Mjengwa Blog na Ujambazi Wa Kifikra, JF Imekushinda?

Jun 9, 2011
92
53
09.jpg

Kwenu Jf,

Watanzania wengi hususani vijana wanahitaji mabadiliko, ni matumaini ya watanzania walio wengi kuwa nchi yetu imeiva kwa mageuzi, na pasipo ubishi wowote waandishi wa habari kama alivyo Mwanakijiji walitegemewa wawe msaada mkubwa katika hili(RESPECT Mwanakijiji), lakini hali ni tofauti kwa kaka yangu wa siku nyingi Maggid Mjengwa, ambaye tangu kuanzisha Blog yake mwaka 2006 amekuwa akipinga mabadiliko kupitia ujambazi wake wa kifikra anaoufanya kupitia maandiko yake ana hoja dhaifu sana halafu zipo ki-ccm lakini thankx to JF members mmemnyoosha kiasi kwamba siku hizi kapunguza "mbofumbofu" zake hapa Home Of Great Thinkers, mpaka huwa najiuliza hivi Mjengwa Jf imekushinda?..................hebu oneni baadhi ya maandiko yake yenye mchoko wa mantiki na mkatiko wa kifikra..."Ndugu zangu,
Katika nchi, uwepo wa uhuru wa kujieleza ni jambo muhimu sana. Maana, nchi haijengwi kwa dhahabu au almasi bali fikra za watu. Na katika nchi, uwepo wa fikra tofauti ni jambo jema kabisa.

Na kwangu mimi, Mzee Mwinyi namwona kuwa ni mmoja wa WaTanzania ambao ametoa mchango mkubwa katika kujenga utamaduni wa kuvumilia fikra tofauti na hata zenye kushutumu. Na mpaka sasa, akiwa amebaki na miaka minne madarakani, Jakaya Kikwete namwona kuwa ni kiongozi anayeonyesha uvumilivu mkubwa wa fikra zenye kushutumu , hivyo basi, kuchangia katika kuimarisha misingi ya uwepo wa fikra huru, hivyo basi, demokrasia. Na kimsingi haya ya ufisadi yaliimarika zaidi enzi za Mkapa. Enzi za Mkapa hayakuwekwa wazi, lakini wakati huu wa Kikwete ameonyesha kuruhusu kuanikwa hadharani.

Ndugu zangu,
Tuliokuwepo tunakumbuka, kuwa pamoja na mema ya Mwalimu, lakini, enzi za Nyerere hakukuwa na uhuru wa fikra. Na si kweli kuwa enzi za Ben Mkapa zilikuwa za Ukweli na Uwazi. Hicho kilikuwa ni kibwagizo tu cha kwenye mikutano na hotuba za Mheshimiwa.

Na namkumbuka Mkapa kwa kauli yake hii; Tanzania hakuna waandishi wa habari. Akamsifu sana mwandishi Riz Khan akisahau kuwa naye ' Mkapa', alikuwa mwandishi wa habari na waziri wa habari katika Tanzania. Na Mkapa aliposema Tanzania hakuna waandishi wa habari labda alikuwa na maana, kuwa mwandishi wa habari aliyebaki alikuwa ni yeye tu!

Kauli ile ya Mkapa kwa wanahabari inanikumbusha miaka ile ya 80. Kwenye moja ya hitimisho la mifungo ya Ramadhan, Sheikh Yahya akatamka; " Ramadhan hii WaTanzania waliofunga ni wawili tu". Baada ya kusikia hayo ya Sheikh Yahya, basi, kilichonijia kichwani ni hiki; yumkini wawili hao waliofunga ni Sheikh mwenyewe na mkewe!

Na ruksa kwa wenye kutaka kunishambulia kwa haya niliyoyaandika.

Maggid,
Njiani kwenda Iringa."
 
Umekuja kuipa promo hiyo blog hapa jf huna lolote
mimi sikuwa na jua kama majid anablog yake na sidhani kama naitaji kuifungua
 
Ana Blog? Oh well hakuna haja ya kwenda huko anyway.......

utaendaje wakati ubongo wako hauhitaji challenge!!! kila siku unapenda kuona na kusikia mambo yanayoendana na mawazo yako mgando,
kwa mtu kama we ni rahisi hata kuvitabiri vituo vya TV unavyoangalia na magazeti unayosoma... mwisho wa siku unakuwa hijui kweli na unabaki kuwa mtumwa wa fikra milele. UTAKUWA brainwashed sana we mtoto
 
Sio Maggid peke yake wako wengi wenye misimamo kama yake; ndivyo dunia yetu ilivyoumbwa, hatuwezi kufanana wote. Wewe pigania misimamo yako huku ukiwashawishi na wengine wengi kukuunga mkono. Mkiwa wengi zaidi ya wapinzani ndo maana yake umeshinda. Lakini tofauti hazitakwisha. Halafu unafuata nini ktk blog ya Maggid wakati mawazo yake huwa ni tata? Leo anapinga hiki, kesho anakisapoti. Tafuta vitu vipya!
 
09.jpg

Kwenu Jf,

Watanzania wengi hususani vijana wanahitaji mabadiliko, ni matumaini ya watanzania walio wengi kuwa nchi yetu imeiva kwa mageuzi, na pasipo ubishi wowote waandishi wa habari kama alivyo Mwanakijiji walitegemewa wawe msaada mkubwa katika hili(RESPECT Mwanakijiji), lakini hali ni tofauti kwa kaka yangu wa siku nyingi Maggid Mjengwa, ambaye tangu kuanzisha Blog yake mwaka 2006 amekuwa akipinga mabadiliko kupitia ujambazi wake wa kifikra anaoufanya kupitia maandiko yake ana hoja dhaifu sana halafu zipo ki-ccm lakini thankx to JF members mmemnyoosha kiasi kwamba siku hizi kapunguza "mbofumbofu" zake hapa Home Of Great Thinkers, mpaka huwa najiuliza hivi Mjengwa Jf imekushinda?..................hebu oneni baadhi ya maandiko yake yenye mchoko wa mantiki na mkatiko wa kifikra..."Ndugu zangu,
Katika nchi, uwepo wa uhuru wa kujieleza ni jambo muhimu sana. Maana, nchi haijengwi kwa dhahabu au almasi bali fikra za watu. Na katika nchi, uwepo wa fikra tofauti ni jambo jema kabisa.

Na kwangu mimi, Mzee Mwinyi namwona kuwa ni mmoja wa WaTanzania ambao ametoa mchango mkubwa katika kujenga utamaduni wa kuvumilia fikra tofauti na hata zenye kushutumu. Na mpaka sasa, akiwa amebaki na miaka minne madarakani, Jakaya Kikwete namwona kuwa ni kiongozi anayeonyesha uvumilivu mkubwa wa fikra zenye kushutumu , hivyo basi, kuchangia katika kuimarisha misingi ya uwepo wa fikra huru, hivyo basi, demokrasia. Na kimsingi haya ya ufisadi yaliimarika zaidi enzi za Mkapa. Enzi za Mkapa hayakuwekwa wazi, lakini wakati huu wa Kikwete ameonyesha kuruhusu kuanikwa hadharani.

Ndugu zangu,
Tuliokuwepo tunakumbuka, kuwa pamoja na mema ya Mwalimu, lakini, enzi za Nyerere hakukuwa na uhuru wa fikra. Na si kweli kuwa enzi za Ben Mkapa zilikuwa za Ukweli na Uwazi. Hicho kilikuwa ni kibwagizo tu cha kwenye mikutano na hotuba za Mheshimiwa.

Na namkumbuka Mkapa kwa kauli yake hii; Tanzania hakuna waandishi wa habari. Akamsifu sana mwandishi Riz Khan akisahau kuwa naye ' Mkapa', alikuwa mwandishi wa habari na waziri wa habari katika Tanzania. Na Mkapa aliposema Tanzania hakuna waandishi wa habari labda alikuwa na maana, kuwa mwandishi wa habari aliyebaki alikuwa ni yeye tu!

Kauli ile ya Mkapa kwa wanahabari inanikumbusha miaka ile ya 80. Kwenye moja ya hitimisho la mifungo ya Ramadhan, Sheikh Yahya akatamka; " Ramadhan hii WaTanzania waliofunga ni wawili tu". Baada ya kusikia hayo ya Sheikh Yahya, basi, kilichonijia kichwani ni hiki; yumkini wawili hao waliofunga ni Sheikh mwenyewe na mkewe!

Na ruksa kwa wenye kutaka kunishambulia kwa haya niliyoyaandika.

Maggid,
Njiani kwenda Iringa."

mbona anacho ongea ni kweli kabisa hapa mimi ni mkristo napenda kusema viongozi wetu wote wajuu toka dini ya kislamu wameonyesha uvumilivu mkubwa tulivyo waponda kuliko sisi wakristo, ebu tazama magazeti yanaandika kwamba jk kahongwa suti wala hakuchimba mkwala wa kufa mtu ni saliva tu kapiga logologo mzee kapoa tu anajua nguvu aliyonayo jk, ok lowasa kaita watu hadi kwao kuchimba mkwala magazeti na bado hana uraisi je akipewa uraisi kubenea atatiwa kwenye acidi , mzee ulimwengu ataambiwa raia wa china, wana jf wataitwa raia wa nigeria
 
Maggid,

Amefilisika kimawazo, anatetea uhuru wa kuongea wakati uchumi wa nchi unaporomoka.
 
Napinga na wewe kidogo, hasa hapo uliposema ana fikra za ki-ccm. Hizo fikra zikoje?
 
Back
Top Bottom