Mjane: Kwa miaka 64 mume wangu alinificha kuwa ni Afisa wa Usalama wa Taifa

Akupe kitambulisho wewe kama nani! Kwanza hairusiwi hata kukionesha.

Ulikutana na muuza mihogo akakuambia yeye ni ofisa usalama nawe ukajaa 😂
Kama umesoma vizuri hakuna mahali niliposema kwamba alinambia ni afisa usalama, lakini pia hata ungekuwa wewe nina imani ungekaa tu.
 
Mimi jana tu nimekutana na njemba tukapishana kauli akaanza kunitishia kwa maneno ya kipuuzi, et mimi hata RPC kwangu ni mdogo nikawa nacheka sana akazidi kujaa nyembe mara apige simu kuita sijui askari, mara aombe kikosi sijui wapi huko mwisho akasema nina bahati vikosi vipo mbali, nilichomfanyia sasa hivi familia nzima wananipigia simu kuniomba msamaha.
 
Wanasema Afisa wa Usalama wa Taifa anatakiwa kuwa Mtu mwenye uwezo wa kutunza siri za kazi lakini pia yeye mwenyewe kutojitambulisha au kusema kwa Watu kama anafanya kazi kwenye Idara hiyo nyeti kwenye Taifa lolote.

Sasa huko Uingereza Mwanaume mmoja aitwae Glyndwr amejichukulia sifa za kutosha baada ya kufariki ambapo Mjane Audrey Phillips (85) juzi ndio amekuja kujua kwamba Glyndwr ambae ni Mume aliyeishi nae kwa miaka 64, alikua Afisa Usalama wa Taifa huko Uingereza.

Amefahamu vipi? …..ni baada ya kifo cha Mume wake huyo ambapo alikua akipanga vitu nyumbani ndipo alipokutana na makaratasi yakionyesha kwamba Glyndwr alikua Afisa Usalama toka akiwa na umri wa miaka 13, Mjane huyu anasema kwa miaka yote ya ndoa alijua Glyndwr alikua Injinia (Mhandisi).

Karatasi zilizomfanya atambue kazi aliyokua akiifanya Marehemu Mume wake ni karatasi za siri ambapo Jamaa alikua ameandika historia yake fupi na kuelezea jinsi alivyoanza kuwa Jasusi kwenye miaka ya 1940, Glyndwr alifariki akiwa na umri wa miaka 83.

Audrey anasema hakuwahi kushtuka chochote kuhusu hiyo kazi ya Ujasusi ambapo Glyndwr alikua akifanya kazi zake mbali na nyumbani mara nyingi sana, sasa imebidi Mjane huyu aandike kitabu kuhusu maisha yake na ya Marehemu Mume wake.
Hapa kwetu vipi?
 
Nilichogundua alikuwa mweupe tu ila maneno na tambo vilimzidi, nilimuomba kitambulisho akagoma nikampeleka polisi yupo huko mpaka leo nitamtoa nikijiridhisha na maneno yake.
Yale yale na wewe unavimba hapa JF tukujue.
 
Wakati wa mwalimu kuwagundua (usalama wa taifa) ni kazi!!
Zi kweli yalikuwa ni yale yale tu,sema wakati ule watu wote walikuwa kama askari ivo ilikuwa si rais kumpata mtu. Usalama wa taifa walikuwa wanajulikana na mpaka wakienda safari na viongozi wa juu watoto zao huwa wanakuja na kutamba mashule tuliposoma nao,pia wengine walikuwa wa pombe za kienyeji wakifika kule wanajulikana.Kama unapajua makumbusho pale palikuwa na mjengo wao sijuinkama bado wapo,wengine Ikulu mjini tena kama mshikaji wako anafanyakazi mle unaingia ki uraini tu.
 
Zi kweli yalikuwa ni yale yale tu,sema wakati ule watu wote walikuwa kama askari ivo ilikuwa si rais kumpata mtu. Usalama wa taifa walikuwa wanajulikana na mpaka wakienda safari na viongozi wa juu watoto zao huwa wanakuja na kutamba mashule tuliposoma nao,pia wengine walikuwa wa pombe za kienyeji wakifika kule wanajulikana.Kama unapajua makumbusho pale palikuwa na mjengo wao sijuinkama bado wapo,wengine Ikulu mjini tena kama mshikaji wako anafanyakazi mle unaingia ki uraini tu.
Aisee wanaingia Ikulu hovyo hovyo
 
Huku Tanzania kijana akijiunga na UVCCM akishavaa shati la kijani tu anawachapa makofi mabaamedi na kujitapa yeye ni usalama wa taifa na atatangaza huwa anaongea na rais ana kwa ana.
Tatizo la vijana wengi background zao za umasikini ndio shida kubwa,akibahatika kupata visenti kidogo na kujuana na watu kadhaa ndani ya serikali hujiona naye ni mtu wa maana.
Tatizo ni umasikini huko kwao vijijini walikotoka.
 
Hawa wa wabongo wakinywa ulanzi wakashiba unasikia "unanijua mimi ni nani". Mimi huwa nawajibu wewe ni kenge.
Mzee huwa una uwezo wa "kusambaza karate" kwa watu kama wangapi kwa wakati mmoja? Maana Karate huwa haipigwi, huwa inasambazwa. Hii ni kwa mujibu wa afande wangu mmoja JKT. Ilikuwa akichaji anapiga mkwara mzito na push-up juu halafu anaanza kusema "tuone sasa kama kuna mtu anaweza kusmbaza karate hapa"
 
Back
Top Bottom