SoC03 Ujasiri wa Afisa Tito utakaokumbukwa kwenye Idara ya Usalama wa Taifa

Stories of Change - 2023 Competition

Kanyu Landa

New Member
Jul 30, 2023
2
0
Kama zilivyo taratibu za utendaji kazi wa Idara ya Usalama wa Taifa, uliletwa mpango wa kuongeza nguvu kazi katika Idara ya Usalama, hatua hii ilitokana na kushamiri kwa matukio ya ugaidi na ulanguzi wa dawa za kule vya Tanzania.

Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa anamteua Afisa Temba na kumpa jukumu la kutafuta vijana 10 watakaochukuliwa kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi na baadae kuingia Idara ya usalama wa Taifa.

Afisa Temba anafanya kazi kwa weledi na kuwapata vijana 10. Tito ni moja ya kijana aliepata bahati ya kuchaguliwa akiwa mhitimu wa masomo ya biashara kutoka chuo cha taifa.

Vijana wote waliitwa kwenye kambi ya jeshi iliyoko Kijiji cha Katunze Mkoani Mara kwa ajili ya mafunzo. Baada ya miezi 12 wanahitimu mafunzo huku Kijana Tito akifanikiwa kuibuka kinara katika mafunzo hayo na kutunukiwa CHETI CHA UADILIFU kilichotolewa Mhe. Rais aliekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo.

Kwenye hutoba Mhe. Rais aliwasisitiza Maafisa hao kuwa wazalendo kwa Taifa lao, na kuwasihi kuwa “hakuna aliemkubwa kuliko Taifa, na sote tunaongozwa kwa katiba ya nchi, hivyo niwaombe mkawe askari wema mtakao linda, kusimamia na kutetea maslahi ya Taifa” wote waliitikia kwa heshima huku wakipiga saluti kama ishara ya utii.

Je, baada ya Mafunzo ya Kijeshi ni nini Kinafuata?

Baada ya miezi minnne, Afisa Tito anapigiwa simu na mtu asiemfahamu anaejitambulisha kama Afisa kutoka Ofisi ya Serikali, aliomba akutanae nae katika hoteli moja pembezoni mwa mji karibu na yaliko makazi ya askari wa magereza.

Tito anaitikia wito na kwenda kukutana na Afisa yule, Afisa anampa Tito pongezi kwa kuhitimu mafunzo ya kijeshi, na kisha akampa maelekezo mafupi na barua iliyokuwa imeandikwa SIRI. Aliporudi nyumbani alifungua barua ile na kukuta maelekezo pamoja na tiketi ya kwenda Israel kwa ajili ya mafunzo ya Ujasusi.

Tito anafanikiwa kusafiri na anafika Israel salama huku akipokelewa na balozi wa Tanzania. Na baadae anaelekea chuoni kuanza kozi ya Ujasusi na mafunzo maalumu ya kudhibiti dawa za kulevya. Tito anahitimu kozi ya ujasusi baada ya miezi 12 tu, huku akitunukiwa tuzo ya afisa bora wa mwaka. Tito anarejea nchini na kwenda kuripoti ofisi ya mkurugenzi wa usalama wa taifa.

Je, ni nini kitafuata baada ya kurejea Nchini?

Mkurugenzi anamkabidhi Tito jukumu zito la kuendesha Oparesheni GXR ya kubaini mtandao wa walanguzi wa dawa za kulevya katika Jiji ambalo wazazi wake walikuwa wakiishi.nAfisa Tito anaanza kazi mara moja, huku akitengeneza mfumo mzuri ya ukusanyaji wa Taarifa ambazo zingeweza kumsaidia. Baada ya muda wa mwaka 1 anapata taarifa za uwepo wa mtandao wa ZONZA uliokuwa ukihusika na kusambaza dawa za kulevya Afrika. Katika ufatiliaji zaidi anagundua kuwa Shirika moja la kutoa msaada kwa watoto yatima linahusika.

Ni shirika lililoanzishwa na kuendeshwa na Baba yake mzazi linahusika na ZONZA, huku akishirikiana na Mkurugenzi wa Bandari na Afisa Udhibiti wa Kemikali ambao walikuwa wakihusiana kwa ukaribu na wafanya biashara wawili wakubwa Afrika.

Tito anaenda kufanya uchunguzi kwenye chumba cha Siri cha baba yake, ambapo katika upekuzi alikuta karatasi yenye ramani imeandikwa The Secrets Of ZONZA “Siri za ZONZA” na Notebook iliyoandikwa After Me “Baada Yangu”.

Baada ya kupitia nyaraka zile aligundua taarifa za siri za Mtandao wa ZONZA unaohusika na kuuza dawa za kulevya, mfumo wa uendeshaji na washiriki wakuu wa mtandao huo, anagundua pia kuwa katika jengo analomiliki Baba yake ambalo liko chini ya shirika la kusaidia watoto yatima, ndio zilipo ofisi za ZONZA na ofisi ya mhasibu mkuu wa shirika ndio iliyokuwa ikiendesha usambazaji wa dawa. Mtandao wa ZONZA ulihusisha pia baadhi ya watumishi wa Serikali.

Ndani ya ile notebook iliyoandikwa After Me, ilikuwa na taarifa zingine za Siri sana za shirika na Mtandao wa ZONZA, huku ikionesha kuwa Mtoto wa Mzee Ivan aitwae Tito (afisa usalama) ndie anaetarajiwa kuwa mrithi mkuu wa mtandao huo siku za usoni. Baba yake alimsomesha masomo ya biashara ili kumwandaa kuwa kiongozi wa Mtandao wa ZONZA, uliokuwa tishio Afrika.

Taarifa zile zilizidi kumchanganya sana. Lakini Tito anakamilisha ripoti yake kwa ufanisi mkubwa.

Nini Kitafuata Baada ya Ripoti Kukamilika?

Haikuwa rahisi kuipeleka ripoti ile kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, kwani ilikuwa inaenda kuwaweka hatiani Baba yake kwa kupata kifungo cha maisha jela, na ndugu wengine waliokuwa kwenye mtandao wa ZONZA, huku mali zote zikienda kutaifishwa kwa mujibu wa Sheria. Ilimchukua siku 15 kutafakari juu ya uamzi wake.

Afisa Tito alikumbuka kiapo chake cha utumishi mwema kwa Taifa, Na ile hotuba ya Rais wakati wa kuhitimu mafunzo ya kijeshi, aliyosisitiza sana juu ya Uzalendo akinukuu “Maafisa nawaomba sana mkawe wazalendo wa kweli kwa Taifa lenu, na hakuna alie mkubwa zaidi kuliko Taifa lenu na wote tunaongozwa kwa katiba moja, hivyo niwaombe mkawe maafisa mtakaolinda, kusimamia na kutetea maslahi ya Taifa”. Baada ya kumbukumbu ile, Tito aliamua kupeleka ripoti kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.

Ni Nini Kitafuta Baada ya Ripoti Kupokelewa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa?

Mkurugenzi anaisoma ripoti, anashangaa anachokiona katika ripoti ya Oparesheni GXR, Kuwa Mtandao mkubwa wa ZONZA ulikuwa unaongozwa na Baba yake Tito. Lakini alijiuliza sana kwanini pamoja na yote Tito hajasita kuleta taarifa hii kwenye Ofisi ya Mkurugenzi?

Mkurugenzi alimuita Tito na alipofika alimuliza swali Moja tu Tito “Ni kwanini umeamua kuleta ripoti hii kama ilivyo, bila kusita wala kuogopa”? Tito alijibu, nalipenda Taifa langu, Nimeapa kulilinda na kulitumikia Taifa langu bila woga na hofu naomba mamlaka zifanye kazi yake ili Tuliokoe Taifa dhidi ya madawa.

Mhe. Rais alifikishiwa ripoti ile na akatoa maagizo ya kufuata sheria dhidi ya wahusika wote. Baadae walifungwa kifungo cha miaka 30 jela na ikawa mwisho wa mtandao tishio wa ZONZA wauza madawa Afrika.

Faida
Uadilifu mkubwa wa Tito utakumbukwa daima katika historia ya idara ya usalama wa taifa kwa uaminifu na uwajibikaji mzuri, kwa kuzuia hisia binafsi za undugu katika kazi na kuliokoa taifa kutoka katika mtandao hatari wa ulanguzi na usambazaji wa dawa za kulevya Afrika.

Ili kujenga uwajibikaji wa kweli na wenye tija pamoja na utawala bora ni muhimu kuwa na ukomavu wa kihisia.
 
Back
Top Bottom