Mjali mama kijacho wako

Mjali mama kijacho wako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,061
Reaction score
79,418
MJALI MAMA KIJACHO WAKO

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Hakikisha unauhakika Mimba ni yako. Usiwe mpumbavu.
Kitendo cha kuhakikisha Mimba ni yako ndio kujali kwenyewe

2. Mpe Maneno matamu mama kijacho wako

3. Msaidie kazi za nyumbani au mtafutie Msaidizi wa Kazi hapo Nyumbani

4. Hakikisha anakula mlo Kamili( balance diet)

5. Fanyeni kwa pamoja mazoezi madogomadogo kulingana na Hali ya ujauzito wa mama kijacho wako.

6. Hakikisha anakunywa Maji ya kutosha kulingana na maelekezo ya wataalamu

7. Muogeshe mama kijacho wako hasa Mimba ikiwa Kubwa

8. Mkatie Bima ya afya tangu Mimba ikiwa changa ili imsaidie wakati wa kujifungua

9. Wekeni utaratibu wa maombi kila siku tangu siku ya Kwanza ya Mimba Mpaka siku ya mwisho akijifungua.

10. Nunueni vifaa vya kujifungua na vya mtoto kidogokidogo kujiandaa na tukio kubwa zuri la kumpokea mtoto.

11. Usimgombeze Mama kijacho lakini hiyo haimaanishi mwanamke akupelekeshe kwa kisingizio cha Mimba.
Mwanamke anaowajibu wa kukuheshimu wakati wote angekuwa na Mimba ya mapacha Saba.

Hakunaga kisirani cha Mimba. Huo ni utapeli na utovu wa Nidhamu kwa baadhi ya wanawake wasio na Adabu

12. Hakikisha mnaishi vizuri na mama kijacho wako ili mtoto akizaliwa awe na utulivu wa Kihisia na kiakili

13. Epuka Washauri ambao sio wataalamu wa mambo ya kina mama wajawazito.

14. Epuka Imani za kishirikina.

15.. Mpeleke Mama kijacho Kliniki awamu zote zinazohitajika.
Usimuache aende pekeake.

Omba ruhusa kazini ukifika Kliniki watampa Mkeo kipaombele mtawahi kuondoka.


Acha nipumzike sasa


Robert Heriel Tz
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hapo inabidi upige hesabu za umri wa mimba na mzunguko wa siku zake. Kama hesabu zinaenda sawa subiri ajifungue kwa ajiri ya hawamu ya pili ya uhakiki
Huo mda sina kwangu mtoto ni mtoto tu .
 
Back
Top Bottom