Lissu: Tuna taarifa za njama zinazopangwa na maadui wa Chama kushambulia mikutano yetu ya hadhara Shinyanga kwa mabomu ya kurusha na mkono

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,366
Taarifa iliyovuja inadokeza kwamba Mikutano ya Chadema ya Oparesheni 255 Kanda ya Serengeti , iliyopangwa kuzinduliwa kesho 25/08/2023 Shinyanga Mjini imepangiwa kuhujumiwa kwa kupiga Mabomu , na ikibidi kuua Watu ili kutisha Wananchi wasihudhurie Mikutano ya Chadema .

Hofu ya Wapanga njama hao inatokana na Ukweli kwamba , Mikutano ya Chadema kote inakopita inahudhuriwa na Maelfu ya Watu ambao wanaelewa mno kila kinachoelezwa na Chama hicho , ikiwemo Katiba Mpya na Ubovu wa Mkataba wa Bandari .

Hata hivyo tulishasema mara kadhaa humu kwamba , hakuna popote kwenye Dunia hii ambako Shetani aliwahi kumshinda Mungu .

Screenshot_2023-08-24-22-00-57-1.jpg
---

Katika ukurasa wake rasmi wa Twitter (X) Tundu Lissu anaandika yafutayo:

Tuna taarifa za njama zinazopangwa & maadui wa Chama chetu kushambulia mikutano yetu ya hadhara inayoanza mkoani Shinyanga kesho kwa mabomu ya kurushwa kwa mkono. Lengo lao ni kuua au kujeruhi watakaohudhuria & kuwatisha wananchi wengine ili wasihudhurie mikutano itakayofuata.

Hatuwezi kupuuzia taarifa hizi. Matukio ya kigaidi ya aina hii yalikwishatokea miaka ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Mikutano ya hadhara ya CHADEMA ilishambuliwa kwa mabomu Nyololo wilayani Mufindi, na Soweto mjini Arusha, na watu wasio na hatia waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Jeshi la Polisi halikuwahi kuchunguza matukio haya ya kigaidi na kuwachukulia wahalifu husika hatua zozote za kisheria. Kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Kikwete, vitendo hivi vya kigaidi havitapunguza nguvu ya mapambano ya kidemokrasia nchini kwetu, & wala havitatunyamazisha.
 
Hawa Jamaa wanapenda sana attentions nyepesi nyepesi

wakiwa na Watawala wanacheka cheka hawaoneshi haya makali wanayoonesha wakiwa na wana vijiji huko Mikoani

Leo Mbowe, Mnyika na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema walikuwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi katika kikao kazi, lakini wakiwa huko Mitaani utaskia hatutaki ushirikiano na msajili wa vyama vya Siasa ni mamluki na blaa blaa zingine

wiki hii mwanzoni Mnyika alikuwa kwny vikao vya ushirikiano na kina Kinana, Lipumba, Babu Duni n.k lakini wakiwa kwingine utaskia blaa blaa sijui hatushirikiani nao n.k
 
Hata aliposema kuna watu wanamfuatilia na gar flan mlipuuza na kuona mzushi, eventually akapigwa risasi!!
Babu Slaa alisema hiyo ni michezo ya ndani ya Chadema

tutaachaje kumuamini aliekuwa Kiongozi wa kiroho na Katibu Mkuu wa Baraza la .Maaskofu Tanzania bara na visiwani na pia Katibu Mkuu wa Chadema ambacho ndio Chama kikuu cha Upinzani kwa miaka mingi.
 
Back
Top Bottom