Mjengwa asitisha mahusiano na Ludovick Joseph kwa tuhuma za 'kuhusika na matukio ya kigaidi'

Kwanini umkane leo? Mnalo la kutuambia na lazima mtuambie

Mjengwa naye akamatwe atoe ushirikiano kwa jeshi la polisi. Kwanini umfukuze kazi ludovick haraka baada ya kuhusika kwenye utekaji na siku ya tukio la kibanda ludovick alikuwa na mjengwa maeneo ya kazini kwa kibanda muda wa saa tano 5 usiku tena muda ambao ndio kibanda aliteswa...kuna kitu hapa

Mjengwa ametudhihirishia kuwa naye yumo kwenye dili hapa anataka kujisafisha tu

it sounds! Mjengwa nae akamatwe! Polisi wanasubiri nini?
 
Wa TZ wanafiki na wabinafsi sana shame on you Mjengwa!
Umeshamhukumu kabla ya mahakama?
 
sasa mlitaka aendelee kumkumbatia muuaji! Kama kuhusika Ludovick na Lwakatare tusubili wataendelea kutaja waalifu wenzao!
Napata shida kuelewa uwezo wako wa akili! labda ututhibitishie iweje mtu akituhumiwa wewe utoe hukumu kubwa hivyo?Ikithibitika kuwa ameonewa wewe utafanya nini? Ushabiki mwingine ni wa kipumbavu kama ulivyo mpumbavu wewe!
 
maggid amechemka kumfuza Ludovick haraka kiasi hiki! Kwanza ilitakiwa mpaka mshikaji wake apatikane na hatia ndiyo angemtema! Je akiwa hana hatina na ulikuwa uzushi si itakuwa aibu kwa Mjengwa?

Sijalisapoti jambo hili kabisa.
we unajua kiswahili lakini au mnataka kila mtu aongee kichagga!amesema amesitisha,kusitisha na kufuka ni vitu viwili tofauti bwashee!alichokifanya mjengwa ndicho kinachofanywa kwenye nchi za wenzetu,haiwezekani mtu anaekabiliwa na tuhuma nzito kama hizo(hata kama sio kweli)uendelee kufanya nae kazi au umuacha kazini,kiungwana anatakiwa akae pembeni kwanza ili alimalize suala lake na kujisafisha then anarudi kazini,ni utaratibu wa kawaida tu sema haujazoeleka sana hapa kwetu,mtu ana mituhuma kibao lakini bado yumo tu,wenzetu kwanza ni yeye mwenyewe anaandika barua kuomba akae pembeni kwanza,hata huyu lwakatare kwa tuhuma zinazomkabili ilitakiwa ama aandike barua yeye mwenyewe kupitia lawyer wake kwamba ananchia ngazi nafasi zote chamani au chama kichukue hatua hiyo ili kujiweka kando na suala lake mpaka atakaposafishwa.tufike huko watz!
 
Huyu jamaaa ni mnafiki sana ngoja tusubiri kumsusa mwenzie haipelekei yeye kuonekana ni muungwana! Anaeongozana na mwizi siku zote nae huwa ni mwizi.
 
Alisema hawakuwahi kumuajiri sio?
huwezi sitisha kama huna mkataba nae

Una uhakika na unachokiongea? Mjengwa alikuwa anamtumia Ludovick kwenye kupeleka invoice kwa wateja wake; alikuwa anamtumia kwa kupost magazeti ya kila siku. Sasa amesema kutokana na Ludovick kuwa na tuhuma polisi za jinai, yeye Mjengwa kama mmiliki, hatomtumia Ludovick katika kazi zake hizo. Sasa ya ajira na mkataba umeyatoa wapi?
 
A Friend in Need is a Friend Indeed..,

With Friends like maggid who needs an enemy ?, what happens to innocent until proven guilty ?

Hivi ikionekana amezingiziwa atamrudisha ?, nadhani angengoja kufanya haya pindi atakaposhitakiwa na sio tuhuma

Nadhani anachofanya mjengwa ni kwamba anampa nafasi bwana Ludovic akajisafishe mahakamani kwa sasa. Kama akionekana hana hatia atarudishwa kuendelea na shughuli zake.
 
TAARIFA RASMI KUTOKA Mtandao Wa Kijamii Wa MJENGWABLOG

Sunday, 17 March 2013 | Written by Mjengwa Blog

Ndugu zangu,
Kutokana na kuwepo kwa taarifa rasmi za kipolisi zenye kumtuhumu Ludovic Joseph kuhusika na matukio ya kigaidi.

Uongozi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog unasitisha rasmi, kuanzia leo Jumapili, Machi, 17,2013, kuwa na Ludovick Joseph kama msaidizi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Maggid Mjengwa,
Mmiliki wa Mjengwablog /Kwanzajamii

Too Late Mjengwa, akikutaja kuwa mipango alifanyia pale kwako na kwamba siku ya tukio alirudi chupi tupu pale kwako, polisi hawawezi kukuacha ukawa uraiani hivi hivi tu bila kutikiswa kidogo. Binafsi sikuhusishi kabisa lakini taratibu hazitambui huruma niliyonayo juu yako.

Lakini: In Allah Maswabirina
 
Mjengwa gangamala wewe! Achana na tabia ya kishenzi ya kutoa matamko ya kijinga.

Kakufaa sana, kakusaidia sana, umekuwa naye muda mrefu akikupa scoops za usalama. Sasa limefumuka, unamruka! (you are a weak character). Kwa nini usingekaa kimya tu ukakomaa kama mwanaume mpiganaji????

1. Maandishi na machapisho yako ya Raia Mwema hayana mkono ya Ludovick??

2. Ludovick amekuwa ni chanzo chako cha habari nyingi (Utakataa au utatoa TAMKO??????????????????
 
TAARIFA RASMI KUTOKA Mtandao Wa Kijamii Wa MJENGWABLOG

Sunday, 17 March 2013 | Written by Mjengwa Blog

Ndugu zangu,
Kutokana na kuwepo kwa taarifa rasmi za kipolisi zenye kumtuhumu Ludovic Joseph kuhusika na matukio ya kigaidi.

Uongozi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog unasitisha rasmi, kuanzia leo Jumapili, Machi, 17,2013, kuwa na Ludovick Joseph kama msaidizi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Maggid Mjengwa,
Mmiliki wa Mjengwablog /Kwanzajamii

Mjengwa ni coward. Hii inadhihirisha alikuwa mshiriki wa suala la Kibanda. Ni kudanganya umma.

Vipi urafiki gani huo? Je kama hiyo ni tuhuma tu utamweleza nini rafiki yako? Waswahili wana sema ije mvua au jua rafiki atabaki rafiki.


MBONA MPO WEPESI SANA KUJIUMBUA? Makamba sinior alikuwa sahihi kuwaambia sisiem wasiende kujieleza kwenye Tv wakati wa mdahalo. Bosi wenu awaambie msiende kwenye mitandao ya kijamii kama verified users
 
Kwa nini mtu huyu atoe hukumu kabla ya hukumu ya kimahakama?
Au mwenzetu anao ushahidi unaomuhusisha Ludovick moja kwa moja na tukio ya utekwaji wa Kibanda?
 
maggid kaka yangu...ulilofanya si jema...nachungulia google group ya wanabidii post zako zimekaa kung'ata na kupuliza hasa kwenye hii link: https://groups.google.com/forum/?fromgroups#!topic/wanabidii/EeEDJUVw4K4

ninai-post na huku ili wengine waione

"Ndugu zangu,
Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.
Namfahamu kijana Ludovik tangu akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini.
Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi kwa namna fulani nimeshtushwa nazo. Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii. Amekuwa na mchango mkubwa, na hata katika miezi ya karibuni,ndiye yeye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti kwenye Mjengwablog kila asubuhi. Akiwa Dar na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali , amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice kwa watangazaji kwenye Mjengwablog. Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti'.
Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.

Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana. Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima.

Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo. Na jamii, ikiwamo mimi, itamlaani vikali.
Hapa chini ni maelezo niliyoyaandika kwenye ukuta wangu wa facebook, siku ile Ludovick alipopatwa na mkasa wa kuvamiwa usiku;
... Na Msaidizi Wa Mwenyekiti Naye Alitekwa Na Majambazi Jana Usiku!

"Kijana Ludovik Joseph. Tulikula wote na kuongea pale Rose Garden jana usiku. Tuliondoka kwenye saa tano usiku. Nikamfikisha mpaka kona ya Shekilango na Morogoro Road. Hapo aliniambia angepata daladala öa kumfikisha nyumbani kwake. Nilimwuliza jambo tu; " Ni salama hapa kukuacha?"
Akanijibu ni salama maana amesafiri mara kadhaa katika muda huo.

Masikini, akafikwa na balaa la kutekwa na majambazi kwenye bajaji. Nilikofikia Dar nikaamshwa saa kumi za usiku. Mlinzi akaniambia kuna ndugu yako amekuja na teksi hata nguo hana. Amebaki na nguo ya ndani tu. Amekabwa na majambazi.

Nikamsaidia Ludovik. Na kwa vile yeye ni Yanga, basi, nikahakikisha nampa suruali na jezi ya Simba!

Naam, iko siku, kila mtu ataishabikia Simba!

Pichani Ludovick akisimulia mkasa uliomkuta kwa Mwanzo Millinga na Joseph Kulangwa. Ndugu yangu Kulangwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Habari Leo."







kaka yangu maggid kuna hili neno la leo umeweka leo ref link: https://groups.google.com/forum/?fr...dii/maggid/wanabidii/wPS4j2QK8H0/ro2pV3ANd7kJ

Ndugu zangu,

DUNIANI hakuna miujiza katika kuyafikia mafanikio. Hakuna njia za mkato pia. Ni sharti tufanye kazi kwa bidii. Tusiwe ni watu wenye kutanguliza taamaa na hata kuwadhulumu wengine.

Tuyaishi maisha ya kadiri. Ni kwa kuyafanya yale yaliyo ndani ya uwezo wetu.

Maana, ni wachache duniani walioweza kufanya miujiza kama tunayoambiwa kwenye vitabu vya dini; Bwana Yesu yu miongoni mwa wachache hao. Tunasoma, kuwa Mafalisayo walimshangaa Yesu na mafanikio yake. Wakatamka; “ Hivi ni Yesu huyu huyu mwana wa Joseph fundi Seremala!”

Naam, mwanadamu usitazame tu alipofikia sasa mwanadamu mwenzako kwenye safari yake. Jitahidi uangalie mwanzo wa safari yake. Alikotokea. Ndipo hapo utayapata ya kujifunza.

Papa Francis wa Kanisa Katoliki amefikia kiwango cha juu cha mafanikio kwenye ngazi ya kanisa. Ni rahisi kumwangalia hapo alipo, lakini ni muhimu kuiangalia safari yake ilipoanzia.

Tunasoma leo, kuwa Papa Francis ni mtu wa kadiri. Muda wote wa uhai wake amejitahidi kuishi maisha ya kadiri. Papa si mtu wa makuu. Na kule Vatican wanashangazwa hata na mavazi yake yasio gharama kubwa, ikiwamo viatu pia.

Hapa kwetu Tanzania Julius Nyerere ni mfano wa viongozi walioishi maisha ya kadiri. Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Ni mfano wa kuigwa.

Ni Neno La Leo
Maggid Mjengwa,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz/ Show trimmed content



Maneno yaliyoko in red yanakuhukumu wewe mwenyewe...ingekuwa vyema ufunguke zaidi kama kuna habari chini ya carpet uzitoe....tuna wasiwasi sana na wewe,na hiyo inaweza ikapelekea tukawa na wasiwasi wa habari zako pia
















Previous Previous Page 1
NextNext
 
Kwanini umkane leo? Mnalo la kutuambia na lazima mtuambie

Mjengwa naye akamatwe atoe ushirikiano kwa jeshi la polisi. Kwanini umfukuze kazi ludovick haraka baada ya kuhusika kwenye utekaji na siku ya tukio la Kibanda Ludovick alikuwa na mjengwa maeneo ya kazini kwa kibanda muda wa saa tano 5 usiku tena muda ambao ndio Kibanda aliteswa...kuna kitu hapa

Mjengwa ametudhihirishia kuwa naye yumo kwenye dili hapa anataka kujisafisha tu

Katika yako yooote, hapa tu ndio una point.
 
Hapa mkuu Mjengwa ule ujasiri wako umepotea na siamini kama umepotea bure kuna kitu umepewa.Mjengwa ninaye mfahamu mimi angesimama kidete kuhakikisha mpaka anajua mwisho wa jambo hili.Mbona ameshaandika makala nyingi za upelelezi?
 
Back
Top Bottom