Mjane: Kwa miaka 64 mume wangu alinificha kuwa ni Afisa wa Usalama wa Taifa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,324
2,000
Wanasema Afisa wa Usalama wa Taifa anatakiwa kuwa Mtu mwenye uwezo wa kutunza siri za kazi lakini pia yeye mwenyewe kutojitambulisha au kusema kwa Watu kama anafanya kazi kwenye Idara hiyo nyeti kwenye Taifa lolote.

Sasa huko Uingereza Mwanaume mmoja aitwae Glyndwr amejichukulia sifa za kutosha baada ya kufariki ambapo Mjane Audrey Phillips (85) juzi ndio amekuja kujua kwamba Glyndwr ambae ni Mume aliyeishi nae kwa miaka 64, alikua Afisa Usalama wa Taifa huko Uingereza.

Amefahamu vipi? …..ni baada ya kifo cha Mume wake huyo ambapo alikua akipanga vitu nyumbani ndipo alipokutana na makaratasi yakionyesha kwamba Glyndwr alikua Afisa Usalama toka akiwa na umri wa miaka 13, Mjane huyu anasema kwa miaka yote ya ndoa alijua Glyndwr alikua Injinia (Mhandisi).

Karatasi zilizomfanya atambue kazi aliyokua akiifanya Marehemu Mume wake ni karatasi za siri ambapo Jamaa alikua ameandika historia yake fupi na kuelezea jinsi alivyoanza kuwa Jasusi kwenye miaka ya 1940, Glyndwr alifariki akiwa na umri wa miaka 83.

Audrey anasema hakuwahi kushtuka chochote kuhusu hiyo kazi ya Ujasusi ambapo Glyndwr alikua akifanya kazi zake mbali na nyumbani mara nyingi sana, sasa imebidi Mjane huyu aandike kitabu kuhusu maisha yake na ya Marehemu Mume wake.
 

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,324
2,000
Huyu jamaa
Screenshot-2019-05-25-at-06.02.19-1.jpeg
Screenshot-2019-05-25-at-04.10.41.jpeg
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,836
2,000
Unajua wenzetu nchi zilizoendelea vitengo vyao vya usalama na ujasusi vimegawanyika sehemu nyingi. Kuna wale undercover ambao ni wa kujificha sana hata familia zao hazijui kama wako kwenye hiyo kazi.

Nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha jamaa wa team SEAL kutoka USA alikuwa anazungumzia kuhusu maajenti wa CIA. Alisema kwenye makao makuu kuna sehemu ya kumbukumbu yenye medali na orodha ya majina ya viongozi wa CIA waliofia kwenye mision. Jamaa alisema kuna sehemu unakuta kuna medali tu bila jina. Akasema hao ni wale ambao hawatakiwi kujulikana hata kwenye umauti wao!

Bila shaka na huyo alikuwa mmoja wa wale ambao hawatakiwi kujulikana kabisa hata baada ya kufariki.
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,836
2,000
Njoo Bongo sasa,utake kujua usitake kujua utaambiwa kwa lazima ili ujue na uwaheshimu watu mjini hapa!
Ila Bongo kipindi cha Nyerere ilikuwa tofauti sana. Wana usalama wa Taifa hawakuwa watu wa makeke na walikuwa wako down to the earth! Kuna jamaa mmoja (ameshafariki) alikuwa msomi mzuri na kila mtu anajua hivyo. Siku moja jirani yake akiwa Arusha akamwona ameshika fyekeo anafanya kazi kama kibarua kwenye ofisi moja ya umma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom