Mjomba akauliza: Jamani Nyumba hii hapaliwi?

Mjomba akauliza: Jamani Nyumba hii hapaliwi?

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394
Juzi tumetembelewa na mjomba wetu kutoka huko Bara mkoani Tabora. Mama yetu ni mwarabu mwenye asili ya Tabora ila aliolewa huku Visiwani, na kule Tabora kuna ndugu zetu na mmojawapo ni huyu mjomba wetu ambaye ni Mnyamwezi pure.

Kwa huku kwetu visiwani ulaji wetu unajulikana lakini unatofautiana sana na wa huko bara. Ingawa kuna tofauti kati ya kaya na kaya, lakini tofauti hiyo siyo kubwa sana kuna vitu vidogo vidogo tu vinavyo tofautisha kati ya kaya moja na nyingine linapokuja suala la maakuli.

Kwa mfano nyumbani kwetu siye, asubuhi majira ya saa nne hivi twapata staftahi nzito yenye mihogo na samaki mmbichi aliyeungwa kwa nazi, wakati mwingine chapatti na egg chopp zaweza kuwepo na vitu vidogo vidogo shokishoki ili mradi kuwepo vionjo kadha wa kadha.

Kwa sababu staftahi ni nzito itatufikisha majira ya saa kumi hivi hapo tutapata chakula cha mchana baab kubwa, na kwa kawaida hakipikwi chakula cha aina moja, kunakuwa na aina mbili tatu hivi za vyakula ili kama mtu hujapenda chakula cha aina hii basi atakula chakula kingine kilichopo.

Ikifika usiku majira ya saa tatu au saa nne hivi, kwa kawaida tunaweza knywa chai na boflo na vitafunwa vingine kama kababu, chapatti au vijiandazi au wakati mwingine pizza ya Kizanzibari. Kwa wale wasiyoijua Pizza ya Kizanzibari wanaweza kuipata maeneo ya Ilala au Buguruni pale Sheli.

Naam turejee kwenye habari ya mgeni wetu. Sasa mjomba alifika juzi majira ya asubuhi, tukapata naye staftahi na ilipofika mchana majira ya saa kumi tukapata mlo wa mchana. Ilipofika usiku majiraya saa tatu hivi tukapata chai ya jioni na vitafunwa kadha wa kadha kama kawaida.


Tulipomaliza tukaendelea kuangalia zetu TV kabla ya kwenda kulala. Ilipofika saa tano usiku kila mtu kwa muda wake akawa anaondioka kwenda kulala, nikajikuta nimebaki na mjomba tukipiga stori akinisimulia habari za Tabora.

Kipindi nilichokuwa nakiangalia kilipokwisha ikanilazimu nimuage mjomba niende zangu kulala. Kwa kuwa alishaonyeshwa chumba chake cha kulala sikuwa wasiwasi nilimuachia remote ya TV ili akimaliza kuangalia azime TV kabla ya kwenda kulala.

Wakati naondoka mjomba akaniita.

‘Zinduna hebu njoo kwanza.'

Nikarudik umsikiliza maana nilishapiga hatua kadhaa kueleklea chumbani kwangu.


‘Hivi nyumba hii hapaliwi' aliniuliza mjomba.

‘Hapaliwi? Unamaanisha nini?' nilimuuliza.

Namaanisha chakula cha usiku hakuna? Alinijibu kwa kuniuliza swali.

‘Mjomba situmeshakula hapa!' nilimjibu nikiwa nimeshangaa.

‘Yaani hii chai na tuvijichapati tuwili tutatu ndiyo mnaita chakula! Acheni masikhara kabisa, miye bila ugali hapa sijalala'

Miye mh! Likanishuka, nikamwambia siye ndiyo ulaji wetu huku visiwani mambo ya kusindilia ugali usiku huku hakuna ni vyakula laini laini vya kusindikiza usingizi.

Basi mjomba alilalamika sana na akasema hatokaa atarudi zake kwao Tabora kwa sababu tunataka kumuua kwa njaa.

Hata hivyo nilikwenda kwenye friji nikamchukulia chapatti kadhaa na mchuzi na chai nikampashia moto na kumpakablaya kwenda kulala.Kesho yake alialamika sana kwa dada yake yaani mama kwamba hataweza kuishi pale nyumbani kwa sababu anaweza kufa na njaa.

Ni kweli leo ameondoka zake kwenda zake Bara, tumemsindikiza asubuhi wakati alipanga kukaa wiki mbili.


Kilichonishangaza mjomba mwenyewe ana mwili mdogo lakini anapeleka msosi na sijui unaendaga wapi. Siyo kwamba namsimangia chakula lakini nimejikuta tu nikijiuliza hivi mtu hawezi kubadilisha utaratibuwake wa maakuli anapokuwa ugenini japo kwa siku chache?

Hivi inawezekana vipi mtu asubuhi chai mchana ugali mkubwa na usiku pia unapeleka ugali si kujaza tu tumbo.

Ulaji huo wala siyo wa afya kabisa.

Nimeshangaa sanakwa kweli.

CC
watu8 Asprin, Ruttashobolwa, Ntuzu, Nyani Ngabu The Boss, Kiranga, Mentor, KakaKiiza, Dark City, Arabela, farkhina, Kaizer, charminglady, Elizabeth Dominic Paloma, Ennie, sister, DEMBA, Heaven on Earth
 
haa haa haa Zinduna sie huku bara tushazoea kuvimbisha tumbo na ugali au wali kabla ya kulala..btw kwa nini mmekubali mjomba aondoke kabla ya muda aliopanga...si mngekuwa mnampikia tu ugali wake wa kinyamwezi ule mgumu ale pekeake ili asuuzike na roho yake.
 
Last edited by a moderator:
Zinduna mwili haujengwi kwa tofali bana na kamwili kake hako kadogo kanabeba zege la uhakika na huku bara tumezoea ugali bana biashara ya kutulisha chapati sijui bajia na halua sisi hatuwezi bana
Hiyo mpe utafiti ataweza ila Ntuzu na Tized na mshana jr zao ni ugali tena dona ule usiku bana
Mr Rocky mie nimeshangaa, yaani hata usiku ugali! tena mjomba mwenyewe kasema hata asubuhi anapenda sana ugali au viazi vitamu na uji
 
Last edited by a moderator:
haa haa haa Zinduna sie huku bara tushazoea kuvimbisha tumbo na ugali au wali kabla ya kulala..btw kwa nini mmekubali mjomba aondoke kabla ya muda aliopanga...si mngekuwa mnampikia tu ugali wake wa kinyamwezi ule mgumu ale pekeake ili asuuzike na roho yake.

Kajilalamisha zake na dada yake alimwambia atakuwa anampikia lakini akasema hataki kutupa kazi anaondoka tu na wala hakuwa na kinyongo
 
DEMBA hata mimi naona hawakutaka mjomba akae muda mrefu maana walikuwa na chance ya kumpikia ugalli wake mgumu muda anaotaka yeye na wakati anaotaka kula
Naona !zinduna alimchoka mapema mjomba wake
 
Last edited by a moderator:
Mr Rocky mie nimeshangaa, yaani hata usiku ugali! tena mjomba mwenyewe kasema hata asubuhi anapenda sana ugali au viazi vitamu na uji

Zinduna ndo maisha ya bara huko mtoto asubuhi anaamka na kiporo cha ugali au mihogo na viazi saa moja kabla ya kwenda shule
Sasa mtu mzima kama mjombako kumpa chapati na viandazi vya watu wa pwani ni kama kumpigisha mswaki tuu
 
Last edited by a moderator:
DEMBA hata mimi naona hawakutaka mjomba akae muda mrefu maana walikuwa na chance ya kumpikia ugalli wake mgumu muda anaotaka yeye na wakati anaotaka kula
Naona !zinduna alimchoka mapema mjomba wake

Wala hatukumchoka sema tu aliona atatukwaza na maugali yake kila siku
 
Zinduna ndo maisha ya bara huko mtoto asubuhi anaamka na kiporo cha ugali au mihogo na viazi saa moja kabla ya kwenda shule
Sasa mtu mzima kama mjombako kumpa chapati na viandazi vya watu wa pwani ni kama kumpigisha mswaki tuu

Mwezangu huku siye wala hatulimi kama huko Bara, tutaweza wapi kujaza matumbo
 
Mr Rocky niambie ukija home sijui shemeji yako apike nini sisi huku ugali usiku hamna
 
Last edited by a moderator:
Hahaha Zinduna
Mumemfukuza kijanja mjomba jamani..
BTW umenikumbusha mbali tuliendaga huko bara kutembea ilikuwa tukae wiki mbili hivi weeee asubuh unashindiliwa viazi mchana kande za kusongwa ka ugali wanaita nini sijui huko, usiku liugali weee nani akae ??wiki moja nikalianzisha tukasepa ningetoka kitambi jeh ..ila watu wa bara wanajua kushindilia jamani khaa!!!
 
Last edited by a moderator:
ooooooooooh Zinduna acha kabisa!!!
Nyamwezi haswaaa zinakula balaa!!!

Mama yangu yalimkuta baada ya kumpikia shemejie kaugali laini alikomzoesha mumewe, na mboga saba, mumewe naye aula kwa uma na kisu!!! Huyo baba mdogo akalalamika saana kwamba amelala njaa! Baba si akamgombeza mama!!! Kesho yake mama alisonga ugali MGUMU, MKUBWA! Mpaka baba akapatwa aibu hakuthubutu kusema kitu tena! Mezani tukabaki tunaangaliana tu!
 
Last edited by a moderator:
Mwezangu huku siye wala hatulimi kama huko Bara, tutaweza wapi kujaza matumbo

Zinduna ndo ujue maisha ya watu wa bara huko
Kule kwao chakula tele na kinapatikana mwaka mzima na chakula kikuu ni ugali na wali
Sasa hivyo vimandazi na halua kwake anaona kama mmemfananisha na mtoto mdogo
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom