?
Hana uhusiano chochote na kufukuza jini isipokua ni imani tu iliyowekwa na baadhi ya mapepo kwa kujitambulisha kuwa yameshika dini ya kiislamu mkuu

Rakims
 
Mtu anapoingia chooni na kuanza kujichua(punyeto) kama vile vijana wadogo wanapokuwa wanafanya hivyo au wale wenye kufanya mapenzi chooni ndio waathiriwa wakubwa wa viumbe hivi navyo hukaa nao muda mrefu sana.
Chooni tu peke yake kuna mashetani wengi sana ambao idadi yake haijulikani kinachojulikana wamo wa kike na wa kiume kuna utajo ukitaka kuwaona mabinti warembo sita humo unaweza kuwaona unaanza na "maridan maridan, baridan baridan........* na kuendelea hutokea mabinti warembo sita ambao ni mashetani nao wanaweza kumpa mtu anachotaka alama ya ujio wao ni choo kupanuka wewe ukiwa huo na ukimaliza mkataba nao panajifunga (USIJIFUNZE)

Upo utajo mwingine unaanza na Sor.........* hii utasikia jitu la miramba minne linahema kwenye kuta unaweza kuliambia likampige stoke yoyote atakae ingine choo chochote duniani na linaenda kufanya hivyo na inaaminika shetani hili ndio huwapa watu stroke wakiwa chooni, mbali na hapo mkuu yapo mashetani aina nyingi chooni ambayo hufanya kazi ya kudhuru watu

Nimekwambia haya ili kujibu swali lako kama bado sijajibu ulivyotaka uliza tena

Rakims
Asante mkuu! Lakini vipi kwa wale ambao labda hujichulia ndani Kisha akaenda kuoga chooni napo pia yanakukumba ??
 
Me mwanamke wangu ananilalamikia kua anaish na jini na humtokea mara kwa mara na kufanya nae mapenz kilazima ila me siamini hk kitu
 
Habari wakuu!

Wengi miongoni mwenu huona kila ninapotoa thread huona kama vile hufundisha uchawi lakini kwa mwenye akili timamu hupata mafundisho kwa asilimia kubwa sana.

Kumekuwa na tungo nyingi sana kuhusu jini mahaba na maelezo mengi sana kuhusu jini huyu, lakini pia watu wengi sana wanaropoka tu bila kumjua, lau kama wangemfahamu basi wangezidi kumuomba Mwenyezi Mungu awaepushe na mtihani wa kiumbe hiki.

MJUE JINI MAHABA:
View attachment 1183758
Jini mahaba ni moja kati ya majini waliokuwa na nguvu sana na waliopo karibu sana na ufalme wa Dajjal/Shetani/Ibilisi/Lucifer/ ambaye pia wengine humuita mpinga Kristo.

Elewa ya kuwa ndugu yangu unaesoma makala hii kwamba kuna daraja tano tu za majini katika ulimwengu huu tunaoishi miongoni mwa ukubwa wa tabaka la majini ambayo yanasadikika kuwa milioni 72 elfu, hii ni idadi iliyopigwa na baadhi tu ya mashetani wenyewe lakini tukizungumzia kiasiri ya majini hawa wapo katika makundi matano peke yake.

Watu wamekuwa wakidanganywa sana kwa hadithi na baadhi ya tungo za viumbe hawa lakini unachotakiwa kuelewa ni kwamba idadi ya viumbe hawa kwa wingi wao anayejua ni Mwenyezi Mungu peke yake na hakuna mwingine.

Elewa pia ya kwamba majini hawa mtu akikwambia masubiani, masharifu, mashetani, mizimu, vibushuti, vinyamkela, mapepo, makudam, muwakili, ruhani, jini mahaba, makata, shetani, subisubi na yote yale majina mengine unayoyajua, hayo yote yapo kwenye kundi moja tu MAJINI. Hayana tofauti isipokuwa tu kwa mageuzi ya maumbile yao au uhasama wao yanayofanya au misaada yanayotoa ndiyo hupewa majina tofauti tofauti kulingana na kile yalichomfanyia au yanavyoonekana.

Sasa nikija kujaaliwa basi nitawaelezea majini ili kila atakayekuwa anatamka jini aelewe anachosema na siyo kutamka tu.

Turejee kwenye kumjua huyu tuliyemkusudia.

Maana ya Jini mahaba:
View attachment 1183766
Asili ya jina hili ni jina lililotungwa tu na sisi wenyewe Watanzania ili kuweza kutambulisha ni kiumbe cha namna gani tunachokuwa tumekusudia, lakini kwa maelezo unatakiwa ufahamu kuwa jini huyu kazi yake na katika mambo ambayo anayafanya zaidi ni kuhakikisha zinaa inatawala na kazi zote zinazohusiana na ngono.

Baadhi ya kazi zake:

View attachment 1183767
Jini huyu hutumika kutumia watu ndoto za ngono, hutumika kuwalawiti wanaume kwa wanawake kama popo bawa, hutumika pia kuwafanya au kuwashawishi wale alionao kuingilia au kuingiliwa kinyume na maumbile, kuwaingilia watu na kuwafanyia michezo ya kinyume na maumbile. Hutumika pia kuua kwa kubaka. Shetani huyu hutumika vile vile katika kuleta ufukara, hutumika pia katika kuwafanya wazee na watu wazima kuzini na watoto wadogo na huwafanya watu wawe na ashiki kupindukia, lakini pia kubwa katika mambo anayoyafanya ni kuwaondolea wahanga hisia za kimapenzi na kumfanya mwanaume asiweze kusimamia uume barabara unakuwa umelegea na pia kuwaondoshea wanawake ladha ya mapenzi na wengine huwafanya kukosa kabisa hamu ya mapenzi na kuwapa mvuto kwenye jinsia inayofanana nao.

Baadhi ya watu humuita popobawa kulingana na yale aliyoyafanya na wengine humuita jini mahaba kulingana na alichofanya. Wengine humuita majina wanayoyajua wao lakini Wazungu hawa huwaita Succubi au Succubus, yaani hiyo mmoja anakuwa ni dume na mwingine ni jike.

Yote kwa yote, elewa ewe ndugu yangu kuwa viumbe hawa hawana wema kwa mtu zaidi ya kuweka naye mikataba ya uhakika kwamba atashindwa na kuweza kukosea masharti kisha lile analohitaji yeye kuanza kulifanya kwa muhusika.

WALIOATHIRIWA:

View attachment 1183764
Mara nyingi walioathiriwa na kiumbe huyu huwa wanakuwa wasiri sana kwa kuhofia fedheha kwenye jamii na pia wengi kati ya wao fedheha ikizidi huanza kutumbukia katika ulevi uliopindukia au kuvuta bangi na vinginevyo ili tu kuweza kuficha aibu aliyo nayo.

UTAJIJUA VIPI KAMA KAKUKUMBA:
Watu wengi mara ya kwanza anapowakumba huwafanya au kuwaingilia au kushiriki nao kinyume na maumbile na pia huwafanya wahanga kuwa ni wenye kujificha sana na aibu hii hata kutafuta msaada kwa maana humtia aibu katika sura yake kuzungumzia jambo hili na kumjaza upepo wa mawazo kuwa yeye akisema au akitaka msaada ataonekana vipi, hivyo anakuwa anacheza na akili ya muhusika,

Wengi huota wakifanya mapenzi na mama zao au baba zao hata kaka au dada au mtu yeyote unaemuheshimu kama shangazi na wengineo.

Muhanga mwingine hujikuta akipitiwa tu na usingizi basi huota mwanamke anakuja na kuanza kumlazimisha au mwanaume wafanye nae mapenzi kinyume baada ya hapo muhusika huishiwa nguvu na kukubali kufanya au kufanyiwa, wengine huona kabisa kama kivuli live kikilazimisha kumuingilia hasa pale ambapo hatasema na kuhangaika kutafuta msaada wa hili, basi kiumbe yule huanza kumfanyia hayo na kumshurutisha mambo mengine yaliyokuwa machafu na kumuadhiri mbele za watu na kumfanya ajihisi kudharaulika na kuchukiwa bila sababu na humfanya kuwa ni mtu mwenye hasira za hovyo au mtu wa kulipuka hovyo, jazba zinakuwa karibu naye kwa muda mwingi.

Muhanga mwingine huyu humkumba na kumuotesha ndoto kuwa anawekewa vidole na watu sehemu hizo za siri na kumkusanyia kundi la watu ndotoni wakionyesha kumcheka na kumdharau.

Muhanga mwingine huyu humkumba na kumfanya live hata watu wakawa wanaona kinachoendelea bila kumuona anayefanya na kuanza kuingiwa na hofu kubwa. Hapa wengine hufungiwa ndani kwa kuficha fedheha nje kwa watu na asijulikane kinachofanyika ndani.

Zipo aina nyingi sana za huyu shetani zilizo mbaya na za aibu kabisa. Wengine pia huzijua waliokwisha kukutana na wahanga au wahanga wenyewe. Hizi nimeweka chache tu, zingine ni kama kutekenywa sehemu za siri na kushikwa sehemu za maziwa bila kumuona anaefanya hivyo na wengine kuingiziwa vidole bila kuona anayefanya hivyo live.

Haya ikiwa hayajakukuta au hujaona basi usidharau na kupuuza kwa maana siku kinakutokea usione kitu kipya au usikutwe ukiwa hujui.

TIBA YAKE:
Katika maradhi ambayo huwashinda matabibu wengi ni haya ya mashetani hawa wa mahaba kwa maana hutakiwa tabia yule kufanya mawili kati ya haya:

1: Kufunga yule jini na kwenda kumtupa mbali (au kama kafanya mtu, kumpa mwenyewe mzigo wake)
2: Kumuua yule shetani kwa maana si rahisi kumtoa kwa makubaliano aondoke. Ukitaka kukubaliana naye ili aondoke utatakiwa kufanya atakayoamuru; anaweza kukwambia ushiriki jambo lolote la kishetani ili amuondokee (hadi kuweza kuzungumza naye imeshapita kazi kubwa)

Kundi la pili la kumsadia muhanga huyu:

Utatakiwa kumpeleka katika Misikiti au Makanisani na upate mtu ambaye ana hofu ya Mwenyezi Mungu au mwenye imani thabiti ya kiroho ndiyo anaweza kumsaidia huyo mtu kwa maombi, vinginevyo sehemu zingine basi huwa ni anatoka na kurudi au kumvaa yule anayemtibu na kuanza kumshughulikia yeye. Inatakiwa busara kubwa sana katika kumuuguza mtu wa hivi vinginevyo yanatoka kwake yanakukuta wewe.

SABABU ZA KUMKUMBA MTU:
Zipo sababu nyingi za haya madudu kumkumba mtu hapa nitataja chache tu kwanza:

1: Kukaa na shahawa muda mrefu
2: Kuchezea baharini nyakati za magharibi
3: Kuingia mkataba kwa ajili ya kupata mali
4: Kujichua au kujisaga maeneo ya chooni au maliwato maarufu kama PUNYETO, (siyo BAFUNI)
5: Kulala uchi huku mwili ukiwa na mafuta peke yako
6: Kulala peke yako ukiwa nusu uchi huku umeweka marashi au air freshener bila kusali
7: Kulala huku kioo kikikuangalia upo uchi
8: Kufanya ngono kinyume
9: Kuchungulia watu wakifanya mapenzi
10: Kukojoa au kumwaga shahawa baharini/kisimani/mtoni/ndani ya mbuyu
11: Kutupiwa jini huyu anakuwa katika mfumo wa popo bawa

View attachment 1183770

MAELEZO:
Hapo katika sababu nilizoainisha za kutolea maelezo ni mbili tu, zingine zinaeleweka na makala za watu wengine zilishazieleza.

1: Kukaa na Shahawa muda mrefu

Elewa ya kuwa viumbe hawa hupenda sana harufu ya shahawa na wanapoiskia wao huona raha ni kana kwamba ni kilevi hivi chenye kuwapa tulizo la akili zao.
Vilevile, kwa watu ambao hukutwa na ndoto nyevu kisha asiamke, basi wao hukimbilia kufyonza hizo mbegu mapema pindi zinapokuwa zimetoka kuwahi uhai ule wa mbegu. Ndiyo maana baadhi ya watu wengi huota wameshusha mbegu nyingi lakini akitizama kwenye shuka vinakuwa kama matone tu.

2: Kuingia mkataba kwa ajili ya kupata mali

Hapa mara nyingi mtu huyu huenda kutafuta jini ambaye atakuwa naye kimapenzi na ampe mali. Sasa huko anakuwa kapewa masharti matatu: asinywe pombe, asivute sigara na asiwe na mwanamke tofauti na yeye huyo jini, au mwanaume tofauti na yeye, kwa muda atakaokuwa kautaka yeye.

Hapo utaambiwa usubiri usiku wa Jumamosi saa sita usiku, ikifika hiyo saa utatakiwa mazingira ya ndani kwako yawe safi na pia uchome udi saba kikiwa chumba kipo tupu kisha zikiisha udi hizo aingize kitanda ambacho atakuwa kakiandaa kiwe cha chuma kipakaliwe rangi nyeupe na nyeusi na kwa siri sana anachora picha ya nyoka aliyetoa ulimi nje, kisha baada ya hapo aweke shuka, godoro atandike shuka nyeupe na pazia ziwe nyeupe na awe anagamba la nyoka kisha alichome moto abaki alivyozaliwa na mwili wake aupake mafuta yang'ae kisha ashikilie udi baada ya kuchoma gamba la nyoka kisha aseme maneno haya mara 7 (*******************************************)

Baada ya hapo utasema jinsia kwa sauti ya hisssssssssssss kama vile nyoka anasema akiwa kainama atakapoinua tu kichwa chake kuangalia kwenye mlango wa chumba hicho anachofanyia ujinga wake huu, atakutanisha macho yake na binti mrembo ambaye urembo wake kwa yeye muhanga ataona duniani hajawahi kutokea na vigezo vyote anavyotaka kuviona kwa binti mrembo au kijana mrembo ataviona kwa kiumbe huyo. Atazungumza naye kisha atamwambia kila anachotaka na hatachelewa kwa muda anaotaka atakuwa kampatia. Baada ya makubaliano atafanya naye ngono na kisha atamuachia kama ni pete au cheni ambayo atakaa nayo na atakuwa kakubali kuolewa na kiumbe huyo, basi akimtaka popote, saa yoyote atatakiwa asugue pete hiyo kwenye meno au kubusu na shetani huyo atatokea hapo hapo hata kama yeye atakuwa magharibi na jini huyo awe mashariki.

Na ukimuona mtu anafanya haya muonyeshe thread hii ajue anathubutu kudiriki na kitu gani. Baada ya hapo watu wengi hawaoni starehe zaidi ya hizi 3 sasa mwanzo wengi hujaribu na kuona ni rahisi vile kiumbe hicho hata ukiambie kikae umbile la nani kitajibadili na hata ukiambie kiigize sauti yake hakitakosea na kitakupenda sana ila sasa ukosee kikutie adabu (utamaliza waganga na waganguzi/maadamu ni maagano ulifanya mwenyewe hiyo ni zima yako) na ukitaka kukiondoa kinaondoka na vyote kilichokupa.

Wengine vikiwazoea huanza kuwaambia toka tu nje ya mapenzi hamna shida, sasa mtu anavurugika taratibu anahisi anaishi na binadamu akiona anafoka hakajibu kanalia akifanya visa kanavumilia, siku umefanya jambo nje ya makubaliano utaona cha mtemakuni.

View attachment 1183769

Nikijaaliwa taongezea nyama kwenye thread hii kwa maana kuna mengi ya kufahamu.

KUMBUKA:
Kila unapokaa muombe Mwenyezi Mungu akukinge na viumbe hivi maana vikikukumba kutoka huwa ni vigumu sana hadi upate mwenye maarifa navyo

Ikiwa una swali na upo nje ya forums:

tumia email hii rakimsspiritual@gmail.com
au namba ya mtu aliye karibu nami:

0626085437
Rakims
Mimi nauliza hizi picha ulizozitumia ni real au ni CGI imagination?
 
Back
Top Bottom