Tatizo la jini mahaba

housekeeper

Member
Apr 21, 2020
31
104
habari wana jukwaa,

Natumai sote ni wazima wa afya njema, na poleni kwa wenye changamoto za aina mbali mbali.

Mimi ni kijana mwenye takribani miaka 32 kwa sasa.
Nina changamoto ya vitu ndani ya mwili wangu ambavyo nahisi inawezekana kuwa ni jini mahaba.

Baadhi ya changamoto nilizo nazo kwenye mwili wangu ni kama ifuatavyo.
1. Kuwashwa mwili hasa kwenye sehemu za siri.

2. Vitu kunitembea mwili kama sisimizi au wadudu wadogo ingawa ukipukuta hukuti chochote.

3. Kuota nimelala na mwanamke pembeni yangu hii inatokea hata mchana nikiwa nimelala.

4. Kuhisi nafanya mapenzi usingizini hadi kufikia mahali nafikia mshindo.

5. Ninapofanya mapenzi na mwanamke ni lazima mwanamke huyo aumwe tumbo au kuumwa baada ya siku kadhaa mbele (baada ya tendo).

Hizo ni Baadhi ya dalili na changamoto nilizo nazo ndani ya mwili wangu.
Nilifanikiwa kupata mtoto miaka ya nyuma ila mtoto ana changamoto ya kuumwa mara kwa mara hadi sasa ana miaka 10.

(Huumwa zaidi mapunye yasiyoisha, homa na UTI)

CHANZO: ilikua mwaka 2012 usiku wa manane, niliona nimelala na mtu pembeni ya kitanda na alikua na sura ya kike. (Ingawa sura sikuitambua.

Mwili ulianza kusisimuka kupita kiasi.

Nilihisi kitu kinatoka kichwani kama kinanivua ngozi (kama unachuna mbuzi halafu unaivua ngozi bila kutumia kisu) hadi sehemu za siri ndipo niliposhtuka na kuhisi kuna kitu kimetoka nikajiangalia sehemu za siri nikakuta Uume umesinyaa.

Toka hapo hadi leo nimekua nikiwashwa na kuhisi vitu kama vidudu au mchanga vinanitambaa ndani ya mwili.

NOTE: hadi sasa sijaoa ingawa nimepata huyo mtoto mmoja.

Kwa mwenye uelewa au mwenye msaada naomba msaada kwenye hili.

Hata kama kuna gharama nitajivuta ili niweze kujikomboa kwenye hii changamoto.

Asanteni na karibu kwa michango.
 
Bosi hakikisha unaoga vizuri, utakua huogi wewe, alafu ndoto, sababu zake huwa ni mawazo yako, na matendo yako ya kila siku, yaani wwe uwe unapenda matako, mara matamanio, usiote ndoto hizo.

Hamna mahaba sijui jini wala mkata kamba, oga vizuri, tafuta mwanamke ukae nae ndani.

Mtoto kuumwa pia inategemea na mazingira yake. Mtunze mwanao huyo.
 
Maombi ndio njia pekee...

Anza kwa Toba na rehema..

Soma Zaburi 51...

Omba kwa kumaanisha,

Sali hivi, Yesu ninajiosha kwa damu yako takatifu, ninaomba Toba na rehema kwa ajili ya zinaa niliyofanya unataja majina ya wanawake au wanaume, naomba unirehemu na kuniosha kwa damu na dhambi hii ya zinaa, ninavua vazi hili zinaa kwa damu ya YESU

Omba Kila siku mpaka utakapoona huoni hali hiyo Tena...
 
Hilo tatizo lako limekaa kiroho zaidi, kama dini yako ni muislam tafuta masheikh wakusomee kisomo, kama mkristo ni maombi yatakusaidia na kama ni mpagani inabidi utafute mganga mashuhuri.

Hakuna swali linalokosa jibu na vilevile hakuna tatizo linalokosa utatuzi.

Usikate tamaa, yote kwa yote amini Mungu atakusaidia.
 
Shukrani sana mkuu!
 
Maombi ndio njia pekee...

Anza kwa Toba na rehema..

Soma Zaburi 51...

Omba kwa kumaanisha,

Sali hivi, Yesu ninajiosha kwa damu yako takatifu, ninaomba Toba na rehema kwa ajili ya zinaa niliyofanya unataja majina ya wanawake au wanaume, naomba unirehemu na kuniosha kwa damu na dhambi hii ya zinaa, ninavua vazi hili zinaa kwa damu ya YESU

Omba Kila siku mpaka utakapoona huoni hali hiyo Tena...
Amen nimajaribu kwenye maombi ila huwa vinatulia na baadae kurudi (hali ya kuwashwa)
 
Kuna asubuhi na mchana ila umeona usiku huu ndio muda bora wa kuleta kisa chako cha usiku wa manane

Enwei, asante kwa kufanya usiku uwe mrefu
Mchana majukumu mengi mkuu!

Ndio nimepata mda wa kuperuzi wakati nacheki BBC hapa.

By the way mimi ndio natakiwa niwe muoga maana naishi mwenyewe na nyumba ni kubwa.

Au wew hata maneno yanakukosesha usingizi?
 
Back
Top Bottom