Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

Gambamala

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2014
Posts
1,045
Reaction score
766
Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.

Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo. Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii, mnawezaje kubadili fikra zetu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court? yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani. Akauliza, then which criteria do you use support him?, yaani mnatumia kigezo gani kumuunga Lowasa mkono? nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.

Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may take you so many years to change. Yaani ninyi ni nchi ya ajabu, kwa style hii itawachukua miaka mingi kupata mabadiliko.
 
Doesn't matter nani kaongea, ila ukweli ni kwamba sisi watz tu wasahaulifu sana. Mimi mwenyewe huwa najiuliza sana hayo maswali ila naamua ku-give time. Ukitokea ufisadi watu huzungumza sana ila it take a week watu kusahau kila kitu. Kifupi tz tunaishi kwa matukio. Mungu atusaidie
 
unaona sasa?
watanzania tunashida sana.
Kimsingi wewe mleta mada hujui unachokitaka na wala hujui unaish ili iwe nini?
ivi mtu kujisemea tu tayari ni credibility ......................
 
Mimi nimewasilisha tu, kama unadhani hafai mbona kila kukicha viongozi wanakwenda kuomba misaada kwao?

huyo mzungu muulize kama walishafidia tanganyika kwa wizi,ukatili,ubakaji,ujangili waliotufanyia,bado unaabudu wazungu?? hopeless
 
Saint Ivuga

Mimi nakijua kiingereza vizuri, nina elimu ya chuo kikuu, na yeye anafahamu kiingereza, nimekutana nae si kwa kubahatisha, tunafahamiana.
Obama alipelekwa Ubungo bila kujitambua, haijui Richmond, yeye kapelekwa na mafisadi wa Tanzania kama njia ya kuua soo.

Hayo mambo ya kusema Lowasa hakuusika ni wewe unasema, Mhusika hajawahi kusema, labda wewe ndie msemaji wake
 
Last edited by a moderator:
Hafai bila sababu za msingi? unataka wote tukuamini kkama tulivyo aminishwa fitna za Mwakyembe na Sitta? ... Mwaga data za Uhakika... Jana Ulimsikiliza Kingunge na Kumuelewa? ...
Usimtetee Lowassa. HAFAI
 
huyo mzungu muulize kama walishafidia tanganyika kwa wizi,ukatili,ubakaji,ujangili waliotufanyia,bado unaabudu wazungu?? hopeless

Mimi nimeelezea mawazo yake, au hivyo ndio kumuabudu?, au ulitaka nikae kimya?
 
Mleta mada labda utuambie waTanzania wangapi ambao wanampenda Lowasa ukageneralise kwamba waTanzania wanampenda. Mikutano yake inakuwa na watu wangapi? Na je kila anayehudhuria mkutano huo anampenda? Je waTanzania wapo wangapi? Ungetumia busara kujali na hisia za watu wengine pia ambao si washabiki wa CCM, wala Lowasa mwenyewe je hawa unawaweka kwenye kundi gani? Eti kwamba unawashangaa waTanzania, sample yako ni ipi hapo ya kuchukulia waTanzania wote wamekufa na kuoza kwa Lowasa? Au kigezo kipi umekitumia hadi kuja na majumuisho kuwa waTanzania wanamtaka Lowasa awe rais? Nasubiri majibu
 
Aibu, Aibu, Aibu

Jaman mnaompigia debe Lowasa ...oneni Aibu.

Pamoja na ushahidi wa kamati ya mwakyemba, kutoswa uwaziri mkuu-Richmond

Pamoja na kuhonga hadharani makanisani na misikitin

Pamoja na kuhonga mashulen na vyuoni..
nk nk nk

Yooote anayafanya hadharani bila kificho, huyu ni adui wa haki, rafiki wa rushwa na ufisadi.

BADO KUNAWANAOMPIGIA DEBE NAKUMUHITAJII??? au ni njaaaa tuuu.
 
Lowasa kwa nini jana hajaongelea kuhusu richmond?
 
Back
Top Bottom