Mjengwa asitisha mahusiano na Ludovick Joseph kwa tuhuma za 'kuhusika na matukio ya kigaidi'

Kwanza Mjengwa ni mnafiki na mlamba viatu vya wapanga magogoni. Hana lolote huyu zaidi ya kutumiwa kama puto.

Ni tatizo la waandishi wetu wa habari ambao wajiingiza kwenye profession bila kuisomea halafu baada ya kugundua kuwa kuna mshiko ndiyo wanakimbilia kutafuta vyeti!! Na TZ waandishi njaa ni wengi kuliko waandishi wa taaluma!!
 
TAARIFA RASMI KUTOKA Mtandao Wa Kijamii Wa MJENGWABLOG

Sunday, 17 March 2013 | Written by Mjengwa Blog

Ndugu zangu,
Kutokana na kuwepo kwa taarifa rasmi za kipolisi zenye kumtuhumu Ludovic Joseph kuhusika na matukio ya kigaidi.

Uongozi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog unasitisha rasmi, kuanzia leo Jumapili, Machi, 17,2013, kuwa na Ludovick Joseph kama msaidizi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Maggid Mjengwa,
Mmiliki wa Mjengwablog /Kwanzajamii

Huyu Maggid ana akili ndogo kweli!!

Kwa mfano tu, kama Ludovik angekuwa ni mke wake, kaka yake au mjomba wake angefanyeje?? Angeuwa undugu??
 
Filamu imefika patamu ila cha kushanganza ni wingi wa makanusho katika filamu hii yamekua mengi na huu ni mwanzo mzuri wa kuwapata wahusika.Mapambano yanaendelea hata nyuma ya kibodi kitaeleweka tu.

Mwisho watajulikana wote japo watatetewa na waliowatuma lakini itakua imekula kwao hawa vidagaa.

Nasema tena kama utakua daktari wa propaganda 2013 hadi 2015 katika nyanja yoyote ya siasa kuwa makini na njia zako za kujilinda na maadui zako ambao yoyote anayeingia katika game hiyo anapaswa kuwajua.

Mungu ibariki Tanzania
 
Huyu nae anapaswa kusaidia polisi, haiwezekani akae na muhalifu muda wote bila kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama.
 
Kapewa maagizo amkane mtu anayedai polisi walimruhusu azunguke Dar es Salaamu nzima akiwa uchi eti anamtafuta mjengwa
halafu pamoja na kutembea uchi eti kamtuma vitabu vya invoice ampelekee Iringa mjengwa tunakungoja mahakamani utakvyokonda kama piritoni kwa sababu wewe unajua nani ameng.oa mwangosi jicho shetani mkubwa weye
 
Nikijaribu kuunganisha dots nagundua kuwa huyo Ludovic nae ni mtu wao hao hao waliopanga deal la kuteka mwandishi wa habari. Ikiwa pale kwenye clip ya Rwakatare alitajwa, na ikiwagundulika kuwa ile clip si ya ukweli, basi huyu jamaa atakuwa lao moja na hao waliokamata. Hii muvi inavutia sana. Unaweza kuta mpaka suala la kukamatwa Iringa lilishapangwa. Ila na wasiwasi kuwa hata Manyerere anahusika kwa jinsi alivyoanzisha thread nyingine tarehe 15/3
 
Kapewa maagizo amkane mtu anayedai polisi walimruhusu azunguke Dar es Salaamu nzima akiwa uchi eti anamtafuta mjengwa
halafu pamoja na kutembea uchi eti kamtuma vitabu vya invoice ampelekee Iringa mjengwa tunakungoja mahakamani utakvyokonda kama piritoni kwa sababu wewe unajua nani ameng.oa mwangosi jicho shetani mkubwa weye

Mkuu punguza hasira! alieng'olewa jicho ni Kibanda sio Mwangosi! Mwangosi aligeuzwa kachumbari! aagh! walaaniwe!
 
A Friend in Need is a Friend Indeed..,

With Friends like maggid who needs an enemy ?, what happens to innocent until proven guilty ?

Hivi ikionekana amezingiziwa atamrudisha ?, nadhani angengoja kufanya haya pindi atakaposhitakiwa na sio tuhuma

nyie bana vipi?
sisi wenzenu (opportunists) mnataka tule wapi??
acheni izo bana!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu punguza hasira! alieng'olewa jicho ni Kibanda sio Mwangosi! Mwangosi aligeuzwa kachumbari! aagh! walaaniwe!
Yaani unapoona watu uliwaamini kama akina Mjengwa ukihudhuria blog zao kila siku ukidhani ni binadamu wenye utu kumbe nao wako kwenye mitandao ya kiharamia ya kisiasa, i hate this
 
Whatever happened to innocent until proven guilty? Ndo mablogger wenu hao, vichwa panzi!
Usisahau kumdai na nguo ulizompa siku ile alipovuliwa nguo na alleged vibaka.

Hapo sasa
Na nani aliemlipia taxi na kumpa jezi za kujistili
Nani aliempa lift na kumuaca sehemu aliyomuuliza kama iko salama
Maswali haya majibu yake ni ya ulakini
 
Ingependeza kama Mjengwa angesubiri uchunguzi na uthibitisho wa tuhuma kwa "udovick. Ina maana mkewe akituhumiwa atampa taraka? Nilitegema angesema watampa msaada kupata haki yake. Kuna jambo nyuma yake.
 
Yaani unapoona watu uliwaamini kama akina Mjengwa ukihudhuria blog zao kila siku ukidhani ni binadamu wenye utu kumbe nao wako kwenye mitandao ya kiharamia ya kisiasa, i hate this

Mkuu naomba nikuulize kitu please naomba unijibu live!
 
Napata shida kuelewa uwezo wako wa akili! labda ututhibitishie iweje mtu akituhumiwa wewe utoe hukumu kubwa hivyo?Ikithibitika kuwa ameonewa wewe utafanya nini? Ushabiki mwingine ni wa kipumbavu kama ulivyo mpumbavu wewe!

mbna mnasema wao 2 au tunajifanya wengine 2mewasahau. inabidi police anze na source mpka kwa lwakatare. nchemba,bukoba boy,mjengwa,michuzi hawa wote wanamajibu ya maswali ye2 yote.
 
A Friend in Need is a Friend Indeed..,

With Friends like maggid who needs an enemy ?, what happens to innocent until proven guilty ?

Hivi ikionekana amezingiziwa atamrudisha ?, nadhani angengoja kufanya haya pindi atakaposhitakiwa na sio tuhuma

Sio atakaposhitakiwa. Atakapohukumiwa.
 
Last edited by a moderator:
TAARIFA RASMI KUTOKA Mtandao Wa Kijamii Wa MJENGWABLOG

Sunday, 17 March 2013 | Written by Mjengwa Blog

Ndugu zangu,
Kutokana na kuwepo kwa taarifa rasmi za kipolisi zenye kumtuhumu Ludovic Joseph kuhusika na matukio ya kigaidi.

Uongozi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog unasitisha rasmi, kuanzia leo Jumapili, Machi, 17,2013, kuwa na Ludovick Joseph kama msaidizi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Maggid Mjengwa,
Mmiliki wa Mjengwablog /Kwanzajamii

Mjengwa yuo have something to hide?! why are you running scared? Ludo hajahukumiwa bali ametuhumiwa tu!!

Mjengwa akamatwe ahojiwe aseme anachokijua kuhusu tuhuma za ugaidi kutokana na uhusiano wake na mtuhumiwa Ludo!!
 
Back
Top Bottom