Zanzibar na ndizi za mjane!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,335
24,232
Kama kuna habari inakera, kufedhesha na kutia hasira wiki hii ni jinsi serikali ya Zanzibar ilivyoshughulikia suala la ndizi za mjane aitwaye Veronica Mwanjala.

Kosa la Veronica ni kupeleka ndizi Zanzibar ili ajikimu kimaisha yeye na watoto wake. Kilichotokea pale bandarini ni maelezo yanayo ashiria hisia za kibaguzi dhidi ya watu wa Bara.

Tunaambiwa eti Veronica ndizi zake hazihitajiki soko la Zanzibar, mara zina vidudu, mara hazina vibali, na faini ya elf 50 juu!

Suala hili ni dogo lakini limeleta hisia za kibaguzi kutoka kwa wazanzibari, tena serikali, dhidi ya Watanzania bara.

Wote tunaelewa jinsi wazanzibari na wapemba wanavyovumiliwa kwa mengi hapa Bara na hawachukuliwi kama raia wa nje kama ipasavyo.

Mnaya zaidi serikali ya Zanziba na waziri wake wamemfanyia uharamia mama mjane!

Hili halikubaliki!

Mwenye namba ya Veronica Mwanjala atupatie ili JF tuanze mchango wa kurejesha mtaji wa huyu mama aliyedhulumiwa.
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar naumithilisha na ndoa ya baina ya mwanaume (Tanganyika) na Mwanamke (Zanzibar) ambapo mwanaume ndio anaforce mahusiano na mwanamke ikiwa mwanamke hataki kuwa katika hiyo ndoa. Hatima yake sasa ni ndugu wa mume kudhalilishwa na upande wa mwanamke, mwanamke kujiona bora zaidi ya mwanaume.

Huu muungano umekaa kinafiki sana, ni wakati sasa kila mtu akashika hamsini zake tujue ni nchi mbili tofauti tu. Kuliko haya manyanyaso na kudhalilishana kunakofanywa na wazanzibari dhidi ya watanganyika.

Mtanganyika akiwa zanzibar anachukuliwa kama takataka lakini wenyewe huku wanajiachia bila bughudha yeyote.
 
Kama kuna habari inakera, kufedhesha na kutia hasira wiki hii ni jinsi serikali ya Zanzibar ilivyoshughulikia suala la ndizi za mjane aitwaye Veronica Mwanjala.

Kosa la Veronica ni kupeleka ndizi Zanzibar ili ajikimu kimaisha yeye na watoto wake. Kilichotokea pale bandarini ni maelezo yanayo ashiria hisia za kibaguzi dhidi ya watu wa Bara.

Tunaambiwa eti Veronica ndizi zake hazihitajiki soko la Zanzibar, mara zina vidudu, mara hazina vibali, na faini ya elf 50 juu!

Suala hili ni dogo lakini limeleta hisia za kibaguzi kutoka kwa wazanzibari, tena serikali, dhidi ya Watanzania bara.

Wote tunaelewa jinsi wazanzibari na wapemba wanavyovumiliwa kwa mengi hapa Bara na hawachukuliwi kama raia wa nje kama ipasavyo.

Mnaya zaidi serikali ya Zanziba na waziri wake wamemfanyia uharamia mama mjane!

Hili halikubaliki!

Mwenye namba ya Veronica Mwanjala atupatie ili JF tuanze mchango wa kurejesha mtaji wa huyu mama aliyedhulumiwa.
Wazo zuri, tuwajali wajane.

Usisahau pia kumhurumia mjane wa Mh Magu unayemtukania aliyekuwa mumewe Kila kukicha.
 
Nasema tu, tukianza kuwakazia wazanzibari kuja na vikorokoro vyao huku bara sijui itakuwaje: kuna majitu yana roho mbaya sana
Hawa watu wana shida mahali! Siyo bure. Miaka nenda wenyewe wanataka Muungano wa kuwanufaisha wao tu.

Nitafarijika sana siku watakapo jitegemea kwa 100%, na hivyo Tanganyika nayo kuondokana na huu mzigo wa kuwabeba watu wasio na faida.
 
Back
Top Bottom