Mjane aliyezuiwa kuingiza Ndizi Zanzibar adai wanaomdai wanataka kwenda kumfilisi, asema ameathirika Kisaikolojia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Wiki chache zilizopita, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Biashara wa Zanzibar, Shamata Shaame Khamis alitoa ufafanuzi kihusu tukio la kutaifisha tenga za ndizi za mfanyabiashara Veronica Mwanjala aliyekuwa akizisafirisha kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa ajili ya biashara.

Mamlaka kutoka Zanzibar ziliweka wazi kuhusu sheria au kanuni ya katazo la kuingiza ndizi ambalo lipo Kisiwani hapo, ikiwa ndilo lililotumika katika maamuzi ya kuzuia ndizi hizo kuingizwa.

Tangu kutokea kwa tukio hilo ukimya umetawala, lakini upande wa pili mwathirika wa sakata amebaki akiwa na hali mbaya kiuchumi huku akidai kuandamwa na madeni makubwa baada ya mtaji wake kuangushwa.

Huyu hapa anaelezea kilichotokea...

Anakumbushia kilichotokea
“Baada ya kushusha mzigo wangu na wahusika kuushikilia katika Bandari ya Zanzibar, Waziri alikuja akiwa ameongozana na waandishi wa habari akanieleza kuwa Sheria ya Zanzibar hairuhusu kuingizwa kwa ndizi kutoka nje.

“Pamoja na kunielimisha hivyo lakini aliniruhusu kuingiza ndizi hizo kwa siku hiyo tu na kuniambia kuwa kama nitarudia kufanya kosa hilo nitapelekwa Mahakamani kisha jela.

“Alipoondoka huku nyuma mama ambaye ni msimamizi wa mizigo pale Bandarini hakunipa mzigo, aliuzuia na kuniambia wanaupeleka kwa Wafungwa gerezani huku nikitakiwa kulipa faini Tsh. 50,000 niliumia sana kwa kuwa ndio mtaji niliokuwa nautegemea.

“Siku tatu baadaye wakanipigia simu kuniambia niende nikauchukue mzigo niurudishe ulipotoka, lakini kwa kuwa sikuwa na hela ya kulipia gharama za kuusafirisha na hata za mimi mwenyewe tu kujilipia kusafiri, sikufanya hivyo, pia kumbuka zile ni ndizi, kwa siku tatu zilikuwa zimekaa tu pale Bandarini hivyo zikawa zimeshaanza kuharibika.

Kwa nini Zanzibar na matenga yalikuwa mangapi?
“Matenga yalikuwa 30 na si 15 kama ilivyokuwa inasemwa, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwenda Zanzibar kupeleka ndizi.

“Nilikubaliana na watu wenye mahoteli kuwa nitawauzia ndizi moja Tsh. 500. Ningefanikiwa kuuza mzigo wote ungekuwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.15 hivi.

Nini kinaendelea
“Muda mwingi nautumia kitandani nimelala sijui nini cha kufanya, mtaji wangu umekufa, nadaiwa, nilikopa hela ambayo nilikuwa narejesha kila baada ya wiki.

“Hapa nina wiki mbili sijalipa marejesho, nipo katika wakati mgumu, kuna Mbunge mmoja wa Bagamoyo alinipigia simu kwa lengo la kunisaidia, lakini baadaye alipofuatilia akaniambia kuwa amejibiwa kuwa kilichofanyika ni sheria ya Zanzibar na hana njia nyingine ya kunisaidia.

“Wanaonidai kule nilipokopa wanataka kuja kunifilisi maana sina cha kuwalipa na sina cha kufanya, mimi na wanangu hatuna uhakika wa kula kwani mume wangu alishafariki muda mrefu.

“Bado nadaiwa Tsh. 750,000 mpaka sasa na sijui nitailipaje.

“Mwanangu mkubwa anasoma chuo, alizuiwa kufanya mitihani lakini baada Chuo kuona hilo sakata mitandaoni nilienda kuwaomba wakanikubalia mwanangu afanya mitihani kisha nitalipa ada baadaye.

Athari za afya
“Hili suala limeniathiri sana kisaikolojia, tangu wakati huo nimekuwa nashinda ndani muda mwingi, nguvu zimeniisha japo mimi ni mpambanaji, nahisi akili yangu haipo sawa.

Wito kwa Serikali
“Namuomba Rais Samia na Serikali yake kwa jumla anisaidie kwa kuwa mimi siombi msaada nikiwa nimekaa bali nina hali mbaya kiuchumi, nina nguvu ya kufanya kazi, ni mjane ninayepambana, lakini matukio kama haya yanakatisha tamaa.

“Ombi langu kwa Serikali ni kuwa kwa watu tunaojituma kama mimi, ambao hatujaingia kwenye shughuli ya kujishushia heshima, basi tutengenezewe mazingira ya kutusaidia.

“Nilipeleka ndizi Zanzibar kwa kuwa niliamini ni biashara yenye faida, kama ni changamoto ya magonjwa ya mimea nadhani mkemia mkuu wa Serikali angeweza kufanya kazi yake kupima kama kweli hazina ubora.”

Pia soma: Zanzibar: Serikali yazuia Mazao ya Ndizi kutoka nje, ndizi za Veronica Mwanjala kuharibiwa ili kuzuia Magonjwa
 
Mamlaka kutoka Zanzibar ziliweka wazi kuhusu sheria au kanuni ya katazo la kuingiza ndizi ambalo lipo Kisiwani hapo, ikiwa
Huu ni ujinga wa viongozi wa Bara.
 
Katazo la kuuza ndizi liliwekwa lini kwani. Serikali ya Zanzibar inaweza kuwa na hatia endapo iliweka katazo ghafla bila kutoa taarifa mapema siku kadhaa kabla, kwa kuzingatia sababu ya kuzuia. Serikali makini mfano leo tarehe 17 Februari ingetangaza kuwa kuanzia tarehe 30 Februari ni marufuku kuingiza ndizi.

Miaka ya juzi hapo Kassim Majaliwa alitangaza kuzuia biashara ya viroba ghafla, yani alifyatuka tu akatoa kauli za 'kuanzia sasa' jambo ambalo nchi zilizoendelea serikali itafunguliwa mashtaka na wafanyabishara kwa wendawazimu wa aina hiyo. Kuna jamaa alikuwa na mzigo wa zaidi ya bilioni moja alijipiga risasi kama mnakumbuka. Katazo la mifuko ya plastiki lililotolewa na Makamba lilitoa muda wa kujipanga ukaacha kuagiza inventory mpya.

Otherwise kama taarifa zipo muda mrefu basi serikali haiendeshwi kwa huruma. Na huyo Waziri aliyesamehe ingekuwa nchi zinazojielewa ashaachishwa kazi.
 
Katazo la kuuza ndizi liliwekwa lini kwani. Serikali ya Zanzibar inaweza kuwa na hatia endapo iliweka katazo ghafla bila kutoa taarifa mapema siku kadhaa kabla, kwa kuzingatia sababu ya kuzuia. Serikali makini mfano leo tarehe 17 Februari ingetangaza kuwa kuanzia tarehe 30 Februari ni marufuku kuingiza ndizi.

Miaka ya juzi hapo Kassim Majaliwa alitangaza kuzuia biashara ya viroba ghafla, yani alifyatuka tu akatoa kauli za 'kuanzia sasa' jambo ambalo nchi zilizoendelea serikali itafunguliwa mashtaka na wafanyabishara kwa wendawazimu wa aina hiyo. Kuna jamaa alikuwa na mzigo wa zaidi ya bilioni moja alijipiga risasi kama mnakumbuka.
Katazo la mifuko ya plastiki lililotolewa na Makamba lilitoa muda wa kujipanga ukaacha kuagiza inventory mpya.

Otherwise kama taarifa zipo muda mrefu basi serikali haiendeshwi kwa huruma. Na huyo Waziri aliyesamehe ingekuwa nchi zinazojielewa ashaachishwa kazi
2017
 
Kwanini Zanzibar waliweka katazo hili la ndizi?Pia sisi ni tupo katika Muungano au kila mmoja anajitegemea,maana sijaona ubaya wa kupeleka ndizi huko anayeelewa anieleweshw
 
Wazanzibari miaka nenda wanapenda uwepo wa Muungano wa changu changu, chako changu! Yaani wao wawe ndiyo wanufaika wakuu wa Muungano.

Kiufupi wana ubinafsi wa kuzaliwa.
 
Duh hii kitu bana....

Kwani kuna sheria inakataza na kama ipo kwanini inakataza ? , Nadhani hayo ndio maswali ya muhimu...

Hayo mambo ya Ujane wake au yeye kuzuiwa kama amezuiwa kadri ya sheria nadhani ni secondary....;
 
Wiki chache zilizopita, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Biashara wa Zanzibar, Shamata Shaame Khamis alitoa ufafanuzi kihusu tukio la kutaifisha tenga za ndizi za mfanyabiashara Veronica Mwanjala aliyekuwa akizisafirisha kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa ajili ya biashara.

Mamlaka kutoka Zanzibar ziliweka wazi kuhusu sheria au kanuni ya katazo la kuingiza ndizi ambalo lipo Kisiwani hapo, ikiwa ndilo lililotumika katika maamuzi ya kuzuia ndizi hizo kuingizwa.

Tangu kutokea kwa tukio hilo ukimya umetawala, lakini upande wa pili mwathirika wa sakata amebaki akiwa na hali mbaya kiuchumi huku akidai kuandamwa na madeni makubwa baada ya mtaji wake kuangushwa.

Huyu hapa anaelezea kilichotokea...

Anakumbushia kilichotokea
“Baada ya kushusha mzigo wangu na wahusika kuushikilia katika Bandari ya Zanzibar, Waziri alikuja akiwa ameongozana na waandishi wa habari akanieleza kuwa Sheria ya Zanzibar hairuhusu kuingizwa kwa ndizi kutoka nje.

“Pamoja na kunielimisha hivyo lakini aliniruhusu kuingiza ndizi hizo kwa siku hiyo tu na kuniambia kuwa kama nitarudia kufanya kosa hilo nitapelekwa Mahakamani kisha jela.

“Alipoondoka huku nyuma mama ambaye ni msimamizi wa mizigo pale Bandarini hakunipa mzigo, aliuzuia na kuniambia wanaupeleka kwa Wafungwa gerezani huku nikitakiwa kulipa faini Tsh. 50,000 niliumia sana kwa kuwa ndio mtaji niliokuwa nautegemea.

“Siku tatu baadaye wakanipigia simu kuniambia niende nikauchukue mzigo niurudishe ulipotoka, lakini kwa kuwa sikuwa na hela ya kulipia gharama za kuusafirisha na hata za mimi mwenyewe tu kujilipia kusafiri, sikufanya hivyo, pia kumbuka zile ni ndizi, kwa siku tatu zilikuwa zimekaa tu pale Bandarini hivyo zikawa zimeshaanza kuharibika.

Kwa nini Zanzibar na matenga yalikuwa mangapi?
“Matenga yalikuwa 30 na si 15 kama ilivyokuwa inasemwa, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwenda Zanzibar kupeleka ndizi.

“Nilikubaliana na watu wenye mahoteli kuwa nitawauzia ndizi moja Tsh. 500. Ningefanikiwa kuuza mzigo wote ungekuwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.15 hivi.

Nini kinaendelea
“Muda mwingi nautumia kitandani nimelala sijui nini cha kufanya, mtaji wangu umekufa, nadaiwa, nilikopa hela ambayo nilikuwa narejesha kila baada ya wiki.

“Hapa nina wiki mbili sijalipa marejesho, nipo katika wakati mgumu, kuna Mbunge mmoja wa Bagamoyo alinipigia simu kwa lengo la kunisaidia, lakini baadaye alipofuatilia akaniambia kuwa amejibiwa kuwa kilichofanyika ni sheria ya Zanzibar na hana njia nyingine ya kunisaidia.

“Wanaonidai kule nilipokopa wanataka kuja kunifilisi maana sina cha kuwalipa na sina cha kufanya, mimi na wanangu hatuna uhakika wa kula kwani mume wangu alishafariki muda mrefu.

“Bado nadaiwa Tsh. 750,000 mpaka sasa na sijui nitailipaje.

“Mwanangu mkubwa anasoma chuo, alizuiwa kufanya mitihani lakini baada Chuo kuona hilo sakata mitandaoni nilienda kuwaomba wakanikubalia mwanangu afanya mitihani kisha nitalipa ada baadaye.

Athari za afya
“Hili suala limeniathiri sana kisaikolojia, tangu wakati huo nimekuwa nashinda ndani muda mwingi, nguvu zimeniisha japo mimi ni mpambanaji, nahisi akili yangu haipo sawa.

Wito kwa Serikali
“Namuomba Rais Samia na Serikali yake kwa jumla anisaidie kwa kuwa mimi siombi msaada nikiwa nimekaa bali nina hali mbaya kiuchumi, nina nguvu ya kufanya kazi, ni mjane ninayepambana, lakini matukio kama haya yanakatisha tamaa.

“Ombi langu kwa Serikali ni kuwa kwa watu tunaojituma kama mimi, ambao hatujaingia kwenye shughuli ya kujishushia heshima, basi tutengenezewe mazingira ya kutusaidia.

“Nilipeleka ndizi Zanzibar kwa kuwa niliamini ni biashara yenye faida, kama ni changamoto ya magonjwa ya mimea nadhani mkemia mkuu wa Serikali angeweza kufanya kazi yake kupima kama kweli hazina ubora.”

Pia soma: Zanzibar: Serikali yazuia Mazao ya Ndizi kutoka nje, ndizi za Veronica Mwanjala kuharibiwa ili kuzuia Magonjwa
Pole sana mama ,
Hii ndio atahri ya kutokuwepo kwa mfumo usio eleweka wa muungano.
Hata sisi Tukileta sukari huko Bongo tunataifishwa.
Tunaambiwa ni marufuku kuleta sukari Tanzania Bara kutoka Tanzania Visiwani.
HUU NDIO MFUMO ULIOWEKWA NA CCM WA MUUNGANO WETU.

JIUNGE NA GURUDUMU LA KUDAI KATIBA NA MABADILIKO YA MFUMO.
 
Wanashindwa nini kujitawala kwa 100%? Wamefungwa mikono na miguu?

How come nchi ina serikali yake, mipaka yake, wimbo wake wa Taifa, Rais wake, Bunge lake, wananchi wake, nk. Halafu ikaliwe kijeshi na nchi nyingine?

Siyo kwamba asali wanayolambishwa miaka nenda na serikali ya ccm, ndiyo inawasababisha kushindwa kuchukua maamuzi sahihi ya kujitawala?
Una umri gani? Tuanzie hapo kwanza, isije ikawa tujadiliana na watoto wa chekechea hii mada iko juu ya uwezo wao wa kufikiri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom