Usiombee, akawa ni demu sasa..
Kuna siku hiyo nafanya biashara ya eneo..
Mwanangu akapata mteja akamleta, jamaa akatizama eneo akalipenda, ikawa uchawi malipo tu, mengine kubadili hati ni juu yake atafanya mwenyewe.
Mara akasema ngoja kuna dada yake yupo njiani, anaishi karibu na maeneo ya hapo, ngoja aje kuona eneo, mie nikaona sawa, haina tabu.
Kufika yule demu, kauli zake mbili za kwnaza tu, nikamnong'oneza dalali, hapa biashara hakuna, akaniuliza kwanini, nikamfunya na kumpa biashara atulie.
Kweli yule dada akaanza kuropoka maeneo yale,sijui kimeenda kimerudi.. bei yetu juu kidogo, wakati bei niliyokuwa nauza ni takriban nusu ya bei yenyewe kwa dhiki zangu.
Ikabidi nimuulize unaishi maeneo haya kweli, akaanza kumung'unya maneno, ooh, sijui nilikuwa naishi hapa, nimehamia wapi sijui, lakini nafanya kazi ardhi.
Nikamgeukia jamaa, nikamwambia ukiwa tayari karibu, kama shida yangu, itakuwa haijaisha nitakuuzia kama imeisha basi bei yake sio hii tena.
Nikafunga safari...
Baada kama ya miezi mi3 jamaa anakuja anataka tufanye biashara, nikamtaji bei yake mpya, mara 2.5 ya ike, akashindwa bei. Tukamwagiana hapo.